Ahsante mume wangu kwa kuachana na mchepuko

Ahsante mume wangu kwa kuachana na mchepuko

Habari zenu wadau,

Wiki kama tatu zilizopita tulikuwa na mgogoro na mume wangu kuhusu kuwa na nyumba ndogo. Katika uchunguzi wangu nikagundua ni single mother alikuwa anajitahidi sana kumbembeleza mume wangu ili ampatie mahitaji mbalimbali kama kodi na ada ya mtoto wake.

So baada ya mimi kugundua na kugombana na mume wangu (hapa niseme kujadiliana sijamtukana) kugombana kwa hekima, mume wangu alinibembeleza sana sio kwa kukiri moja kwa moja (wanaume hawaombi msamaha direct) akanishukuru kwa kumlinda na kanihakikishia mimi ndio chaguo la moyo wake kama ambavyo ameapa mbele ya Mungu.

Sasa basi huwa nafatilia status yake WhatsApp nikakuta anasikitikia mapenzi yamekufa. Akaja kuweka nyingine anasikitikia kuwa "mume wa mtu atakuchezea, atakugeuza na atafanya anavyotaka kisha atarudi kwa mkewe".Nilichogundua ni kuwa mume wangu kaachana na mchepuko wake.

Jamani michepuko mkiachwa msilalamike sana kwa kuwa nyinyi ni viburudisho tu, na ukimpata mume wa mtu usijione kuwa wewe ni zaidi sana ya mkewe.

NDOA NA IHESHIMIWE
Matatu hapo; kapigika na kasi ya Magu hii dili hamna, kaokoka au umemroga. Michepuko haiepukiki.
 
Mkapime ukimwi kwanza
 
Nashukuru ile allergy yako ya sherehe inakuisha taratibu
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Naweza jiandaa kabisa then nikaishia kuvua nikalala. Yaani hata sielewi[emoji134] [emoji134] [emoji134]
 
Angekuwa anaamini alichokiandika basi asingefungua huu uzi. Yuko in denial, Kafungua ili angalau apate mawazo ya kujustify anachojaribu kujiaminisha. Ukweli ni kwamba hili jambo bado linamtafuna ndio maana yuko busy kuchungulia status za mumewe na za mchepuko.

Angalia hata kauli zake juu ya huyo mchepuko, simtetei mchepuko ila namshangaa anavyojaribu kuonyesha mumewe ni mwema sana na mchepuko ndio una makosa.
Yes hata mie nimefatilia inajionesha kuna tatizo, ukweli anaujua sema tuu hataki kuukubali,

Hata hivyo hakuna aliyemsafi kati ya hao wote huyo mumewe na mchepuko.
Yes najua inauma kuingiliwa ndoa yako ila apambane na mumewe sio kutafuta unafuu juu ya maumivu ya moyo wake kwa kumsema vibaya huyo mchepuko.

Lakini pia mapenzi ni upofu, waweza ugeuza ujinga kuwa ujanja na ujanja ukaona ni ujinga vilevile.
 
Sawa nataka shari kacheze kwaito mpaka ung'oe kisigino.

Hope unaendelea vizuri mpz
Haha me mzima kabisa mpenzi, za wewe?

Aisee sinaga utani kwenye kwaito, sikumbukagi hata kama kuna kula kwenye sherehe. Yani nakuwa na kisebengo jamani mweeh[emoji151] [emoji151] [emoji126] [emoji126]
 
Haha me mzima kabisa mpenzi, za wewe?

Aisee sinaga utani kwenye kwaito, sikumbukagi hata kama kuna kula kwenye sherehe. Yani nakuwa na kisebengo jamani mweeh[emoji151] [emoji151] [emoji126] [emoji126]
Ahahahaaaaaa
Unavua viatu unaweka pembeni alafu unakuwa usawa wa camera [emoji327] ili usijekosa kutokea kwa dvd [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Hahahaaa wanaume wapi hao !
Hapo anakupaka mafuta kwa mgongo wa chupa
Siku akikumbuka kiuno kama cha wacheza shoo wa Twanga pepeta
Anamtxt tu baby am back...huyu fala nimeshamtuliza njoo tujilie mema ya nchi...
Nyumba ndogo hawanaga hiyana
Exactly na Side chick hawanaga makuuu
 
Back
Top Bottom