Nimemsikia Ahmed Rajab leo asubuhi akihojiwa na Waziri Hamsini wa BBC. Akijibu swali juu ya mwaliko wa Kikwete toka kwa Obama kuhudhuria mkutano wa G8, mchambuzi Ahmed Rajab kasema kaalikwa kwa vile nchi yetu TZ inaongoza kwa kuuza ardhi kwa wageni(wawekezaji wa kimataifa). Nakiri Ahmed Rajab ni mchambuzi na mwandishi mzuri na mimi ni msomaji mzuri wa makala zake katika gazeti la kila wiki la Raia Mwema. Nimemsikia mara kadhaa akichambua juu ya hali ya mambo katika mashariki ya kati, lazima nikiri nimeelimika sana juu ya hali ya mambo ilivyo mashariki ya kati kupitia chambuzi zake katika BBC.
Pamoja na hayo yote nilianza kutilia shaka dhamiri yake katika kuhabarisha umma pale alipoandika katika Raia Mwema historia ya mapinduzi ya Zanzibar ya 1964. Katika mfululizo wa makala zake kuhusu mapinduzi hayo Ahmed Rajab alijitahidi sana lakini bila mafanikio kuponda umuhimu(significance) wa ushiriki wa Field Marshal John Okello katka mapinduzi hayo matukufu. Ahmed Rajab alijaribu kuonyesha kuwa John Okello alidandia tu kilele cha mapinduzi lakini si mtu aliyeshiriki kikamilifu katika kuyaandaa na kuyatekeleza kama dunia nzima inavyojAhmed Rajabua. Katika kilele cha uongo wake aliandika kuwa siku chache baada ya mapinduzi, Mzee Aboud Jumbe siku moja alimuona John Okello katika kambi ya Welezo ,akiwa na bastola kiunoni kama ilivyokuwa kawaida yake, na kuuliza huyu ni nani. Mwandishi mahiri na mkongwe nchini Joseph Mihangwa alishindwa kuvumilia ghiliba hizi za mwandishi mwenzake Ahmed Rajab na kumjibu kikamilifu kwa kutoa maelezo ya kina juu ya nafasi ya John Okello katika mapinduzi ya Zanzibar.
Tukija katika uchambuzi wake wa leo kuhusu JK kualikwa na Obama napata shaka sana kuamini maneno ya Ahmed Rajab. Mchambuzi Ahmed Rajab atufanyie hisani wasomaji wake kwa kutoa takwimu za ekari za ardhi ambazo zimeuzwa kwa wageni kipindi cha JK. hili ni muhimu ili kulinda imani ya baadhi ya wapenzi wa makala na chambuzi zake.