Je, picha hii ya Mbowe ina tofauti gani na ile ya askari wa usalama barabarani wakiwa wanapigana mabusu?
Hii ndiyo singo mpya ambayo Mwenyekiti wenu asiyemheshimu Nyerere kiasi cha kushindwa kumwita Baba wa Taifa au Mwalimu badala yake akaanza kumwita Mzee Nyerere amewatuma muanze kuiuza kumwokoa na aibu na mashambulizi anayoyapata sasa ya kuonesha uwezo mdogo wa kiuongozi Kama ambavyo Mwalimu alimtabiria?
Au ndiyo singo mpya ambayo Mzee wa Weka Mbali na Tembo amewatuma vijana wake mje nayo ili kupunguza mashambulizi ya tuhuma za kumaliza tembo wetu ambazo zimeanza upya baada ya yeye kwa kushirikiana na mwenzake mmoja hivi walipoamua kumshambulia mwenzao mmoja katika circles za keki yao!
Waambieni wakuu wenu! Kila wanapokuwa wamezidiwa mashambulizi ya hoja za maana huwa wanaingiza mambo kama haya eti kubadili upepo na kuwarubuni wananchi!
Singo zilizoko mjini kwa sasa ni Katiba Mpya, Uchaguzi Serikali za Mitaa na
Naona umekuja mbio mbio kumtetea bosi wako hadi unapata shida kuyanyoosha maandishi yako vizuri. Kijana kuwa mpole, hichi ambacho bosi wako amefanya sio kitu cha mzaha, ni aibu kubwa, ukosefu wa maadili na miiko.
Katika maelezo yako yote hapo juu, hakuna hata sentensi moja uliyogusia uchafu wa bosi wako Mbowe, bali ulichofanya ni ujanja ujanja wa kutaka kuigeuza mada! Kijana, kuwa mpole.
Hivi, kama uliweza kupigia kelele suala la askali wa usalama barabarani kupiga picha ya hovyo kama hiyo ya Mbowe na hadi askali wale husika wakaachishwa kazi. Iweje leo hii utete uozo wa bosi wako na kutaka kutuaminisha kuwa picha hiyo ya Mbowe ni ya kawaida tu na haina tatizo lolote? Badala yake unatutaka tukomalie katiba mpya? Hivi uandaaji wa katiba mpya unafanya mambo yote mengine yasijadiliwe!?
Mbona wale askali wa usalama barabara uliwajadili vizuri tu na huku mchakato wa katiba mpya ukiwa unaendelea!?
Muleta mada Hammy D Ana wivu wa mke mwenza ...........
Siku zote wewe Makene huwa unatetea uozo. Usitutoe kwenye maada ya msingi. Kila kitu kinachofanywa na viongozi wako wewe unashabikia hata kama ni uozo. Jaribu kutumia akili angalau hata hiyo ndogo uliyonayo kudadavua mambo. Au ndo kusema kwamba unalinda kibarua kisiishe. Kuwa mtu mwenye busara. Hapa tunaongelea picha huyu kiongozi wa Chadema. Sasa kiongozi wa nchi ametoka wapi tena kwenye hiyo picha? Unatumika vibaya na siku wakikuchoka hao unaowatetea utakuja chuta. Waulize wenzako waliojifanya wanawatetea mpaka walishiriki kutunga Ilani ya uchaguzi ya chama chako, lakini walivyochokwa waliitwa wasaliti na wewe ukaja na ushabiki huo huo. Mnakiuwa chama kwa kushabikia vitu vya ajabu. Sasa mmebaki kwenye koti la UKAWA (Uchakachuaji wa Katiba ya Wananchi). Wakati washikaji walivyokuja na mkakati wa mabadiliko ndani ya chama mkawaita wahaini na wasaliti. Damu yao sasa inawatafuna.
huenda yeye Mbowe hajavaa sare za chadema. but inasikitisha sana. He is a state diplomat
WanaJF,
Kwa nafasi aliyonayo Mbowe kama mwenyekiti wa CHADEMA pia mbunge wa jimbo la Hai, kuna namna ambavyo anapaswa kuyaendesha maisha yake na SIO kuishi kihuni na kisela kama ambavyo amefanya katika picha zinazo endelea kusambaa mitandaoni!
Mbowe ambae pia ni mmoja wa viongozi wa UKAWA leo katika siku ya kukumbuka miaka 15 ya kufariki kwa baba wa taifa, ame-post kwenye ukurasa wake wa Facebook picha ambayo imejaa aibu na isiyo na maadili katika jamii yetu.
Picha ambayo Mbowe ame-post ni yenye kumuonyesha mheshimiwa huyo akimpiga "busu" mwanamke ambae hakufahamika kwa haraka wakiwa katika mgahawa.
Je, hayo ndiyo mambo ambayo kiongozi anayejitapa kuwa ana uadilifu anaweza kufanya? Ukizingatia tupo kwenye siku muhimu ya kumbukumbu ya kifo cha muasisi wa taifa letu!
Je, picha hii ya Mbowe ina tofauti gani na ile ya askari wa usalama barabarani wakiwa wanapigana mabusu?