AI video generator applications za gharama nafuu

AI video generator applications za gharama nafuu

prida

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2026
Posts
1,285
Reaction score
2,573
Kwa kawaida mimi ni mtu nisiyeweza kukaa tu bila kutumia muda wangu kufanya jambo lenye manufaa kwangu.Katika maisha yangu nishaandika Novel,jifunza tailoring,mapishi ya mataifa mbalimbali,kifaransa,kiarabu,kuigiza,kuimba,,ufundi plumbing.Mimi ni fimale plumber mzuri sana ni hivyo tu maisha hayajatoa nafasi kupiga hii mishe.Kuna siku nilimshangaza fundi fulani alitaka kunifanyia upuuzi.

Anyway,kwa sasa nina maternity leave ya mwaka mzima na tayari maisha ya kukaa tu yashaanza kunichosha na ninataka kutengeneza Documentary fulani ambayo nina ndoto ya kuiuza somewhere.

Nataka kuitengeneza kwa AI.
Ni makala ndefu yenye episodes 11 na kila episode itakua na dakika 20.

Sasa kwa apps ninazozijua mimi hii kitu inaweza kula credits za kama milioni 6 hivi.

Uchumi wangu ni mdogo kutumia 6M ambayo sina uhakika kama itarudi ndo mana nimekuja kwenu kuomba kujuzwa kama kuna apps za low cost.

Hivi wale wanaotengeneza AI movie nao wanatumia hizi hiz costy credits?Maana sidhani kama zile movie zao zinawapa kipato cha kufidia gharama kubwa za credits?

Asanteni.

By mama wawili.
 
Ya gharama nafuu ambayo hata mm natumia ni gemini ya 50k per month hii ina 1000 credit, hi nayo ipo safi tuu.

Zile za kutengenezea movie kama higgsfield yenyewe inakula $1.5 kwa video ya sekunde moja h n kama usipotegemea mambo ya credit, but ikitegemea mambo ya credit bc utatoa 70k kwa credit 600

All in all, gemini naona ipo simple kuitumia.
 
Hongera Sana mkuu
Nilikutana na fundi rangi wa kike, mzuri Sana kwenye kazi yake.

Bahati mbaya au nzuri ni kwamba aliolewa na fundi mwenzetu na Juzi kati nilikuwa kwao amezaa watoto wawili na Sasa amekuwa mama wa familia nyumbani.
Amepigwa stop mambo yote ya saiti, kitu ambacho hata mimi bila shaka naweza kufanya kama nikioa mwanamke anayeingiliana na mambo ya saiti in direct

Wanawake mnapitia mengi Sana huko Saiti.

Samahani nimetoka Nje ya mada
 
Hongera mama wawili..
Kwanza unaonekana kuwa mtu perfect sana na mpambanaji, hongera tena.
Unaweza kunipa mchanganuo kidogo wa hiyo 6M? kisha baada ya hapo nitarecommend kitu.
Btn inaonekana unafanya mambo mengi for fun, kwani hutaki kufanya hii documentary for fun lkn kikaacha footprints hata kama kitakupa 0 or - profit?
 
Ya gharama nafuu ambayo hata mm natumia ni gemini ya 50k per month hii ina 1000 credit, hi nayo ipo safi tuu.

Zile za kutengenezea movie kama higgsfield yenyewe inakula $1.5 kwa video ya sekunde moja h n kama usipotegemea mambo ya credit, but ikitegemea mambo ya credit bc utatoa 70k kwa credit 600

All in all, gemini naona ipo simple kuitumia.
Unamjua Claude? Sijawahi kutengeneza videos.. natengeneza picha tu zenye captions.. claude ananibaruzia kinoma
 
You berra watch ur back.. si kila fursa ni fursa. Kuna fursana
Tatizo lako umenifikiria vibaya

Ishu n kwamba hy 6m n nyingi japokuwa video za AI zinaumiza kichwa mno mana unaweza kuandika prompt video ikatoka ndivyo sivyo na credit zishaenda hvy na itachukua muda mrefu kuzimaliza.

Ila mm hy kazi naweza kufanya vyema tuu hata kwa bei chini ya hapo.
 
Chatgpt simkubali.. kazi yake ni 3/10

Nitawajaribu..
Chatgpt humkubali?

Moja kati ya AI zangu bora ni hiyo, labla uwe unatumia ya bure ndo hutoweza kuifurahia Ila chatgpt ya kulipia imenyooka kinoma haina vipengele.

Mfano unataka prompt za video, then umelipia hy chatgpt inakupa kitu kimenyooka

Hata picha nazo zimenyooka ukiwa na ya kulipia.
 
Documentary nzima kutumia AI generated video lazima iwe ni gharama kubwa. Maana gharama sio video pekee hata sauti, picha, script bado editing. Ila inategemea documentary ya nini.

Nawaza labda kwenye kupunguza gharama utumie hiyo unayotaka. Hapo unapata kama sekunde 10 na kuendelea then kwingine unatumia picha, maana sio movie ni documentary visuals si lazima zipishane litoke tukio hili lije hili. Unatumia ipi nazijua Runway, King na Veo. Theoretically maana mwenyewe mwaka huu niliwaza kwenye kupoteza muda niwe nafanya hizi maana kukaa nje ni mvivu sana.

Ila sina practical experience.
 
Ya gharama nafuu ambayo hata mm natumia ni gemini ya 50k per month hii ina 1000 credit, hi nayo ipo safi tuu.

Zile za kutengenezea movie kama higgsfield yenyewe inakula $1.5 kwa video ya sekunde moja h n kama usipotegemea mambo ya credit, but ikitegemea mambo ya credit bc utatoa 70k kwa credit 600

All in all, gemini naona ipo simple kuitumia.
🙏🙏
 
Chatgpt humkubali?

Moja kati ya AI zangu bora ni hiyo, labla uwe unatumia ya bure ndo hutoweza kuifurahia Ila chatgpt ya kulipia imenyooka kinoma haina vipengele.

Mfano unataka prompt za video, then umelipia hy chatgpt inakupa kitu kimenyooka

Hata picha nazo zimenyooka ukiwa na ya kulipia.
Tumetumia ya kulipia na akawa anafanya ufala tu

Cc Selikavu
 
Hongera Sana mkuu
Nilikutana na fundi rangi wa kike, mzuri Sana kwenye kazi yake.

Bahati mbaya au nzuri ni kwamba aliolewa na fundi mwenzetu na Juzi kati nilikuwa kwao amezaa watoto wawili na Sasa amekuwa mama wa familia nyumbani.
Amepigwa stop mambo yote ya saiti, kitu ambacho hata mimi bila shaka naweza kufanya kama nikioa mwanamke anayeingiliana na mambo ya saiti in direct

Wanawake mnapitia mengi Sana huko Saiti.

Samahani nimetoka Nje ya mada
Hujatoka.
Hongera zake fundi mrembo.
Mimi sijawahi kupahatika kufanya kazi kwenye ma site.Nina ujuzi tu.Ila life likinipiga sitaenda kujiuza naingia site kama plumber watoto wanaendelea kusoma
 
Ushauri..

AI generated videos hazina human touch na ni rahisi kupuuziwa..

Hiyo 6m ni kubwa mno, kama ungeweza Unge fanya real production,, trust me ukienda kusaka director ambaye yuko hungry ukawa unampa laki kwa siku.. Then ukagharamia location hauta tumia hela nyingi na itauza sana.

Sijui kwanini but I find AI generated stuff hectic..

Sijajua maudhui ya hiyo documentary ila kama ni ya kibiashara tumia AI kwa uchache sana. Itakusaidia kwenye sales.

Anyways, hongera kwa kujifungua, Mwambie uncle Nakuja kumwona soon(jokes).

Best wishes
 
Back
Top Bottom