Kuhusu gharama uliyotaja naamini ndivyo ilivyokuwa imekadiriwa. Msemaji mmoja wa AICC alisema na kutoa maelezo yanayofanana na yako alipohojiwa kwenye TV. Na aliyataja kwa majina hayo makampuni ya nje na nchi yaliko.
Huu utata unaojitokeza sasa, kweli unastaajabisha na naanza kuamini madai yako yanaweza kuwa kweli.
Kazi nzuri bwana socrates.
.
Tusubiri kuona kama ripoti ya Mkaguzi Mkuu itaonesha jambo lolote.
Tutegeme lini hiyo Report, maana waswahili wanasema ngoja ngoja humiza matumbo, au ngoja ngoja utakuta mtoto si wako kama ni muda mrefu toka sasa , then wanatakiwa wafanye special audit.
na Hivi hawa watu wa wa Arusha/Meru wanamjaribu Raisi ili wakichukuliwa hatua waseme JMK ana uadui nao aU? Maana Kwenye Mwananchi kuna issue ya Severe kukaa hotelini kwa miezi 9 sasa kisa anasubiri nyumba inayo karabitiwa, cost so far ni 9million, ambayo ingetosha kukodisha nyumba sema 1mill a month. Kisa hakuna fedha za ukarabati, lakini za Hoteli Zipo?
Hivi kuna connection yoyote kati ya Kaaya - AICC na Kaaya ya DAWASCO?
Connection ipo through EL
AICC ilikuwa inaendeshwa kifisadi tangu enzi za Lowassa. ni Idara nyingine yenye mauza mauza katika nchi yetu..hili halinishangazi hasa ukizingatia kuwa Kaaya ana malengo ya kugomea mbunge 2010 kupitia ccm. Katika kura za maoni 2005 alikosa kwa sababu za kinithamu lakini amepania 2010 kurekebisha..huenda ndio anajikusanyia mtaji wa kampeni hivyo.
Well,this is getting nastier!Jamani kwenye huu uchunguzi msimsahahu huyu Bwana anaitwa Tsavo maana aliingia AICC hana kitu sasa hivi ana majumba kadhaa,magari na hata petrol station jamani kazitoa wapi hizi?
Huyu Kaaya amekuwa anafanya mabo jinsi anayojisikia. Ameweza hata kupandisha kodi za nyumba za AICC kwa asilimia mia moja na hajataka hata kukutana na wapangaji ili hata kutoa maelezo kwa nini kodi ipande kiasi hicho. Na sio kwamba wanahudumia hizo nyumba hakuna chochote kinachofanyika nyumba zinazidi kuchakaa kadri siku zinavyoenda.