Aina mpya ya ujambazi

Mbinu nyingine ambayo wameifanya mtaani kwetu, ilikuwa kwamba siku hiyo kulikuwa na mkutano wa mtaa na mwenyekiti wa mtaa akawa amesisitiza kuwa vijana na wanaume walio nguvu sio wazee watatakiwa kuweka mpango madhubuti wa kufanya doria usiku. Siku hiyo hiyo baada ya kikao hicho wezi wakatunga mbinu, wakaenda kwenye nyumba ya mtu, wakamgongea kijana wao dirishani maana hiyo nyumba haina fensi (sijui walijuaje dirisha la kijana yule), wakaanza kumfokea "YAANI WEWE UMELALA NDANI MUDA HUU, INA MAANA HUTAKI KUFANYA DORIA NA HALI LEO MWENYEKITI WA MTAA ALISISITIZA KUWA TUFANYE DORIA? TOKA NJE" yule kijana akatoka. Alivyotoka wakamuuliza mko wangapi humu? kijana akasema idadi. Mwamshe baba yako haraka (ilikuwa mbinu wajue kama baba yupo au hayupo). kijana akajibu kuwa baba yuko safari yuko mama tu. wakamwambia amwamshe mama yake. Yule mama alivyofika na yeye wakaanza kumfokea kuwa kwanini vijana wake hawaenda doria. Wanasema hao wezi mmoja wao alivaa suruali kama ya polisi. Basi wakamwamrisha mama afungue mlango waingie ndani, wakaingia ndio wakaanza kumpiga na mabapa ya mapanga, waliiba laki nne, mfuko wa sukari, tv flat screen.
Nashkuru Mkuu wa ushuhuda huu
 
Kuna ile style yao nyingine ya kufungulia maji.Wanachokifanya ni kwamba kama nyumbani kwako una bomba nje, jamaa wanakuja usiku wanafunguliua maji mpaka mwisho,sasa wewe jifanye kiherehere utoke nje kwenda kuyafunga......hapo ndo utajua kwanini Idd Amini Nduli anaitwa dada.Ni bora uyaache yamwagike bili isome mtapambana na mamlaka ya maji muda wa bill ukifika.
Ukiona ii kitu inatokea,funga milango yote afu zima taa zote za ndani, zibaki za nje,
unawamulika tu, ao ao,.. Usitoke ita polisi,
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom