Ahsante mume wangu kwa kuachana na mchepuko

Ahsante mume wangu kwa kuachana na mchepuko

We muache tu ajikute kumuona mumewe malaika as if huyo anayemuita mchepuko alijitongoza.We shukuru tu umepewa heshima ya kuwa mke lakini kuanza kumdhihaki huyo dada na kumuona mumeo mwema si vizuri au labda hajawahi ona kuna familia mwisho wa siku ule ulioita mchepuko ndo unakuwa mke halali na uliyekuwa ukiitwa mke ndo unabaki huna mbele na hichi na uthibitisho nacho kwa asilimia tisini cause imetokea kwenye familia yetu.
ni kweli mbaya sana kumdharau huyo dada
 
hahha kweli nyie mko dunia ya mabali !alichoongea Kitumburee ni kweli zaid ya 100% kuna mdada mmoja yupo hapa mjini !nguo zooooote za watoto wa mume wake ananunua yeye had mashuka ! narudia tena nguo zote za watoto wa mume wake had mashuka anapewa hela ananunua mume anazipitia jion dukan kwake anazipeleka hom ! shopping ndogo ndogo zote shost anafanya ! acha kbs !had simu anayotumia mkewe mchepuko ulienda dar kununua !upo?
Cases hizo zipo nyingi tu.
 
Mie utundu wa nini ?
Kila mtu apambane na hali yake.
Nivunjike kiuno na uzee huu kisa kubuni style mpya za kumtuliza mume ndani ?

Hapana aisee kama anajielewa ataridhika na anachopata na atatulia mwenyewe.
Au kisukari kitanisaidia kumtuliza.
Kabisa mydear
 
Habari zenu wadau,

Wiki kama tatu zilizopita tulikuwa na mgogoro na mume wangu kuhusu kuwa na nyumba ndogo. Katika uchunguzi wangu nikagundua ni single mother alikuwa anajitahidi sana kumbembeleza mume wangu ili ampatie mahitaji mbalimbali kama kodi na ada ya mtoto wake.

So baada ya mimi kugundua na kugombana na mume wangu (hapa niseme kujadiliana sijamtukana) kugombana kwa hekima, mume wangu alinibembeleza sana sio kwa kukiri moja kwa moja (wanaume hawaombi msamaha direct) akanishukuru kwa kumlinda na kanihakikishia mimi ndio chaguo la moyo wake kama ambavyo ameapa mbele ya Mungu.

Sasa basi huwa nafatilia status yake WhatsApp nikakuta anasikitikia mapenzi yamekufa. Akaja kuweka nyingine anasikitikia kuwa "mume wa mtu atakuchezea, atakugeuza na atafanya anavyotaka kisha atarudi kwa mkewe".Nilichogundua ni kuwa mume wangu kaachana na mchepuko wake.

Jamani michepuko mkiachwa msilalamike sana kwa kuwa nyinyi ni viburudisho tu, na ukimpata mume wa mtu usijione kuwa wewe ni zaidi sana ya mkewe.

NDOA NA IHESHIMIWE
Mume anaweka mafumbo status kama mwanamke.Pole dada yangu kwa kulamba gulasa.
 
Si angeolewa na aliyemzalisha? Kimemshinda nini? Ndo maana amekuwa single mother kwa kuwa siku zote anatumika km kiburudisho na sio mke...
And wewe unayetumika kama mke still mumeo anatoka nje ya ndoa lol!! Kuna vitu huwa tunazungumza kujipa moyo tu ila ndani tunaungua. Huo ndio ukweli mchungu.
 
Kuachana sidhani kikubwa ni mume wako mvumilie tu wanaume wote wapo sawa baba mmoja na mama mmoja
Mtuvumilie tu, kwakuwa sisi wote ndivyo tulivyo. Sirahisi kuacha nje na kufanya hivyo si kuwa hatuwapendi sasa sijui kwanini lakini karibuni wanaume wote tuko hivyo. So long as wewe umepata bahati ya kuolewa just tulia, omba tu mumue awe makini asisahau familia. Mbaya zaidi anaweza akamuacha huyo kutokana na pressure na akajenga mahusiano na mwingine. Usijaribu kuamini kuwa mumeo hafanyi, la ni bado hujamkamata lakini wote tipo hivyo na hakuna mwingine aliyebora zaidi ya aliyokuoa hivyo usidhani ukimwacha huyu utapata aliyesafi, hakuna kitu kama hicho mimi ni mwanaume nakuelza kwakuwa tunajijua.
 
Mmh! Si bure ntaendelea kucheza kwaito kwenye harusi za mashosti mpaka 70. Kiwango changu cha upumbavu na kiburi bado kiko juu sana. Sasa kwa nini umemwambia mume wako asante baada ya kujiridhisha ameacha mchepuko? Alikuwa na haki ya kuchepuka useme amekufanyia fadhila kuuacha mchepuko au hii asante ni ya nini?
Alafu anajiona ana akili kuliko huo mchepuko, funny!!!
 
Mmh! Si bure ntaendelea kucheza kwaito kwenye harusi za mashosti mpaka 70. Kiwango changu cha upumbavu na kiburi bado kiko juu sana. Sasa kwa nini umemwambia mume wako asante baada ya kujiridhisha ameacha mchepuko? Alikuwa na haki ya kuchepuka useme amekufanyia fadhila kuuacha mchepuko au hii asante ni ya nini?
Heaven Sent nimekumisimo jamani.
 
Si kila mwanamke anaweza kuolewa na mwanaume aliyemzalisha. Wengine wanazalishwa na baba na wajomba zao, wengine na watoto wenzao, wengine na wabakaji, wengine na wanaume kama mume wako, wengine waliolewa ila ndoa zao hazikufanikiwa, wengine walifiwa na waliowazalisha, wengine walikataliwa,,,,,,,,,

Bila kujali sababu ya mwanamke kulea peke yake, haihalalishi mwanamke kuingilia ndoa ya watu, wala haihalalishi mume wa mtu kwenda kumtongoza. Mnyonge mnyonge ila umpe haki yake. Huyo dada na mume wako wote ni WAZINZI. Ukiuliza kimemshinda nini kuolewa na aliyemzalisha uulize pia kimemshinda nini mumeo kudumbukiza kidude chake kwenye kishimo chako tu? Hao waasherati wawili wawili wote ni wadhaifu. Usiwe kama wale mafarisayo waliompeleka kwa Yesu mwanamke waliyemfumania wakitaka apigwe mawe. Kuwa fair. Kama mume wako karudi basi tumia muda wako kumshukuru Mungu na kuomba asianguke. Kumnanga huyo "single mom" mwenzangu kutakupa furaha ya muda tu na kukupotezea muda wa kuchungulia status. Siku ukikuta kaandika kinyume na matarajio yako moyo ukupwite bure kumbe anaongelea mume mwingine.
Thanks for comming.
 
Ndo wale michepuko waache kujiona kuwa wao ni suluhisho la matatizo ya kwenye ndoa ya mme/ mke wa mtu. Kama ilivo hakuna sababu moja ya kujikuta umekuwa single mother ndo hivohivo Hakuna sababu moja ya mwanaume kuchepuka. Usihalalishe ufuska
Mbona wewe unahalalisha ufuska wa mumeo? Au huyo mchepuko ulimbaka mumeo?
 
Ahahahaaaaaa

Sasa hiyo asanteh kubwa kaitoa kwa kejeli au?
Mbona na wewe unanivuruga?
Teh teh teh teh
Angekuwa anaamini alichokiandika basi asingefungua huu uzi. Yuko in denial, Kafungua ili angalau apate mawazo ya kujustify anachojaribu kujiaminisha. Ukweli ni kwamba hili jambo bado linamtafuna ndio maana yuko busy kuchungulia status za mumewe na za mchepuko.

Angalia hata kauli zake juu ya huyo mchepuko, simtetei mchepuko ila namshangaa anavyojaribu kuonyesha mumewe ni mwema sana na mchepuko ndio una makosa.
 
Back
Top Bottom