puza46b
Member
- Nov 3, 2010
- 91
- 261
Leo nimetumiwa video ya binti mtanzania aliyeiba akiwa anapigwa mawe. Niliishia pale wamemuwekea kuni. Sikuweza endelea angalia.
Nilipofika kazini kuna swali moja likawa linakuja kichwani. Why we Africans, especially Tanzanians don't hold each other to the highest standards? Ingetokea Ulaya that would have been an outrage.
Lakini pia juzi tumewakasirikia South Africa kwa kuchoma Waafrica wenzao.
Sisi ni wanafiki. Na vyombo vya habari Tanzania ni vinafiki, vinaogopa kuwaambia Watanzania ukweli kwamba tuna psycho kwenye jamii yetu. Vinaogopa kuiambia serikali mihimili ya sheria nchini vimefeli kwenye wajibu wao. Vinaogopa kuwaambia wananchi wa Tanzania, haswa wale wanaoshangilia hawana tofauti na walioua Rwanda au waliokaa kimya ndani ya nazi Germany. They are all guilty.
Ningeomba vyombo vya habari vilishikie njugu hili balaa ya hukumu za mitaani kama ambavyo vilitangaza taarifa za ESCROW. Wachomaji na wauwaji wa vibaka au wezi wadogo waone aibu na kujificha kama ambavyo wauwaji wa albino wanajificha sasa.
Nakumbuka dunia ilipoanza kuonyesha mauaji ya albino tulisema hizo ni imani za vijijini. Ikachukua nguvu ya under the same sun project na kina Vic Mtetema kulazimisha serikali ikubali kuna tatizo nchini.
Leo tena tumekamatwa na mifupa. Sisi ni fisi na tunaringa kuwa ni kondoo. Tusijione kutopigana baada ya uchaguzi kunamaanisha kuna amani nchini. Amani ya kweli ni ile inayomfikia hadi mnyonge.
Shame on us.. again..
Tata.