Zitto: Tunapokea bil 640 na tumepoteza tril 1.8 ya capital gain ya makinikia kwa ubabe usio na tija

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Mwezi Machi 2017 niliwaambia Watanzania kuwa tumepoteza TZS 1.8 trilioni za kodi ya capital gains kwa maamuzi ya papara ya Rais kuhusu mchanga. Nilitukanwa Sana.

Leo tumeishia kupata TZS 640 bilioni ( 1/3 ya tulichokosa ). Mnashangilia Sana.

Nikiwaita Mazwazwa mnasema nawatukana.

Niliandika Machi 2017

" Amri ya Rais kuhusu 'Mchanga wa Dhahabu' imepotezea nchi Tshs 1.8trn Capital Gains Tax

Jana nilipokuwa natoa mada kuhusu miaka 50 ya Azimio la Arusha niliongelea pia suala la umakini wa viongozi katika kauli zao. Kwamba Kiongozi lazima ujue unatoa kauli gani wakati gani. Niliwaeleza wanachama na wageni wengjne katika mkutano wa ACT Wazalendo kuwa Amri ya kiholela aliyoitoa Rais John Magufuli kuzuia usafirishaji wa Mchanga wa Dhahabu imepelekea nchi yetu kupoteza USD 880m Kama kodi ya ongezeko la Mtaji kutokana na mauzo ya Acacia Mining.

Hivi sasa nchini kwetu kuna sheria ya kutoza 20% ya thamani ya mauzo iwapo kampuni zinauziana hisa. Tozo inayotozwa inaitwa Capital Gains Tax. Kodi hii mpya ilitungwa mwaka 2012 ili kukabili wawekezaji waliokuwa wanauziana makampuni juu Kwa juu bila Tanzania kupata lolote. Tanzania imeshafaidika na kodi hiyo Kwa mauzo mbali mbali ambayo yamekwisha fanyika kwenye sekta mbalimbali.

Wakati Rais anatoa AMRI kuhusu Mchanga wa madini kusafirishwa kwenye nje ya nchi kulikuwa na mazungumzo yanaendelea kati ya Kampuni ya Acacia mining ( yenye Assets zinazozalisha nchini Tanzania tu kwa sasa - Buzwagi, Bulyanhulu na North Mara) na kampuni nyengine ya nchini Canada kuhusu Acacia kununuliwa Kwa USD 4.4bn. Mara baada ya amri hiyo mazungumzo yalivunjika na hivyo mauzo kutofanyika.
Iwapo Rais angechelewa kutoa kauli yake Kwa wiki moja tu mazungumzo yale yangepelekea mkataba wa mauzo kusainiwa na hivyo Serikali ingepata 20% ya thamani ya Mauzo Kama kodi ya Ongezeko la Mtaji ( capital gains tax ). Hivyo kauli ya Rais imesababisha hasara Kwa nchi yenye thamani ya USD 880m sawa sawa na shilingi 1.8 trilioni".

Watanzania amkeni huu usingizi wa pono.
 
Hatuna rais bali mkurupukaji asiyetaka ushauri
Angeachia mchanga huku mazungumzo yakiendelea ila kama kweli tumepoteza hizo trilioni 1.8 kwa kuzuia makinikia then tukapata bilioni 700 tu ni zaidi ya upuuzi na phd zetu ni feki kabisa

Hii kweli Tanzania ya viwondor
 
K

Kwani hayo makenikia yameshuka thamani hivi sasa??????
 
Hatuna rais bali mkurupukaji asiyetaka ushauri
Angeachia mchanga huku mazungumzo yakiendelea ila kama kweli tumepoteza hizo trilioni 1.8 kwa kuzuia makinikia then tukapata bilioni 700 tu ni zaidi ya upuuzi na phd zetu ni feki kabisa

Hii kweli Tanzania ya viwondor
Kimario
Hata kusoma tu hapo dk 2 umeshindwa unakuja kukomenti,hamna sehemu Zitto kasema tumepoteza tr 1.8 kwa kuzuia makinikia
 
Zitto kitu ambacho hajui ni kwamba Acacia bado inaweza kununuliwa na kampuni nyngne tukapga ndege wanne kwa jiwe moja,tukapa tax gain ya tr 1.8 ,plus bil 700 za sasa ,bado tukawa na 50/50 pamoja na 16%,Magu piga kazi baba tuko nyuma yako
Hii ni dhana,na vipi isipotokea hali uliyoieleza,kwanini tusione tumepoteza sasa kwakuwa tumeshazikosa wazi kabisa.
Bado la makinikia lingeamshwa baada ya mauziano na resolution ingekuwa kama ilivyo leo,kwa hizo 700bn+50/50+16%.
 
pambana na mazingira ya nyumbani maana nyumba inazidi kuteketea!
Katika hii post hicho ulichokiandika kina maana gani ni vizur kukaa kimya kificha ujinga kama kilichoandikwa hukijui unakuwa mtu mwenye busara inshu imekaa kitaalamu wewe umesoma civics na kiswahili mwisho wa siku utaandika hicho ulichokiandika ili kiendane na uwezo wa fikra zako.
 
Shida yangu ni kwenye ku calculate faida ili tupigiane pasu...
Hizi zako ni fikra pevu kabisa,changamoto zitakuwa nyingi.
-kununuliwa watu wetu na kukubali matakwa ya kimahesabu ya babylon's
-Uwezo binafsi wa watu wetu kitaaluma na maujanja ya wakongwe kimahesabu.
-Kusimamia uhalisia wa gharama wanazoweka ambazo zitakuwa ni sehemu ya uendeshaji kama hawatazizidisha ili kupunguza faida.
-NK.
 
Kwahiyo kama angetulia,wakauziana halafu tukapiga hiyo 1.8tn,halafu akakomaa nao tukaipata hiyo 6.4bn leo maana JPM angekuwa katuletea 2.4tn!?

Si ndiyo?
 
Back
Top Bottom