Ahadi zenu wanasiasa mzitimize

DAD'S SON

JF-Expert Member
Nov 18, 2015
392
500
Wasalaam,
Ukweli utabaki pale pale wanasiasa ndio watu ambao wanadhima kubwa sana katika maisha yetu.Ukizungumzia siasa unazungumzia uongozi.

Leo la huu uzi ni kuwakumbusha wale wanasiasa walio tuahidi mambo mazuri huku muda ukiwa unakaribiakuisha ila napenda kuwaambia kuwa muda bado watimize hata machache waliyotuahidi(it's not over until it's over).

Kikawaida binadamu ana memory 3
1.sensory memory,hii huifadhi vitu kwa sec kadhaa then vitu unasahau so hata ukijaribu kuretrieve information haiwez kuja.

2.short term memory hapa mtu anaifadhi vitu kwa muda wa masaa kulinganisha na sensory memory,mfano kwa wale ambao wanasomaga notice siku ya paper alafu anaingia kwa paper na bado anakumbuka alichosoma soma saa kadhaa zilizopita basi fahamu short term memory yake ifanya kazi ya kuifadhi ilo faili kwa masaa kadhaa.

3.Long term memory hii bana huwa inahifadhi big files hata za miaka miaka na miaka ndo maana leo hii mtu anakumbuka kitu alichofnya miaka10 iliopita wengine wanakumbuka mpk utoto waoWakuu hii memory huwa hapotezi kumbukumbu kizembe km izo memory zingine hapo juu.

Nimeweka izo aina za memory hapo juu kuwaambia wanasiasa kuwa memory number 3 huwa inahifadhi big files na kusahaulika ni kazi pia memory hiyo huwa hainaga kusahau mateso,furaha,ahadi hasa kubwa kubwa Mfano unakuta watu waliahidiwa maji cha kwanza ukosefu wa maji ni mateso memory haiwezi sahau cha pili ni ahadi ya kuondoa hayo mateso(ukosefu wa maji) so ni ngumu kusahaulika.Kwa muktadha huo naomba niwaambie kuwa tunakumbuka na ndio maana nawakumbusha.

Dini pia zinazungumzia masuala ya ahadi pia,na kwa wale ambao walitoa Ahadi warejee kwenye holy books waone ulazima wa kutimiza walichoahidi.Dini zinahimiza kutimiza ahadi pindi tu ukifanikiwa kuwepo ulipopakusudia,wanasiasa tuliwapa kura zetu so kusudi lenu limetimia basi na sisi tutimizieni mliotuahidi kabla hamjafika hapo mlipo.Dini zinasema kwa asietimiza Ahadi zake chance ya kwenda kwenye "burning fire" ni kubwa.

Yangu ni ayo tu kama umekwazika basi unisamehe ila nilikuwa katika harakati za kukumbushana tu maana sifa ya binadamu huwa anajisahau sana hasa wale tuliowapa dhamana.
...it's worse to regret
 

fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
6,421
2,000
Dawa ni kuwa na mifumo (system) madhubuti na wala sio kutegemea kudra za wanasiasa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom