Aina za majini na kazi zake

Aina za majini na kazi zake

Hakuna haja tena ya kutoa tafsiri ya majini kwakuwa tayari tumeshalidajili hili kwenye post iliyopita kwamba majini ni viumbe roho waliofukuzwa toka mbinguni na kutupwa ulimwengu wa giza.

Mada hii ni maalum kwa ajili ya kutambua aina za majini na kazi zake
Kuna wakati katika jamii unaweza kumshangaa mtu au hata kugombana naye kutokana na tabia zake na mambo yake huyu si wa kulaumu sana saa nyingine si yeye bali ni jini, hata hapa JF tunao wengi tuu.

Kimsimgi wapo majini tofauti tofauti zaidi ya 60 lakini kazi zao kwa sehemu kubwa zinaingiliana hivyo nitaweka baadhi tu ambayo kwa kiasi kikubwa ndio hubeba mambo mengi fuatana nami.

1. SUBIANI - hili ni jini linalosababisha ajali na lenye kuzuia hedhi kwa mwanamke, lina penda sana damu hasa hiyo ya hedhi.

View attachment 342303

2.MURAFARI- hili ni jini la kuzuia mafanikio ya kimaisha kielimu na hata kipato, ukitupiwa hili jini utahangaika sana na maisha.

3.LATIFU- jini la mateso ufukara na matumizi ya hovyo unakuwa ni mtumwa wa kupata kupoteza na kutumia bila tija.

4.JAHARI-jini jizi la biashara, unafanya Sana biashara lakini huoni ustawi wala mafanikio yoyote.

View attachment 342305

5.HASINANI- Jini la fujo ulevi wa kila aina bhangi sigara madawa pombe nk

6.JUBE- Jini la utasa, hili unaweza kutupiwa tu na mbaya wako au ukiwa mtoa mimba au mpiga puchu mahiri.

7.RUYATI- ndoto mbaya, ukiacha ndoto maono au ndoto ujumbe , hizi ndoto za kutisha husababishwa na jini ruyati.

8.TAJARUNI-hili ni la utajiri wa masharti ya kutoa kafara la ndugu na kufanya ngono na mzazi au mwanao.

9. WAIDADAT- jini linalomfanya mwanaume aige mambo yote ya kike kuanzia tabia mpaka mavazi.

View attachment 342307

10. ALIBADIRI- Ukitupiwa hili kwa sababu yoyote ile hasa kutenda uovu huponi.

11.ANZURA -kuzuia ndoa hasa kwa wanawake, utakuta binti mzuri kakamilika kila idara lakini anaishia kuposwa tuu.

12.MAIMUNA- jini mfarakano wa kuleta magomvi kwenye ndoa hatimaye kuvunjika.

13 . MAKATA- Jini makata ni noma hili likiingia kwenye familia au ukoo basi vifo vitafululiza mpaka mbaki wachache kabisa.

View attachment 342306

14.TARIK- jini hili hufarakanisha marafiki watu wanaofanya biashara pamoja kwenye vyama nk nk..likishaingia mahali hili lazima kinuke.

15. JINI WIVU KIJICHO NA ROHO YA KWANINI-hili bwana hili popote litakapoona new post ni mtu fulani sikilizia mashambulizi yatakayofuata.

[emoji15] [emoji15] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Katika mambo yote hayo hakuna jini lolote linalofaidika na chochote bali kumletea shida mwanadamu ili afarakane na mola wake
Kumbuka kuna majini ya kutupiwa kutumwa na yale yanayofanya kazi yenyewe kwa utashi wao.

==========================
NB: Picha zimewekwa ili kuleta uhalisia zaidi ingwa zinaweza zilihusiane moja kwa moja na Majina ya viumbe hawa.
Mkuu Mshana Jr!
Ukimaliza kutaja aina ya majini na Kazi zake! Usisahau basi na Aina za Malaika na kazi zake!
 
Majini ni fixed false idies ( attitudes ) ambayo ipo ndani ya ubongo wa mwanadamu.Hakuna binadanu yeyote duniani anaeweza kumwona na kumgusa jini wala jini haliwezi kuishi ndani mwili wa binadamu kwa sababu hakuna "hollow space"yaani uwazi ambao utaruhusu liingie na kukaa ndani ya mwili wa binadamu.Watu wote wanaopatwa na hali hiyo ya kuwa na majini huwa wamepatwa na magonjwa ya akili na moja ya brain center hua imeathirika.Wagonjwa au watu wanaopandisha mashetani au mapepo hua wamepata tatizo la kiakili lijulikanalo kama "double man personallity psychosis." Halafu kuna wale wagonjwa wanaona vitu au viumbe vinawajia mbele na wakati mwingine wanaweza kukimbia na kupiga kelele wakihofia viumbe wanaowana mbele yao.Wakati wakifikwa na hali hiyo watu wengine waliokuwa karibu nae hawaoni kitu chochote.Kwa kifupi mgonjwa huyu nae hua amepatwa na matatizo kwenye ubongo wake na hiyo hali kiutaalamu inaitwa " hallucinations "Kwenye ubongo kuna brain centers nyingi na kila moja inakuwa na kazi yake.Majini saba yanasemwa yaweza kuwa ni moja tu ya brain centers ambazo hutafsiriwa na watu ambao hawana elimu ya jinsi mwili wa binadamu ulivyo yaani " anatomy "na jinsi mwili huo unavyofanya kazi kikawaida "physiology."Pia watu hao hua hawana elimu ya ni jinsi gani magonjwa yanamwingia binadamu na kuleta shida yaani "pathology."Kutolea mifano kwenye vitabu vitakatifu vya biblia na quran kuwa Yesu au Mtume alikemea au kukimbiza mapepo kutoka kwenye miili ya watu hakuwezi kuwa kigezo kuwa kweli majini au mapepo yanaweza kukaa na kutulia tuli ndani ya kichwa cha binadamu wakati majini yenyewe ni makubwa kama huyo mtu !!.Vifungu vya Quran au Biblia ni vitabu vinavyosimulia maisha ya watu wakale (mambo ya walawi) ambao walikuwa ni binadamu kama sisi na pia walipungukiwa na elimu ya sayansi ya binadamu kama tulivyo sisi.Hizi attitudes za mashekhe kutafisiri aina ya majini ni POROJO za duniani tu.
Pumba tupu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakika upo sahihi mkuu
Nadhani haya anayofanya ni elimu nzuri na si dhambi kuijua na ndio maana Mwenyezimungu katika kitabu chake kitukufu akatuletea sura nzima sura til JINN ili tuwajue, vizuri tabia zao na makosa n.k., hata wewe ulijua kama walilaaniwa sabab Qur'an imekwambia, kwahiyo kuwafahamu kwa undani si dhambi na wala hakuna ubaya, Na aliekwambia kama wote wachafu ni nani?? TAFUTA SHEIKH AKUFAFANULIE Kuna aya inasema "Sikuwaumba majini na watu ila tu waniabudu" kwa taarifa yako kuna majini wanamuabudu Mwenyezimungu na kumuogopa na wapo majini wataingia motoni na wa peponi watakuwepo, NA NI NANI AMEKUDANGANYA KUNA SHETANI, kuhusu ushetani hata binadamu anaweza kuwa shetani kuna mipaka sisi binadam na majini tukivuka tunaingia kweney ushetani, shetani si kiumbe kama uanvyodhani, SHETANI HATA WEWE WAWEZA INGIA KWENYE USHETANI KUTOKANA NA MAASWI UTAKAYOFANYA, Jini ni kiumbe kama sisi ameumbwa na atapotea, na wataingia motoni na wapo wa peponi, Enzi za Mtume Mohammed (S.A.W) Alikuwa anakaa akiwafundisha Qur'an na kuwaslimisha (TAFUTA SHEIKH UKAMUULIZE KUHUSU HILI) Na je Nabii Sulyeiman je umati wake ulikuwa ni wakina nani? Na alipewa uwezo gani? Hii ni Elmu kama ELIMU NYINGINE UKIONA HAINA MANUFAA KWAKO, IPOTEZEE, ILA SIDHANI KAMA KUNA UBAYA UKAWAJUA ZAIDI TABIA ZAO HAO WA UPANDE WA PILI, MANA SI DHAMBI KUWAJUA.

Pinga hoja kisomi. Unaonekana umeishia darasa la 7, au form 4 dvn 4
Huoni hata aibu kupinga hoja bila kuwa na hoja ndugu?
Naww unajuita great thinker ha ha ha.
Kwa ulivyoipinga hoja ya jamaa mpaka nimesikitika sana yaan umeipinga kidarasa la 7.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] anaitwa baro kaitohoa kwa kiingereza ni barrow

Jr[emoji769]
 
Je huyu naye ni jini?
FB_IMG_1638167878789.jpg
 
Somo zuri.
Baadhi ya Vijana wa Kiume wa kisasa wamepagawa na
Jini Waidadat
Linalo pelekea kufanya mambo ya Kike na Ushoga.

Mada zako Kwa wanaojitambua ni nzuri sana.
Zinatufundisha madhara ya ulimwengu tusiouona na namna ya kukabirina nao.

Niliongea Juzi kuwa madhara yanayosababishwa na kupagawa na Majini kama Kuupenda Ushoga dawa yake sio ushauri, bali kulikemea hilo Jini inalosababisha hiyo tabia, ili limtoke mwathirika husika.
Na njia ya kuyaondoa hayo Majini zimeeezwa kwa ufasaha humu.

Matatizo yanayosababishwa na kukaliwa na Majini yanazidi kuikumba jamii yetu ya sasa.
Hatuna namna zaidi ya kuikabili kikamifu.

Watu mnaomkebehi mtoa Mada mshana, naomba muwe na Busara japo kidogo Tu.

Kama nyinyi ni wema Sana na hamwezi kusumbuliwa na Majini basi mtupushe sisi wenye dhambi tunaotaka kukabiliana na Majini wanaotusumbua kila kukicha.

KAMA MADA HAIWAHUSU KAENI KIMYA.
HATUTAKI KUMKATISHA TAMAA MWALIMU WETU MSHANA.

HILI LICHUKULIWE KAMA ONYO LA MWISHO.
 
HILI LICHUULIWE KAMA ONYO LA MWISHO.
Niliongea Juzi kuwa madhara yanayosababishwa na kupagawa na Majini kama Kuupenda Ushoga dawa yake sio ushauri, bali kulikemea hilo Jini inalosababisha hiyo tabia, ili limtoke mwathirika husika.
Na njia ya kuyaondoa hayo Majini zimeeezwa kwa ufasaha humu.[emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545]
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom