Aina za majini na kazi zake

Aina za majini na kazi zake

Huyu Jamaa anataka kuwaona Majini? Mwambie achukuwe Matı-ongotongo ya Mbwa mweusi ajipake kwenye macho yake atawaona Majini lakini akishawaona majini anawezakuwa ni Mwendawazimu shauri yake Majini yanatisha sana. kama hauko Strong aka Huna nguvu ya kukabiliana nao usijaribu hiyo dawaunaweza kuwa mwendawazimu.

nitafanya utafiti
 
Hakuna haja tena ya kutoa tafsiri ya majini kwakuwa tayari tumeshalidajili hili kwenye post iliyopita kwamba majini ni viumbe roho waliofukuzwa toka mbinguni na kutupwa ulimwengu wa giza.

Mada hii ni maalum kwa ajili ya kutambua aina za majini na kazi zake
Kuna wakati katika jamii unaweza kumshangaa mtu au hata kugombana naye kutokana na tabia zake na mambo yake huyu si wa kulaumu sana saa nyingine si yeye bali ni jini, hata hapa JF tunao wengi tuu.

Kimsimgi wapo majini tofauti tofauti zaidi ya 60 lakini kazi zao kwa sehemu kubwa zinaingiliana hivyo nitaweka baadhi tu ambayo kwa kiasi kikubwa ndio hubeba mambo mengi fuatana nami.

1. SUBIANI - hili ni jini linalosababisha ajali na lenye kuzuia hedhi kwa mwanamke, lina penda sana damu hasa hiyo ya hedhi.

View attachment 342303

2.MURAFARI- hili ni jini la kuzuia mafanikio ya kimaisha kielimu na hata kipato, ukitupiwa hili jini utahangaika sana na maisha.

3.LATIFU- jini la mateso ufukara na matumizi ya hovyo unakuwa ni mtumwa wa kupata kupoteza na kutumia bila tija.

4.JAHARI-jini jizi la biashara, unafanya Sana biashara lakini huoni ustawi wala mafanikio yoyote.

View attachment 342305

5.HASINANI- Jini la fujo ulevi wa kila aina bhangi sigara madawa pombe nk

6.JUBE- Jini la utasa, hili unaweza kutupiwa tu na mbaya wako au ukiwa mtoa mimba au mpiga puchu mahiri.

7.RUYATI- ndoto mbaya, ukiacha ndoto maono au ndoto ujumbe , hizi ndoto za kutisha husababishwa na jini ruyati.

8.TAJARUNI-hili ni la utajiri wa masharti ya kutoa kafara la ndugu na kufanya ngono na mzazi au mwanao.

9. WAIDADAT- jini linalomfanya mwanaume aige mambo yote ya kike kuanzia tabia mpaka mavazi.

View attachment 342307

10. ALIBADIRI- Ukitupiwa hili kwa sababu yoyote ile hasa kutenda uovu huponi.

11.ANZURA -kuzuia ndoa hasa kwa wanawake, utakuta binti mzuri kakamilika kila idara lakini anaishia kuposwa tuu.

12.MAIMUNA- jini mfarakano wa kuleta magomvi kwenye ndoa hatimaye kuvunjika.

13 . MAKATA- Jini makata ni noma hili likiingia kwenye familia au ukoo basi vifo vitafululiza mpaka mbaki wachache kabisa.

View attachment 342306

14.TARIK- jini hili hufarakanisha marafiki watu wanaofanya biashara pamoja kwenye vyama nk nk..likishaingia mahali hili lazima kinuke.

15. JINI WIVU KIJICHO NA ROHO YA KWANINI-hili bwana hili popote litakapoona new post ni mtu fulani sikilizia mashambulizi yatakayofuata.

[emoji15] [emoji15] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Katika mambo yote hayo hakuna jini lolote linalofaidika na chochote bali kumletea shida mwanadamu ili afarakane na mola wake
Kumbuka kuna majini ya kutupiwa kutumwa na yale yanayofanya kazi yenyewe kwa utashi wao.

==========================
NB: Picha zimewekwa ili kuleta uhalisia zaidi ingwa zinaweza zilihusiane moja kwa moja na Majina ya viumbe hawa.
Wewe una cheo gani katika majini?
 
Ndugu wana jf, Habari, Humu tunaelimika sana, tena sana, Matusi Na Kashfa sio mahala pake, Kama MTU huamini kitu njoo Na hoja, Kuna watu tunajifunza mengi Kupitia Huyu huyu mshana, japo hatujawa wepesi kutoa maoni, ila ukweli tunafaidika sana, Kama mtu ukinyamaza ILi wenye hoja Waje Utapungukiwa na nini?
Mungu anatufikia kwa njia /Namna nyingi sana. Elimu hii ni nyeti sana, imebeba Chanzo cha nguvu ya maisha.
 
Asante sana JOSEPH555...vumilia tu kama utaitwa msukule
 
Ni mpaka likushike na uambiwe ndio utajua hivi hivi ni ngumu japo kuna watu walishawahi kuniambia humu kuwa nimetupiwa jini la kupenda mambo ya kishirikina...
Niliambiwa Nina subiani Na sifa zake mbona Sina naenda mwezini as usual with a good flow sema Sasa nimeambiwa n mjeuri Na hapandi kixhwani Na sjatupiwa amependa mwenyewe kiti sielewi Kwa kweli
 
Kwa nini majini hayo umeleta kwa majina ya kiarabu? Je wachawi wazungu, waamerika, wakichina majini yao nayo ni aina gani? Je ana wao wanazungumza kwa lugha gani? mshana jr
 
We jamaa aise km nikiishi karbu na ww naweza ama hata kbla kodi kuisha au km nmejenga,ntaama,hivyohivyo,maana stori zako nazisomaga alafu naota ndoto,za kutisha
 
Niliambiwa Nina subiani Na sifa zake mbona Sina naenda mwezini as usual with a good flow sema Sasa nimeambiwa n mjeuri Na hapandi kixhwani Na sjatupiwa amependa mwenyewe kiti sielewi Kwa kweli
Kumbuka hili. '....umeambiwa...'
 
Kwa nini majini hayo umeleta kwa majina ya kiarabu? Je wachawi wazungu, waamerika, wakichina majini yao nayo ni aina gani? Je ana wao wanazungumza kwa lugha gani? mshana jr
Kwakuwa nimeandika kiswahili, ningeandika kichina kispaniola au kikhosxa hakika majina yasingekuwa haya
 
We jamaa aise km nikiishi karbu na ww naweza ama hata kbla kodi kuisha au km nmejenga,ntaama,hivyohivyo,maana stori zako nazisomaga alafu naota ndoto,za kutisha
[emoji87] [emoji87] [emoji87] [emoji3] [emoji3] [emoji13] [emoji13] [emoji13]
 
Kwakuwa nimeandika kiswahili, ningeandika kichina kispaniola au kikhosxa hakika majina yasingekuwa haya
Sawa lakini asili ya majina ni kiarabu. Kwa mfano Ahmed, hata ikiandikwa kichini asili yake, matamshi yake inabaki kuwa ya kiarabu.
 
Mshana Jr nilikuuliza; Je Mtu aweza kurogwa Na Mtu zaidi ya mmoja? Yaani mfano Watu watatu kila Mtu Kwa namna Na wakati waje wanaweza mroga Mtu mmoja? Au Yule wakwanza aliyeanza ndiye peke Yake uchawi wake utafanya kazi Na wa Hawa wengine utadunda?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom