Ahadi ya ajira milioni moja changa la macho?

Hizo ajira za JK zitakuja linio Jamani? Mbona nina elimu , sikuwa na ajira na bado sina ajira? Zitakuja lini hizo ajira ? Hizo naona zilikuwa ni usanii tu wa kujitafutia urais. Likini JK ujue umetuangusha sisi wengine masikini , tusiokuwa na ajira japo tuna ka-elimu kidogo.
 
wakuu
Naona wakuregenzi wengi humu wanashida moja kama iliyonikumba mimi wakati ule nayo ni-

Siku napanda pipa si nikachengi burungutu la Fedha TSHS nakapewa EURO kiduchu hata kigajani mwa mtoto zinalegalega ,mie nikahisi wameniingiza mjini nini?? maana nikipiga mahesabu ni zipo sawa lakini nikiangalia uwiano wa namba nilizitoa na kupokea haziwiani.

Kubwa kuliko baada ya kutua na pipa nikaingia supermarket da si nikakuta kuku anaenda EURO 3 mie nikaona duu yani kuku bei raisi namna hii wakati kwetu ni TSH 1500-2000 si nikazivamia ,na kilichokua kinanidaganya kumbe ni TARAKAMU na hisi humu watu wengi wanadanganywa na TARAKIMU

Hapa nataka kusema hivi mtu unaweza lipwa mshahara wa TSH 150/= ukaishi kama mfalme ama ukalipwa TSH 5000000/= bado ukaishi maisha ya dhiki mnooooooooooo.

Pia kulinganisha mishahara ya wafanyakazi ktk nchi tofauti kwa kutumia TARAKIMU ni batili na haufai maana mazingira na huduma ktk nchi husika ni tofauti kabisa mfano-

Juma anaishi UK analipwa Dola US$6000 kwa mwezi lakini kodi ya nyumba kwa mwezi ni US$ 3000 umeme na maji US$ 1500 nauli ya mama ya juma na wanae kwenda shule US$ 500 School fee ya mwanae USD 600 na matibabu tusema US$ 300 inayobaki ni kwa ajili ya chakula na matumizi madogo madogo ambayo ni US$ 100

ASHA anaishi CHINA analipwa US $ 200 kwa mwezi lakini kodi ya nyumba kwa mwezi ni US$ 5 umeme na maji US$ 10 nauli ya mama ya juma na wanae kwenda shule US$ 5 School fee ya mwanae FREE FEE na matibabu FREE inayobaki ni kwa ajili ya chakula na matumizi madogo madogo ambayo ni US$ 180.
Sasa ni yupi mwenye maisha bora?????????????
 
Vipi Mkuu wangu heri ya mwaka mpya

kumbe ni wewe M+4nz4/4? nilifikiri tumeingiliwa na watu wa fujo.

.......kama inavyodaiwa.......eti tumpe nafasi ya mwaka huu na mwaka ujao.......halafu eti ndio tuta-judge

Wadanganyika tuna safari ndefu sana mkuu Ogah. Usione nakumbushia hivi vitu ukadhani ni utani. Inasikitisha wakuu kama Kulikoni wanashangilia hizi ajira 'invisible' za JK. Angalia outcome ya kupandishwa ghafla na bila mpangilio kwa kima cha chini cha mshahara. Walalahoi kibao wametimuliwa vibaruani. Hakuna anayejali. Subiri msikie wizi utakavyoshamiri Tanzania.

Najiandaa, naweka mmasai kwangu... wakimuua nazaa nao!
 
A million jobs coming as promised - Kapuya

2008-07-19 09:27:41
By Guardian Reporter, Dodoma

The government said yesterday it has gone almost half way in fulfilling President Jakaya Kikwete`s promise to create a million jobs and should be through with the task by 2010 as planned.

According to Labour, Employment and Youth Development minister Juma Kapuya, 43.7 per cent of the target has been achieved.

He made the remarks when unveiling the budget estimates for his ministry for financial year 2008/09 in the National Assembly here yesterday.

?Information obtained in June 2008 says a total of 437,205 new jobs had been created in various sectors from January 2006 to December 2007, which is equivalent to 43.7 per cent of the one million jobs goal expected to be attained by 2010,? he said.

Prof Kapuya clarified that the assessment excluded jobs created in agriculture a sector that employs some 70 per cent of the country?s populace, adding that the private sector created the biggest number of job opportunities.

An index attached to the ministry?s budget speech and made available to House members and the media yesterday shows that 58,399 jobs were created in the public sector, 183,789 in the private sector and 195,017 in the informal sector.

However, House Community Development Committee chairperson Jenista Mhagama said the government was moving too slowly in implementing the initiative on creating the one million jobs.

She challenged the ministry to elaborate on the challenges it saw lying ahead of it, noting: ``Given the fact that the private sector has vast potential to create even more jobs in the future, our committee strongly advises the government to exploit this avenue more fully.``

She called on the rest of the government to join hands with the ministry in pushing the course further for the good of the nation.

Presenting views of the opposition on the estimates, Labour,
Employment and Youth Development shadow minister Salim Abdallah Khalfan underlined the importance of improving labour relations at workplaces.

``True democracy in countries the world over starts with workers having vibrant trade unions that operate freely and that can demand their members` basic rights,`` he said.

Prof Kapuya asked the House to endorse for his ministry 6.5bn/- for recurrent expenditure and 6.2bn/- for the implementation of development activities during the year.

My take:

1. Kwenye hizo statistics za Kapuya inaonyesha 45% ya ajira hizo imetokana na informal sector and this is a group which no one in Tanzania has reliable data. kAPUYA AMETOA WAPI HII NAMBA???????

2. Kapuya haelezi hiyo job creation ni based on current requirements au ni thru govt efforts kama JK alivyoahidi 2005.

3. Kwamba kilimo hakikuhusishwa kabisa katika hizi Statistics, in some sense anataka kutuambia ahadi ya ajira milioni imetimilizwa..............du! Hivi sisi ni mabwege kiasi hiki kuamini upuuzi huu????

4. NSSF na PPF mifuko mikubwa kabisa ya social security mpaka leo haijafikisha wanachama milioni. Hizo ajira mpya wahusika hawalipi nini?

5. Nafikiri Prof. Kapuya anafahamu kabisa anachosema ni uongo na ni hoja ya kufikirik pia sidhani kama hata yeye anaziamini takwimu zake.

TUTAZUGWA MPAKA LINI?????????????
 
Tukubali ama tukatae ishu ya kutengeneza 1million jobs is a cliche.Haiwezi kutimilika na hata hizo ajira wanazosemea ni danganya toto.
 
tukubali Au Tukatae Hakuna Kitu Kinaitwa Ajira Kwa Vijana.walitudanganya Tu Tuwape Kula Na Sasa Wanakula.
 
I reserve further comments until I receive a full break down of these employment figures on aspects like the mean wage in the various new employment destinations, the wage range, the likelihood of the newly employed to remain in their jobs, etc.
 
Hizi ni ajira za kuwapa vijana ukatibu wa CCM tawi ,wilaya, na mikoa hivyo ukizihesabu na ukawaangalia makatibu waenezi n.k. zinaweza kufikia kiwango hicho.
 
Hizi ni ajira za kuwapa vijana ukatibu wa CCM tawi ,wilaya, na mikoa hivyo ukizihesabu na ukawaangalia makatibu waenezi n.k. zinaweza kufikia kiwango hicho.

Mkuu mpaka kieleweke umenifurahisha sana na hii comment...... Well usikute hata zile NGO za mifukoni nazo zimeingizwa kwenye takwimu hizi
 
Tatizo ni kwamba hii ahadi ya ajira milioni moja ilitolewa kwa sababu za kisiasa, na hizo cooked statistics za Muheshimiwa hapo juu ni ushahidi wa wazi kuwa bado serekali yetu haijatambua kuwa hili ni suala la kiuchumi and they will need more than political blah blah to deliver this promise.
 
Hivi kwa nini Muungwana anaammua kuendeleza usanii wake?

Kwa nini anakubali kuzungukwa na watendaji ambao ni wasanii wakubwa kama yeye? Kwa nini asijisafishe? Kwa mtazamo wangu njia pekee ya Kujisafisha ni kuachia madaraka, jambo ambalo halitaja tokea.

Ni aibu kubwa Mheshimiwa Mbunge kutoa Takwimu zenye kudanganya umma kwa kiasi hiki. Ni kwa faida ya nani? Wapenda maendeleo ya kweli naona nao wapo likizo!
 
YAANI HII INAONYESHA KWAMBA KUNA JAMAA WAKO BIZE MNO SASA HIVI KUPIKA DATA KWA AJILI YA KAMPENI ZA 2010. tusubiri tu mtaambiwa hata maisha bora yameshawasili, ari, kasi na nguvu mpya imewezesha mafisadi kuumbuliwa, barabara km 10,000 zimejengwa na stori nyingi tu...... yetu masikio
 
Wajinga ndio waliowao. Ila sasa miye nimechoka sitaki kuendelea kuliwa. Ninataka data kamili wazimwage hapa nihangaike nazo, siyo haya majibu ya jumla jumla waliyozowea kutumia ili kututafuna. Kumbe Kapuya naye kishakuwa hivi? Alipokuwa anafundisha Botany alikuwa mtu makini sana. Kumbe mtu akishakuwa mwanasiasa ndani ya CCM anakuwa mbabaishaji? Duh!
 
Serikali kumwaga ajira milioni tano

2008-07-22 10:55:44
Na Mashaka Mgeta, Dodoma

Serikali inakusudia kutengeneza ajira mpya milioni tano, zikiwa ni zaidi ya zilizoahidiwa na Rais Jakaya Kikwete, wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005.

Akiwa kwenye kampeni hizo, alipogombea kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Kikwete, aliahidi kuwa serikali yake itatoa kipaumbele katika maeneo mbalimbali, ikiwemo kutengeneza ajira mpya milioni moja.

Hata hivyo, akijibu hoja za Wabunge waliochangia hotuba ya bajeti ya wizara yake, Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Profesa Juma Kapuya, alisema serikali inakusudia kufikia ajira milioni tano, kutokana na mkakati uliaondaliwa kuhusu ukuzaji wa ajira nchini.

Alisema mkakati huo uliandaliwa kwa ushirikiano wa serikali, Shirika la Kazi Ulimwenguni (ILO) na Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).

Alisema mkakati huo unatoa fursa zaidi kwa watu wa kada na makundi mbalimbali, wakiwemo wenye ulemavu.

Aidha, Profesa Kapuya, alisema hivi sasa serikali inawasiliana na wadau kama taasisi zisizokuwa za kiserikali na mashirika mbalimbali, ili kupata takwimu halisi ya ajira mpya zinazotengenezwa nchini.

Alisema hadi kufikia sasa, takwimu zinaonyesha kuwepo ajira mpya 437,035, ambazo zinatarajiwa kuongezeka kupitia jitihada mbalimbali zinazofanywa na kutoa mfano wa Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini (MKUKUTA).

Profesa Kapuya, alisema fasihi ya elimu ya Ukimwi mahali pa kazi, ipo katika hatua ya uchapishwaji na itakapokamilika, itasambaza kwa ajili ya matumizi yake.

Aidha, alisema serikali inatambua kuwa viwango vinavyolipwa kutokana na madhara yanayotokea sehemu ya kazi, havilingani na athari zinazowakabili walengwa.

Alisema kutokana na hali hiyo, serikali inapitia sheria hiyo kwa ajili ya kuandaa mswada wa mabadiliko yake, utakaowasilishwa bungeni katika mkutano ujao mjini hapa.

Pia, Profesa Kapuya, alisema wizara yake inaendelea na mpango wa kukagua vibali vilivyoombwa na wageni kwa ajili ya kufanya kazi nchini, ili kubaini ikiwa vinakiuka taratibu zilizopo.

Alisema kwa mujibu wa taratibu hizo, kazi zinazopaswa kufanywa na wageni, hazitakiwi kuwa katika kiwango kinachoweza kufanywa na wazawa.

Wakati huo huo, Profesa Kapuya, alisema imebainika haja ya kuongeza wigo wa ushiriki wa vijana, kushiriki katika uundwaji wa baraza la vijana la Taifa.

Profesa Kapuya, alisema mchakato huo ulianza, ulisababisha kufanyika kwa mikutano miwili, ambapo iligundulika kuwepo haja ya kuwashirikisha vijana wengi zaidi, hasa kutoka maeneo ya vijijini.

Alisema mchakato wa sheria unaokidhi mkakati wa kuundwa kwa baraza hilo, utawasilishwa kwenye kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, mara utakapokamilika.

SOURCE: Nipashe

Tuma Maoni Yako
 
This is kidding!!!!! Kwi kwi kwi !!!!!!
 
Jamani hili la wageni kufanya kazi ambazo mtanzania wa kawaida anaweza kufanya nafikiri serikali ama imeshindwa kulidhibiti ama ufisadi uliotawala kila kona unatumika kuhalalisha hata watu wanaofanya kazi za ulinzi kuwa ni expatriates.Inasikitisha sana kuona kwenye makampuni mengi ya kigeni badala ya kuwajengea uwezo watanzania ili waweze kufanya kazi zinazoshikiliwa na wageni wanafanya kila jitihada kuhakikisha kwamba wazawa hawapati nafasi ya kufahamu mambo mengi na hivyo kuonekana hawafai kushika position za juu katika makampuni hayo.Kuna mifano lukuki kuthibitisha hayo lakini naona hakuna ambaye yuko tayari kusikiliza kilio cha wananchi wa nchi hii.Inasikitisha sana.
 
Huu upuuzi zile ajira 1mil. zimewashinda sasa mnakurupuka na ajira 5mil. nyie endeleeni kutuona kama wendawazimu siku zenu zinahesabika tu maji yatawafika shingoni tu ngoja tupashe misuli tujiandae kuchukua jasho letu...maana jasho la mtu haliliwi hivi hivi watakiona cha moto.
Kapuya wewe hufai toka ulipo kuwa kwenye ELIMU tulisha kumulika na wewe ni fisadi tu na tunajua unamiliki MGODI sasa hao watu unataka kuwaajili kwenye mgodi wako?????
 
Back
Top Bottom