Aicc Watinga Kwenye Ufisadi

socrates

Member
Jun 26, 2008
15
0
Nilivyopata habari hii nilidhani ni udaku lakini baada ya kutemebelea Arusha hivi majuzi kwa lengo la kubook mktano kwenya ukumbi wa Simba Uliokarabatiwa nilishangaa na kuamini ni kweli. Nimepata data kidogo tu za kuanzia .

Katika kukarabati ukumbi wa AICC kwa ajili ya Sulivan , kiongozi wa AICC Bwana Kaaya aliingia mikataba ya kujenga ukumbi huo kitapeli na kusababisha hasara kubwa. Makampuni mengi yalikuwa ya nje na walichofanya ni wizi wa wazi wazi mchana kweupee. Mfano nilpata info kuwa Kampuni moja ya iitwayo Notson Accustica ya Spain na Ufaransa ililipwa paundi 85,000. 00 bila kufanya kazi yoyote .Kazi hiyo alipewa fundi wa Kibongo kwa hela kidogo tu huku wazungu akiishia na kitita hicho cha fedha bureee.

Kwa macho yangu nimeshuhudia ukumbi huo .Japokuwa ukiona kwa macho tu unapendeza lakini mkikaa hamuwezi kupishana na hatari ikitokea kujiokoa ni ndoto. Viti vyote ni vya sinema hall na hkuna meza. Nilihoji kidogo niliambiwa hata hmeshimiwa Jk aliwahi kuhoji ila Kaaya ni best yake . Gharama ilitomika ni zaidi ya billion 4 na asilimia 75% ya gharama hiyo zililipwa kampuni za kitapeli na amabzo kuzipata haukufuatwa utaratibu wa manunuzi PPRA. Nimeambiwa Bwana Kaaya alisafiri mwenyewe na kuingia maktaba na kampuni hizo moja kwa moja huko huko France na Spain. La zaidi sana ni kwamba kampuni hizo zinahisiwa kuwa na uhusiano wa karibu sana.

Ili kuthibisha hili nimejaribu kuuliza washkaji Wizarani ya Mambo ya nje nikaambaiwa fedha hizo zote zinalipwa na serikali . Hapa ndipo pamenipa confu maana sasa naamini ufisadi umetinga huko. Ukiacha kazi za ujenzi ambazo nilishuhudia kampuni za kibongo zikifanya makampuni haya yalilipwa fedha hizi bila utaritibu. Licha ya hiyo nyingine hazikufanya kazi kabisa.

Figuera International 507,465.00

Jordi Mas I Sangeles 73,195.00

Notson Acustica 185,000

Audio Visuel Company 507,244.00
Total Euros 1,272,904

Na Huu si udaku. Mapamabano dhidi ya ufisadi na magumu kuliko chochote. Walioko Arusha fuatilieni ukweli wa mambo mmwage hapa.
 
Kaaya hajaanza leo haya.Ni matendo yake machafu anayofanya kila leo.Anataka mpaka kuinunua AICC Hospital anafanya juu chini yeye na Mkurugenzi wa Estate Kulwa.
 
Kevo,

Nahisi kizungu zungu kabisa.....Hivi tutabaki na kitu gani katika hii nchi kila mahali ni ufisadi kwa kwenda mbele???? Shamba la bibi watu wanahamisha mazao tu...Bibi anakoroma!!! Aibu!!!!!!!!
 
Kuhusu gharama uliyotaja naamini ndivyo ilivyokuwa imekadiriwa. Msemaji mmoja wa AICC alisema na kutoa maelezo yanayofanana na yako alipohojiwa kwenye TV. Na aliyataja kwa majina hayo makampuni ya nje na nchi yaliko.

Huu utata unaojitokeza sasa, kweli unastaajabisha na naanza kuamini madai yako yanaweza kuwa kweli.

Kazi nzuri bwana socrates.

.
 
Mhh jamani sasa tukikaba kila idara hakuna atakaye salimika wote wameoza kabisa hakuna msafi tuna kazi ngumu sana kuwashughulikia hawa watu.Ila njia pekee nikuendeleza mapambano tu.
 
Tanzania inaliwa juu, chini, katikati, pembeni, kushoto, kulia, mbele na nyuma.
Anyway, mwenye uwezo, hasa kwa wale walio A town wanaweza kukusanya data kuhusu ufisadi hii na kuzimwaga hapa ili mambo mengine yanedelee
 
Kuhusu gharama uliyotaja naamini ndivyo ilivyokuwa imekadiriwa. Msemaji mmoja wa AICC alisema na kutoa maelezo yanayofanana na yako alipohojiwa kwenye TV. Na aliyataja kwa majina hayo makampuni ya nje na nchi yaliko.

Huu utata unaojitokeza sasa, kweli unastaajabisha na naanza kuamini madai yako yanaweza kuwa kweli.

Kazi nzuri bwana socrates.

.

Hizo Euros 1,272,904 ni kwa ajili ya viti,carpet, na vifaa vya sauti tu. Gharama kamili ni Tsh 4.5 billion. Huwezi kuamini hadi leo kuna viongozi wanafanya vitu kama vile nchi imeshakuwa Somalia. Inawezekaneje mtu mmoja kujiamulia kutumia fedha ya Umma bila kufuata taratibu?

Taarifa za kuaminika ni kwamba ni kweli serikali ndio imtoa fedha kupitia katibu Mkuu Wizara ya Nje.
 
Yote yana mwisho,na mwisho wake ni mchungu kuliko subiri!!mawazo ya viongozi wa awamu ya nne ni ya kifisadi,ila mwisho wa yote hatimaye ukweli utashinda ni saa ya ukombozi,tuchukueni hatua!!!
 
cha muhimu tuchunguze uteuzi wake ni kwa sababu ni Kijana wa Elenino au ni mtu aliye kula na JMK hapo mwanzo.
 
Tusubiri kuona kama ripoti ya Mkaguzi Mkuu itaonesha jambo lolote.

Tutegeme lini hiyo Report, maana waswahili wanasema ngoja ngoja humiza matumbo, au ngoja ngoja utakuta mtoto si wako kama ni muda mrefu toka sasa , then wanatakiwa wafanye special audit.
na Hivi hawa watu wa wa Arusha/Meru wanamjaribu Raisi ili wakichukuliwa hatua waseme JMK ana uadui nao aU? Maana Kwenye Mwananchi kuna issue ya Severe kukaa hotelini kwa miezi 9 sasa kisa anasubiri nyumba inayo karabitiwa, cost so far ni 9million, ambayo ingetosha kukodisha nyumba sema 1mill a month. Kisa hakuna fedha za ukarabati, lakini za Hoteli Zipo?
 
Hapo ndo huwa naona kihindi hindi siku zote! Nashindwa kuelewa hili neno serikali utadhani haiundwi na watu wenye akili timamu wanao weza fikiri!.

Kulipa mahoteli, kuandaa ma workshop makubwa na makongamano ya garama kubwa hizo pesa zipo lakini si za mambo ya msingi ambayo yangepunguza upotevu wa pesa nyingi kama hizi!
 
AICC ilikuwa inaendeshwa kifisadi tangu enzi za Lowassa. ni Idara nyingine yenye mauza mauza katika nchi yetu..hili halinishangazi hasa ukizingatia kuwa Kaaya ana malengo ya kugomea mbunge 2010 kupitia ccm. Katika kura za maoni 2005 alikosa kwa sababu za kinithamu lakini amepania 2010 kurekebisha..huenda ndio anajikusanyia mtaji wa kampeni hivyo.
 
Well,this is getting nastier!Jamani kwenye huu uchunguzi msimsahahu huyu Bwana anaitwa Tsavo maana aliingia AICC hana kitu sasa hivi ana majumba kadhaa,magari na hata petrol station jamani kazitoa wapi hizi?
 
Huyo ni shemeji yake Kaaya . Alipata CPA kwa kupitia mfumo wa NABE N.K . leo ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala. Kaaya kama kawaida yake ya kuspin aliwadanganya Board yao wakampa ukurugenzi bila kuangalia vigezo muhimu.

Halafu hiyo Bodi inaongozwa na wasomi wa chuo kikuu wengi tu lakini wakishapewa mshiko na Kaaaya hawaoni tena upuuzi mwingine. Profesa Posi hili linakuhusu asilimia 100. Wake up.
 
Huyu Kaaya amekuwa anafanya mabo jinsi anayojisikia. Ameweza hata kupandisha kodi za nyumba za AICC kwa asilimia mia moja na hajataka hata kukutana na wapangaji ili hata kutoa maelezo kwa nini kodi ipande kiasi hicho. Na sio kwamba wanahudumia hizo nyumba hakuna chochote kinachofanyika nyumba zinazidi kuchakaa kadri siku zinavyoenda.
 
kama hakupandisha bei atakula wapi? Jua hela za Sulivan zilkuwa mara moja tu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom