Watanzania wenzangu kitendo hiki cha Mwenyekiti wa chama kikubwa cha upinzani, Mbunge wa jimbo la Hai na Kiongozi wa upinzani kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kusambaa kwa picha zake zikionyesha kubusuana na mwenzi wake mbele ya watoto ni kinyume kabisa na Mira na Tamaduni zetu sisi watanzania.
Sijawahi, toka udogo wangu mpaka sasa kuona haya mambo yakifanyika hadharani mbele ya watoto, hii kitu haipo hapa Tanzania, na hatupaswi kufundisha watoto wetu wala vijana wa Taifa hili tamaduni chafu kama hizi. Twaweza sema inatokeaga kwenye harusi lakini na ibakie huko kwenye harusi na iswe utetezi kwenye hili.
Kiongozi wetu mkubwa kama huyu kufanya haya na kuweka wazi kwenye jamii si sawa kabisa na Mh. Mbunge anafahamu hivyo. Mh. Mbowe anapaswa atuombe radhi na ajivue nyadhifa zake zote kwasasa sababu kitendo alichokifanya hakileti taswira njema kwa kiongozi mkubwa wa umma. Kwenye jamii yetu huu ni uhuni.
View attachment 193361