ZeMarcopolo
Platinum Member
- May 11, 2008
- 14,017
- 7,220
Mungu wangu eee...bado unaendelea kujichanganya. Wasomi mchango wao huo ni wa mawazo. Siku hizi wanaita consultancy. Michango ya aina hii huwezi kuonesha rundo la kazi kama fundi seremala anavyoweza kuonesha rundo la maranda ujue kafanya kazi. Mtei hana rundo la Maranda kuonesha kafanya lipi. Lakini pamoja na kazi yake kuwa ya kitaalam, bado naweza kukuonesha kitu kafanya.
Hii kauli uliyoibandika hapa ni ya uongo: Kwamba "usomi wake alihakikisha unamfaa yeye tu." Design ya mfumo wa kodi mpya kafanya mtei na kamati yake wakati wa Mwinyi. Matunda yake tunayaona. Kwenye bodi ya Kahawa ameweka mawazo mazuri mengi kuboresha zao hili, likiwapo la matumizi ya miche ya kisasa, ambapo mawazo na mitizamo mingine anafundisha watu kwa matendo badala ya maneno au maandiko. Mtei analo shamba la kahawa la mfano watu wakajifunze kwake kwa matendo.
Wewe ZeMarcopolo hujui kitu kuhusu Mtei.
Chadema kilipoanza 1992/93 Mtei alikusanya Watanzania wenzake kutoka karibu kona zote za Tanzania kuanzisha chama pale Kisutu. Ni mtu aliyekubalika na Watanzania wenzake wa wakati huo, akaweka mchango wa mawazo uliokubalika kikazaliwa chama makini. Nimetaja mchango wake katika Tume ya kubadili mfumo wetu wa kodi kuleta huu tunaoutumia sasa, nimetaja mchango wake katika bodi ya Kahawa hadi siku za hivi karibuni (sijui kama bado yupo humo wiki hii) na uasisi wake wa chama makini; lengo langu ni kufuta fikra zako potofu kuwa elimu yake imemsaidi yeye binafsi. Elimu yake imelisaidia taifa letu. Wasomi hufanya kazi ya kushauri. Kazi ya kushauri ameifanya vizuri katika maisha yake kwa faida ya Watanzania wote.
Kajipange vizuri urudi kubishana na mimi.
Yaani mamenno unayoandika unakubali moja kwa moja kuwa Mtei mchango wake kwenye kupigania uhuru ni SIFURI.
Unaongelea mambo ya Serikali ya Mwinyi wakati swala hapa ni mchango wa Mtei kwenye harakati za kupigania Uhuru.
Hizo kazi unazosema ni AJIRA. Mtei aliajiriwa na alilipwa pesa stahiki.
Kusema kuwa mchango wa wasomi ni consultancy hivi Mwalimu Nyerere hakuwa msomi? Je angezubaa kwenye mambo ya kitaifa kama Mtei nchi ingekuwa wapi?
Historia sio siri. Kama kuna jambo Mtei alilifanya kwa kujitolea ili kuifanya Tanganyika iwe huru litaje hapa.
Hivi wewe ukiwa dereva wa Hiace halafu ukaipeleka Hiace garage unaweza kujivunia kuwa umempa mwenye Hiace msaada? Hizo kazi unazotaja zilikuwa ajira na Mtei tulimlipa, hakujitolea. Ni AIBU kwa kijana wa enzi za kupigania Uhuru tena kijana msomi kuwa na historia TUPU kama ya Mtei.
Shughuli za TANU zilifanywa na watu ambao hawajui hata kusoma vizuri, lakini vijana wasomi kama Mtei walikuwepo ila walijiweka pembeni na harakati za TANU. Uhuru ulipopatikana tu wakajitokeza kuchukua "shavu". Usomi wa namna hii ni ubinafsi ambao Mtei mwenyewe sasa hivi hawezi kujivunia.
Chama kilichoanzishwa na mtu wa namna ya Mtei hakiwezi kuwa na lengo la kuwanufaisha watanzania wote kwa usawa. Ili chadema iwe na malengo mema kwa watanzania ni LAZIMA itoke mikononi mwa mbinafsi Mtei.