Aibu kubwa kwa polisi - hadi sasa wachoma makanisa Zenj na waliomteka Ulimboka hawajakamatwa!


Vyombo vya usalama vikiamua vinaweza tatizo ni vile vinafanya kazi kwa mashinikizo/maagizo kutoka juu kwa manufaa ya walio juu(viongozi Wa juu Serikalini)
 

Haaahaaa! Polisi nikatafute nini MAMA POROJO? Unafikiri matatizo yanayoikumba Afrika yanaanzishwa na nani? Anyway kitu ambacho najivunia bila shaka wala wasiwasi ni kuwa mimi sio mkabila wala mdini. My life talks for itself...MAMA POROJO, siasa hizi za maji taka zinatupotezea muda. Imefika wakati sasa tuanze kulete hoja na hamasa za kujenga uchumi. kama nguvu tunazotumia kupigana vikumbo kwenye siasa tungezitumia kwenye kujenga nchi, unafikiri tungekuwa wapi?
 
Last edited by a moderator:
Mhalifu sugu angekuwa uraiani!?

Ndio maana anakuwa mhalifu sugu. Angekuwa jela huo uhalifu angeufanya saa ngapi? umesahau, kuna mmoja kakataa hata dhamana ili akawatembelee wenzake jela?
 
Jeshi la polisi la kina Chagonja na Kova unategemea nini? Ni jeshi la ma-nyinyiemu!
 

kwa technology ya sasa hata mazungumzo ya sauti yanapatikana, lakini sasa kama serikali imehusika nani anathubutu kutoa huo ukweli? Nchi ilishaoza hii. Hakuna system inayofanyakazi sawa sawa, tunaishi kwa rehemua za mwenyezi mungu tena kwakuwa watz ni waoga.
 
Ukidhani unaimani na jeshi la polisi basi ujue una matatizo makubwa tu! ndiyo maana Kova watu wana mwambia hatuna imani na wewe yeye ana lazimisha 'ohhh mimi lazima tu nita fanya uchunguzi" kama hatuna imani na wewe tutawezaje kuwa na imani na matokeo ya uchunguzi wako? Jshi la polisi lijiweke wazi kwamba wao wako kwa maslai ya serikali basi, unafifki hausaidii.
 

unajua ng'ombe haoni umuhimu wa mkia wake mpaka akiukata nzi wakianza kumsumbua ndo ataukumbuka nina maana kwamba wapo wasiouona umuhimu wa jesh la polisi mpka matatizo yawakute ndo watawakumbuka na kujua umuhimu wake.
 

Bado taarifa za "KIINTELIGISIA HAZIJAWAFIKIA RASMI" zikisha wafikia watatoa tamko endelea kusubiri
 
vyombo vya usalama vikiamua vinaweza tatizo ni vile vinafanya kazi kwa mashinikizo/maagizo kutoka juu kwa manufaa ya walio juu(viongozi wa juu serikalini)

una maana gani unaposema shinikizo toka juu kwa manufaa ya walio juu
 
Walioweka vinasa sauti chumbani kwa Dr Slaa pale dodoma ni miaka mi4 sasa hawajakamatwa, waliowajeruhi Hainess Kiwia na Machemli karibu mwaka unapita, achilia mbali matukio kibao ya wizi na ujambazi.

Jeshi la polisi la Tz ni kitengo cha propaganda cha chama cha Mapinduzi a.k.a mabwepande na chama kinawalipa kwa kuwaacha wapokee rushwa wapendavyo, wapeane ajira kindugu na kushirikiana na majambazi bila kuchukuliwa hatua yoyote. Wako active kuzuia maandamano wanayodhani yanatishia uhai wa CCM.
Utendaji kazi wa polisi wetu ni sawa na ahadi za Kikwete, vyote havitekelezeki.
 
unajua ng'ombe haoni umuhimu wa mkia wake mpaka akiukata nzi wakianza kumsumbua ndo ataukumbuka nina maana kwamba wapo wasiouona umuhimu wa jesh la polisi mpka matatizo yawakute ndo watawakumbuka na kujua umuhimu wake.
Ukipata matatizo halafu uwe hauna hela ya kuwahonga polisi utajuta kuzaliwa. Mimi nawachukia polisi na nikipata matatizo nitatoa hela kununua huduma kwa vile huduma pale haitolewi bure, kuingia ndio bure kutoka hadi utoe hela
 


Pole sana kwa mawazo mgando: kwa upande wa zanzibar, tafuta ripoti ya kanisa katoliki iliyotolewa na baraza la maaskofu katoliki tanzania. humu jamvini ipo, (makanisa 23 yameshachomwa tangu mwaka 2003) na hakuna aliyekamatwa wala kushtakiwa mpaka sasa. Ishu ya Ulimboka labda uwe kipofu na kiziwi kuweza kuelewa. Polisi imeoza nani asiyejua. kama hauamini endesha gari lako ovyo alafu wakukamate...uone walivyooza...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…