Aibu: Polisi Tabora waipigia magoti benki ya Access iwatengenezee gari la malindo

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,787
Katika hali ya kusikitisha, jeshi la polisi Tabora, kitengo cha kutuliza ghasia wameiomba Benki ya Access kuwatengenezea gari ambalo linatumika kutuliza ghasia.

Swali la kujiuliza, kwani serikali haitoi fungu la matengenezo ya magari ya jeshi la polisi mpaka wakaililie taasisi isiyo ya umma?

Sasa kama mkulu amesema pesa zote za serikali zipitie NMB, si vyema wangeenda kuililia NMB?

Aibu.

tmp_16965-IMG-20170307-WA0020-2008080206.jpg
 
"Ukitaka kula na wewe lazima uliwe... unataka kula tu halafu kuliwa hautaki; HAIWEZEKANI!"

By JK!!

Serikali kula kula hiyo... shauri zenu!!!
 
kawaida vyombo vya ulinzi na usalama inabidi viwe vinajitosheleza kwa kila kitu hivyo basi ni vyema ikitengewa bajeti ya kutosha itasaidia sana maana.. Madhara ya kuomba msaada kwa taasisi au mtu binafsi itakuja kuleta ugumu baadae nawaza kama hiyo taasisi ikianza kufanya vitendo vya kihalifu unadhani polisi watakuwa na kiburi au nguvu ya kuwakamata ilihali wanajua wao ndo wafadhili wao
 
Walipewa wakazitumia vibaya, hawana ubavu wakuonyesha kubuja pesa za wananchi.
 
aibu ya karne hii.

hizi kodi tunazokatwa zinapelekwa kununua magari ya maji washa wakati hakuna pesa ya kufanyia service magari ya patrol.
Mbona mkulu amewaambia majeda kuwa atachota fedha mahali po pote kutengeneza barabara kutoka Ngerengrere kuunganisha na barabara ya Iringa kwa kiwangi cha lami, sasa hawa mapolisi kwa nini wasimuombe achote fedha po pote watengeneze magari yao!!

Uzoefu unaonyesha mkulu hajali bajeti, yeye ni kuchota tu po pote hata fedha za mikopo ya wanafunzi!!
 
Tukiwasaidia kusema ukweli nchi inaelekea siko wanakataa, wakiambiwa hawapewi hela za OC wanatuita wachochezi Mi naomba mungu huyo meneja wa hiyo benki akatae ili na wao waisome namba vizuri
 
Back
Top Bottom