Ahmed Rajab sikubaliani na wewe katika hili! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ahmed Rajab sikubaliani na wewe katika hili!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by thatha, May 18, 2012.

 1. t

  thatha JF-Expert Member

  #1
  May 18, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Nimemsikia Ahmed Rajab leo asubuhi akihojiwa na Waziri Hamsini wa BBC. Akijibu swali juu ya mwaliko wa Kikwete toka kwa Obama kuhudhuria mkutano wa G8, mchambuzi Ahmed Rajab kasema kaalikwa kwa vile nchi yetu TZ inaongoza kwa kuuza ardhi kwa wageni(wawekezaji wa kimataifa). Nakiri Ahmed Rajab ni mchambuzi na mwandishi mzuri na mimi ni msomaji mzuri wa makala zake katika gazeti la kila wiki la Raia Mwema. Nimemsikia mara kadhaa akichambua juu ya hali ya mambo katika mashariki ya kati, lazima nikiri nimeelimika sana juu ya hali ya mambo ilivyo mashariki ya kati kupitia chambuzi zake katika BBC.

  Pamoja na hayo yote nilianza kutilia shaka dhamiri yake katika kuhabarisha umma pale alipoandika katika Raia Mwema historia ya mapinduzi ya Zanzibar ya 1964. Katika mfululizo wa makala zake kuhusu mapinduzi hayo Ahmed Rajab alijitahidi sana lakini bila mafanikio kuponda umuhimu(significance) wa ushiriki wa Field Marshal John Okello katka mapinduzi hayo matukufu. Ahmed Rajab alijaribu kuonyesha kuwa John Okello alidandia tu kilele cha mapinduzi lakini si mtu aliyeshiriki kikamilifu katika kuyaandaa na kuyatekeleza kama dunia nzima inavyojAhmed Rajabua. Katika kilele cha uongo wake aliandika kuwa siku chache baada ya mapinduzi, Mzee Aboud Jumbe siku moja alimuona John Okello katika kambi ya Welezo ,akiwa na bastola kiunoni kama ilivyokuwa kawaida yake, na kuuliza huyu ni nani. Mwandishi mahiri na mkongwe nchini Joseph Mihangwa alishindwa kuvumilia ghiliba hizi za mwandishi mwenzake Ahmed Rajab na kumjibu kikamilifu kwa kutoa maelezo ya kina juu ya nafasi ya John Okello katika mapinduzi ya Zanzibar.

  Tukija katika uchambuzi wake wa leo kuhusu JK kualikwa na Obama napata shaka sana kuamini maneno ya Ahmed Rajab. Mchambuzi Ahmed Rajab atufanyie hisani wasomaji wake kwa kutoa takwimu za ekari za ardhi ambazo zimeuzwa kwa wageni kipindi cha JK. hili ni muhimu ili kulinda imani ya baadhi ya wapenzi wa makala na chambuzi zake.
   
 2. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Unajua umekwisha muhukumu kwenye kichwa chako kwamba ni mtu asiyeelezea mambo kwa ukweli.Wasi wasi wangu hata akikupa maelezo unayoyataka hadithi itakuwa ni ile ile ya kumpinga
   
 3. t

  thatha JF-Expert Member

  #3
  May 18, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Mkuu nakubaliana na wewe 100%, nadhani huyu mpemba mwenzio kaamua kutupotosha wadanganyika.
   
 4. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #4
  May 18, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Sasa mtoa mada hukubaliani nae wapi???kwenye suala la muungano au kwenye suala la mapinduzi?????
   
 5. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #5
  May 18, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,336
  Likes Received: 1,801
  Trophy Points: 280
  Mimi nina shaka shaka sana na nia za ujumbe kwenye maadishi yake mengi. Kusema kweli sio mpenzi kabisa wa articles zake kwa sababu mara nyingi anakuwa kama afanya biashara ya kuwamba ngoz...anajaribu sana kuvutia kwake!
   
 6. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #6
  May 18, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Amesahau Zanzibar walipoiuza Mombasa kwa Wakenya? Wamevunja rikodi kwa kuuza mji mzima na vitongoji vyake.
   
 7. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #7
  May 18, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Ahmed rajab ni mchambuzi ninaemuheshimu sana na huwa haumi umi maneno kama wewe.....

  nikuulize....niwekee sababu za JK kwenda G8.....very concreate reasons...usiniambie ati kaalikwa na Obama....weka sababu za msingi
   
 8. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #8
  May 18, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  Hata mimi sikubaliani na madai ya Rajabu lakini vilevile sikualiani na Aya ya Pili ya Mtoa mada manake naona kama haina uhusiano! Sana sana ninachokiona ni dhamira ya mtoa mada kuanza kujenga taswira kwama Ahmed Rajabu si mtu wa kumwamini linapokuja suala la uchamuzi wa baadhi ya mambo! Hapa, amewakosea wasomaji kwavile baadhi watakuwa tayari wameshaathiriwa na aya hiyo ya pili ya mtoa mada ambayo tayari imeshatoa negative perception abt Rajabu!
   
 9. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #9
  May 18, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  madai ya leo asbuhi au ya MAPINDUZI????
   
 10. J

  JokaKuu Platinum Member

  #10
  May 18, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,805
  Likes Received: 5,114
  Trophy Points: 280
  ..hebu tuweke kando views za Ahmed Rajabu kuhusu muungano.

  ..ukweli ni kwamba Tanzania na Ethiopia ziko ktk harakati kubwa sana za kuuza mapande ya ardhi kwa wawekezaji wa nje ili walime mazao kwa ajili ya ku-export. kuna mwanachama mwenzetu wa JF alilete article inayozungumzia suala hilo.

  ..Ahmed Rajabu hajakosea ktk madai yake.
   
 11. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #11
  May 18, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Huyu Jamaa anachuki Binafsi na huyo Rajabu, njia sahihi ya kuonyesha upotoshaji wa Rajabu ni kwa mtoa mada kufanya hili kifuatacho.
  1. Kuweka hapa sababu rasmi za mualiko wa Jakaya
  2. Kuweka ushahidi kwamba sio kweli kwamba Tanzania inauza Ardhi Mapande kwa Mapande kwa wageni hasa wamarekani.

  Ama sivyo naona Rajabu anataka kushambuliwa bila sababu za msingi.
   
 12. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #12
  May 18, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Ni kweli Tanganyika inauza ardhi yake suala hili halina ubishi kabisa.
   
 13. A

  ATA Member

  #13
  May 18, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 84
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 15
  sio kwamba wanauziwa ni kwamba wanapewa ardhi bure, mfano kule Rukwa wamarekani kupitia kampuni ya Agrisol wamepewa maelfu ya hekari kwa gharama ya tshs.200 (two hudred shillings) kwa hekari
   
Loading...