Wito wangu kwa wanandoa na wenye mamlaka!

AbuuMaryam

JF-Expert Member
Dec 26, 2015
2,537
4,517
بسم الله الرحمن الرحيم.

Mimi ni mwalim wa dini na imam katika msikiti ulipo eneo ninalo ishi...

Kwa nafasi yangu huwa napokea kesi na migogoro mbalimbali kusuluhisha na kushauri.

Nina wito huu kwa wanandoa wa dini zote na mamlaka zote zinahusika na masuala ya ndoa na muunganiko wa kijamii;

1. Mke na mume. Mapenzi ni kama kiumbe chochote kile...Huzaliwa, hukua, hustawi na mwishoni hupata maradhi(ambayo ndio migogoro ya ndoa) na mwishoe hufa kabisa.

2. Chondechonde wanandoa...Usikubali wala usilazimishe kuishi na mtu ambae wazi anaonekana hakupendi tena kwa ishara zote atakazokuonesha kuwa hakupendi bila shaka...Au usiishi na kuforce kuishi na mtu ambae humpendi.

3. Kwakuwa ndoa iliasisiwa na mapenzi. Basi yanapoisha mapenzi...Na ndoa vilevile haina kazi tena...

4. Watoto wasitumike kama sababu ya kulazimisha watu wasiopendana waishi pamoja, hao watoto walikuja kwa wakati wao, wakakuta watu wamependana ndipo wakapatikana wao...Watoto hawakuwa chanzo cha wazazi wao kukutana. Wamekuja baadae. Kwahiyo wasitumike kama sababu ya kulazimisha mapenzi yaliyokufa.

5. Ukiona humpendi mtu tena kama unaweza na unamuamini anaweza kuhimili utakapomwambia kuwa humpendi. Basi mwambie. Kama huwezi. Potea kabisa kwenye upeo wa macho yake. Kwa kipindi kidogo ili azoee kuishi bila wewe.

6. Ukiona unampenda mtu lakini yeye hakupendi tena... Kubali...Ndio maisha...Nyanyuka hapo...Pukusa makalio yako...Piga hatua moja mbili tatu...Songa mbele maisha yanaendelea... Kila lenye mwanzo halikosi mwisho .

Kwa sababu mapenzi ni kama daladala. Siti uliyokalia leo. Alikalia mtu jana. Hivyo kesho atakalia mtu mwingine...Haya ndio maisha.

7. Hukuzaliwa na mtu...Kiasi kwamba kwakuwa umependana na mtu kwenye maisha yako...Basi kutengana lazima iwe ni kifo...La hasha...Kwa sababu kabla yake huyo mtu unayempenda uliishi vizuri tu bila tabu...Iweje iwe tabu baada yake ..Kubali songa mbele utapata mwingine. Naye utaachana nae utaenda kwa mwingine...Ndio maisha...

8. Inapotokea unamfuatilia mwenza wako. Jipime na ujikadirie. Hayo unayoyafuatilia utakapoyaona unaweza kustahamili...? Yaani kwa mfano ukigundua mkeo anachepuka. Unaweza ukafanya maamuzi ya kumuacha? Kama huna uwezo huo unafuatilia ya nini? Kubali kuwa mume zoba upate unachokusudia...Ila kama ukifuatilia ukagundua anakusaliti ..Unaweza kumuacha. Achana nae tupa kule.

9. Usikubali kufa, kudhurika wala kubeba dhambi ya kuua mtu bure, wala dhambi ya kudhuru mtu ambae hata hujui kitovu chake kilidondokaje...Huo ushetani...Uzuzu Upoyoyo...Upumbavu na ujinga wa hali ya juu.

10. Ukiona umefumaniwa live na mwenzio. Ule msamaha unaopewa baada ya fumanizi usiuamini kamwe...Na wewe songa mbele endelea maisha na huyo uliyefumaniwa naye.

Ukiona eti nimekusamehe. Ujue ni bomu la kisasi linaandaliwa kwa ajili yako...Usirudi nyuma. Utajutia milele.

11. Polisi, mahakama, bakwata, mabaraza ya usuluhishi katika taasisi zote za kidini. Jamani linapokuja kwenu gogoro lolote la ndoa baina ya wanandoa.

Msiwarudishe wakayazungumze au kuwalazimisha waendelee kuishi pamoja hali ya kuwa bado wana migogoro...Tena wasaidieni hata kuwatenganisha kwa muda au hata milele panapobidi.

Kwa sababu mpaka limefika kwenu. Ujue wao binafsi limewashinda ..

Na huku mkijulisha vyombo vya usalama ili kufuatilia usalama wa baina ya wanandoa ili wasije leteana madhara wenyewe kwa wenyewe.

Mwisho;
Tusisahau kuwa sisi ni binadamu watu...Tuwe na roho za kiutu...Tusiendekeze za kishetani kudhuriana kisa...A mere thing eti "Nampenda" eti "Amenisaliti"!.
 
Wewe sheikh gani unahamasisha Halali inayomchukiza Mungu. Dini zimeingiliwa sana hizi
 
Ukiona message hujaielewa...basi JUA HUJAANDIKIWA WEWE...KIFUPI "HAUKUHUSU...!"
Kiongozi gani wa dini huna subra, hekma na busara. Hivi mitume na maswahaba wangekosa subra, hekma na busara uislamu ungekufikia wewe na mimi?
 
Mchezo gan huo wa kuangaliana hadi kugaaa. Dah anyway tuwaachwe wapunguzane kama ndo maidha wanayataka hivyo
yule kayataka mwenyewe.. sijui hakuwaza kama ana watoto (ubinafsi ni asili yao), hujiwazia wao pekee..
 
Wewe sheikh gani unahamasisha Halali inayomchukiza Mungu. Dini zimeingiliwa sana hizi
Kwenye dini yetu hakuna kilicho halali kinachomchukiza allaah...

Hizo ni za vijiweni labda...Ila uislaam kila kilicho halali kinapendeza kwa allaah...Allaah hawezi halalisha analolichukia kamwe...
 
Kiongozi gani wa dini huna subra, hekma na busara. Hivi mitume na maswahana wangekosa subra, hekma na busara uislamu ungekufikia wewe na mimi?
Kila kitu na mahala pake ..Subra ina mahala pake ..Hekima na busara zina mahala pake...

Dini ya kiislaam kila kitu na mahala pake...

Dini haitaki uwe zoba, zuzu na mjinga...Eti kisa subra, hekima na busara...

Kuna wakati unamjibu mtu vile alivyokuja...Na hiyo ndio hekima yenyewe ..

Hata kumchapa mtoto bakora ndio hekima yenyewe...

Nyie mwatafsiri hekima na busara kuwa ni uzoba na uzuzu..
 
Lakini kwa mujibu wa Qruan mwana ndoa anaye fanya uzinzi adhabu yake ni kifo kwa kupigwa mawe na sikuachana.
 
Lakini kwa mujibu wa Qruan mwana ndoa anaye fanya uzinzi adhabu yake ni kifo kwa kupigwa mawe na sikuachana.
NDIO SAHIHI...ILA HIYO ADHABU ITATOLEWA NA KIONGOZI NA UTEKELEZAJI WAKE UTASIMAMIWA NA KIONGOZI AMA SERIKALI...

SIO MIMI NA WEWE KUJIAMULIA TU UOKOTE MAWE UPIGE MTU MPAKA KUFA...UISLAAM HAUELEKEZI HIVYO...NA UKIFANYA HIVYO UTAKUWA UMEUA DHAMBI YA KUUA.
 
wanandoa mnatutisha sana sisi ambao bado hatujaoa :):)
🤣🤣Wameyafanya maisha ya ndoa kuwa magumu sana,Kama kusomea digrii ya udaktari wa kufanya upasuaji wa ubongo 🤣btw unawezaje kwenda kumweleza mtu baki matatizo yenu mnaoishi na kulala kitanda kimoja?Kama nyie mnaojijua in and out mmejishindwa,yeye mtu baki ataweza kweli?
 
Ukiona message hujaielewa basi jua hujaandikiwa wewe.. YANI HAIKUHUSU
"@!bra_maino...
 
Back
Top Bottom