Eric Ongara
Senior Member
- Sep 19, 2006
- 165
- 8
Wakati wa Kampeni Jakaya,ili kuteka vijana,ambao ndio wapiga kura wengi alitoa ahadi chongo juu ya ajira.Akaahidi ajira milioni moja!
Kwanza ahadi yenyewe haieleweki! Ukifuatilia kwa mujibu wa takimu,kila mwaka kwa wastani vijana kati ya 650,000 mpaka 750,000 wamaingia katika soko la ajira.Sasa tukichanganua ahadi ya Jakaya,kila mwaka ndani ya miaka mitano atatengeneza ajira kwa wastani wa 250,000 kila mwaka.Maana yake ni kwamba,kila mwaka vijana laki tano watakuwa hawana ajira!
Halafu anasema ajira anazo tengeneza zitatokana na mpango wa manedeleo ya shule za sekondari na ule wa shule ya msingi pamoja na sekta ya afya,huu mtazamo si sawa kwani sasa serekali ni mtengeneza mazingira na si muajiri mkuu,mikakati ilipaswa kuegemea zaidi kwenye sekta binafsi!
Bajeti ya mwaka huu,wameshindwa kusema watatengeneza ajira kwa kiasi gani na kwa njia zipi! Bora angeahidi kutaja asilimia la ongezeko la ajira na sio kutaja takwimu ambazo hazina mantiki yoyote! Anachemka!
Nasema,sioni muelekeo wala uelewa wa Jakaya na Baraza lake la mawaziri katika kutekeleza azma hii!