AIBU ya Mwaka: Wanafunzi 400 wanakaa chini

AIBU ya Mwaka: Wanafunzi 400 wanakaa chini

Determinantor

Platinum Member
Joined
Mar 17, 2008
Posts
61,192
Reaction score
99,924
What a shame? Majivuno, kuringa, kujikweza, kujiona wao ndio wao, kumbe kuna Malaika wasio na hatia wanakaa chini! Mnatoza tozo mjenge Barbara na watoto wetu wakae chini? Hivi tuna akili kweli sisi? Yaani ununue ndege kwa pesa cash na huku Wanao wanashinda darsani wakiwa wamekaaa chini?

Tuna tatizo kubwa sana akilini mwetu, tuna IQ ndogo sana sana

====

Sengerema.Wanafunzi zaidi ya 400 wa darasa la nne na tano wanakaa chini na kutumia chumba kimoja cha darasa kwenye Shule ya Msingi Bugumbikiso iliyopo kata ya Chifunfu wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Paul Vicent amesema shule hiyo ina walimu 30 na wanafunzi 3, 118 kuanzia darasa la awali hadi la saba.

Amesema sababu ya kukaa chini ni idadi kubwa ya wanafunzi licha ya Serikali kutoka Sh71 milioni kujenga vyumba vitatu vya madarasa na matundu 10 ya vyoo.

Mbunge wa Sengerema, Hamisi Tabasamu amesikitishwa na hali hiyo licha ya kutoka ushauri kuwa fedha hizo zitumike kujenga shule nyingine ili kuondoa msongamano huo.

Tabasamu amesema ushauri wake ulipuuzwa na viongozi wa Halmashauri hiyo huku akimnyooshea kidogo ofisa elimu msingi Halmashauri ya Sengerema, Donalt Bunonosi kuwa ndiye aliyesababisha hali hiyo kwa kupuuza ushauri.

shulepiccc
ADVERTISEMENT
Naye Bunonosi amesema hakuwa na maelekezo ya fedha kutumika kujenga shule nyingine bali alikuwa na maelekezo ya kujenga vyumba vitatu vya madarasa na matundu 10 ya vyoo.

Mwenyekiti wa kijiji cha Chifunfu, Dominic Tilosahu amesema wataalamu hawana ushirikiano na wananchi na ndio sababu ya shule hiyo kuendelea kuwa na wanafunzi wanaokaa chini.

Kaimu mkurugenzi Halmashauri ya Sengerema, Ally Salim amesema watazifanyia kazi changamoto za shule hiyo na kuzipatia ufumbuzi.

Akili za Magufuli hizi.
FB_IMG_1623187789249.jpg
FB_IMG_1622734978097.jpg
 
Mbele kwa mbele 60 Yrs wimbo huohuo na chorus ya maisha iko palepale
 
Serikali iuze ndege moja tu Ili tujengee vyoo vya shule nchi nzima tuepuke vyoo vya msaada
 
What a shame? Majivuno, kuringa, kujikweza, kujiona wao ndio wao, kumbe kuna Malaika wasio na hatia wanakaa chini! Mnatoza tozo mjenge Barbara na watoto wetu wakae chini? Hivi tuna akili kweli sisi? Yaani ununue ndege kwa pesa cash na huku Wanao wanashinda darsani wakiwa wamekaaa chini?

Tuna tatizo kubwa sana akilini mwetu, tuna IQ ndogo sana sana

Siku tutakayojifunza kuja na suluhu badala ya lawama ndio siku tutakapoweza kujenga siasa yenye mashiko, vyama imara, jamii makini

Sisi ni watanzania na hawa watoto ni wa Tanzania sio wa chadema wala CCM

Binafsi ningewashauri wapinzani wawe wanatumia matukio kama haya kujijenga badala ya kulalama maana laumu bila mabadiliko yatakayogusa maisha ya hiyo jamii ni bure...

Natamani kujua hiyo shule iko mkoa gani na wilaya gani
 
Serikali iuze ndege moja tu Ili tujengee vyoo vya shule nchi nzima tuepuke vyoo vya msaada

Hiyo misaada ndio wanaipigia promo kila leo
Na wataendelea kuomba ili wajinufaishe wao

Na baada ya miaka 20 au zaidi hali itakuwa mbaya bora ya leo wanafunzi wanakaa chini

Kujisaidia porini haliwezi kutatuliwa kama tumeshindwa miaka yote hii tangu enzi na enzi
 
Waziri mwenye dhamana ya tamisemi ameshalitolea maelezo ya kueleweka

Kumbe shule yenyewe haina muda na tunachokiona ni matokeo ya jamii za wafugaji zinazohamahama
 
What a shame? Majivuno, kuringa, kujikweza, kujiona wao ndio wao, kumbe kuna Malaika wasio na hatia wanakaa chini! Mnatoza tozo mjenge Barbara na watoto wetu wakae chini? Hivi tuna akili kweli sisi? Yaani ununue ndege kwa pesa cash na huku Wanao wanashinda darsani wakiwa wamekaaa chini?

Tuna tatizo kubwa sana akilini mwetu, tuna IQ ndogo sana sana

Chama Cha Mazezeta kimeshindwa kutoa huduma Bora za kijamii kwa watu wake, licha ya kuwakamua Kodi hadi tone la mwisho.
Misitu tunayo, inakuwaje tunakosa madawati?
Mazezeta wameshindwa kuongoza nchi, wawaachie watu wenye utimamu wao walibadilishe Taifa hili
 
Siku tutakayojifunza kuja na suluhu badala ya lawama ndio siku tutakapoweza kujenga siasa yenye mashiko, vyama imara, jamii makini

Sisi ni watanzania na hawa watoto ni wa Tanzania sio wa chadema wala CCM

Binafsi ningewashauri wapinzani wawe wanatumia matukio kama haya kujijenga badala ya kulalama maana laumu bila mabadiliko yatakayogusa maisha ya hiyo jamii ni bure...

Natamani kujua hiyo shule iko mkoa gani na wilaya gani
Wakati vyama vya upinzani vikizuiwa kufanya siasa wewe unashangilia alafu sasa hivi unasema vije na suluhu.hiyo suluhu utaipata vip bila kuacha watu wawe huru kuongea?.Kwa akili za kawaida iko wazi kua ccm imeshindwa kufanya mambo ya msingi kwa ufanisi ndo maana wanaangaika nayale yanayowapa ufahari wa muda kidogo uku mambo ya msingi na muhimu yakiwashinda ndo maana hawataki wengine wawakosoe maana ni aibu.Mkisikia hoja ya katiba mpya ndo mnachanganyikiwa kabisa kwasababu mnajua uwezo wenu mdogo na hamna uwezo wakujenga hoja pale wananchi watakapokua na mamlaka yakuhoji na kuwajibisha.
 
Back
Top Bottom