Ahadi kumi (10) za mwana TANU na Tanzania yetu ya sasa

AHADI KUMI ZA MWANATANU

1. Binadamu wote ni ndugu zangu na Dunia ni moja.
2.Nitaitumikia nchi yangu na binadamu wenzangu wote kwa unyenyekevu na moyo wa upendo na huruma.

3.Nitajitolea nafsi yangu kuondoa umaskini,ujinga,maradhi na dhuluma hapa nchini na duniani pote,
4.RUSHWA ni adui wa HAKI, SITATOA wala KUPOKEA RUSHWA,

5.cheo ni dhamana,sitatumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu,

6.Nitajielimisha kwa kadri ya uwezo wangu na kuitumia elimu yangu kwa faida ya wote.

7. Nitashirikiana na wenzangu wote kuijenga nchi yetu na dunia yenye haki na amani,

8.Nitasema kweli daima,fitina kwangu mwisho,

9.Nitakuwa raia mwema wa Tanzania,Afrika na Dunia nzima,

10.Nitakuwa mtii kwa rais na serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania,

11.Usiwe na hisa katika kampuni
12. Usiwe na nyumba ya kupangisha au mishahara miwili.

Huu ndio mjadala nawaletea tujadili zitto,anaweza?,
 
Hizi ni kanuni, imani au ahadi? Ahadiziko 10 tu
 
hata aliyetangaza kiama kwa wenye vyeti fake ilipofika kwa bashite uzalendo ulimshinda akavunja ahadi ya 8 ya mwana Tanu.
 
Chama cha TANU ni chama kilichosaidia sana katika harakati za kuikomboa nchi yetu katika makucha ya ukoloni chini ya Uongozi madhubuti wa Hayati Julius K. Nyerere.

Malengo makubwa ya chama hiki ilikuwa ni ukombozi wa nchi yetu lengo ambalo kwa kiasi kikubwa lilitimia.Kinachonofurahisha sana ni jinsi viongozi wa TANU walivyokuwa na dhamira za kweli na kujitolea kwa hali na mali katika kuikomboa nchi yetu.

Lengo kubwa la post hii, ni kuwakumbusha wana JF Ahadi za Mwana TANU, na kama bado ni relevant kwa wakati huu ambapo Tanganyika(Tanzania) imefikisha miaka 49 ya uhuru, zifuatazo ni ahadi za Mwana TANU enzi hizo:

Je, ahadi hizi za Mwana TANU zimeendelezwa na CCM au ndio zimepigwa dafrao?

Sisi kama Taifa hatuwezi kuziendeleza na kuzitekeleza ahadi hizi na kuzifanya kuwa ni za kitaifa kuliko kuwa za chama?

Lengo la post hii ni kuchochea mjadala ili kuona namna gani nchi yetu inaweza kujikwamua kutoka katika umasikini huu tulionayo kama taifa.

Naomba kuwasilisha wadau
Kwa sasa haziheshimiwi kabisa

Nape ametekeleza ahadi namba nane huku akivunja ahadi namba 10
 
zingekuwa zinazingatiwa kusingekuwa na ubaguzi wala wimbi la viongozi au wanadamu wala rushwa na mafisadi
 
Watanzania tufike mahala tutambue matatizo yanayotukabili.Kimsingi tukubaliane kuwa CCM kama chama cha siasa kimeshindwa katika kukabiliana na maadui wetu watatu ambao ni ujinga,maradhi na magonjwa,na rushwa (nyongeza).Serikali imebaki kuwa gulio la watu wenye hamu ya kuishi peponi ilihali wako peponi.Cheo ni dhamana tena bali ni zawadi,vyeo vinagawiwa kwa marafiki,vimada na wote wanaochangia mkuu kupata madaraka.

Kimsingi hatuhitaji kuwa na utitiri wa vyama vya siasa ambavyo mipango madhubuti ya kushika dola na kufanya mambo ambayo chama tawala kimeshindwa.Ni vyema tukaunga mkono harakati zinazofanywa na vyama vya upinzani.Kwa sasa,na wala sio siri kwamba CHADEMA ndicho kinaonekana chama mbadala(Kwa mtazamo wangu).
Ulienda vizuri mkuu lkn ulivyotaja cdm ndiyo umeharibu kila kitu kwani hawa watu ni sumu kali kwa taifa letu

1. Lowasa
2. Sumaye
3. Nyalandu
4. Masha

Wasingewapokea hao watu cdm ingekuwa vizuri sana.
 
Ahadi 10 za maccm

1. Binadamu wote si ndugu zangu. Nitawateka, kuwatesa, kuwabambikia kesi, kuwavunjia nyumba zao na hata kuwaua

2. Hainihusu kitu kumtumikia yeyote yule siku zote nitaweka mbele maslahi ya tumbo langu na matumbo ya wale walio karibu nami. Maslahi ya Tanzania na Watanzania hayanihusu.
3. Sitajitolea nafsi yangu kuondoa ujinga na umaskini. Nitafanya wizi, ufisadi na kuwadhulumu wakulima, wafanyakazi na wafanyabiashara nchini pia kudumaza elimu nchini ili kuongeza wajinga.

4. Rushwa si adui wa haki, bali ni njia rahisi ya kujitajirisha na pia kupata kile nitakacho. Nitatoa na kupokea rushwa kama kawa.

5. Cheo si dhamana na nitakitumia kupata utajiri wa haraka haraka kwa njia halali na haramu pia.

6. Sitajielimisha na hata nikiamua kujielimisha ni kwa faida si kwa faida ya yoyote yule.

7. Kushirikiana ni kupoteza muda, na sina huo muda wa kupoteza. Kila mtu abebe msalaba wake.

8. Nitasema uongo daima na kufanya fitina kwa yeyote anayetishia madaraka yangu na hata naweza kumpa kifungo cha muda mrefu au hata kumuua.

9. Uaminifu na uraia mwema hauhusu kitu. Wizi, ubadhirifu, ufisadi na uongo kama kazi.

10. Rais mwenyewe si mtiifu na wala si mwaminifu kwanini niwe mwaminifu kwake?
 
Ona ahadi namba tano, halafu angalia mambo anayofanya Jiwe, mpwa wake na genge lake la mapolitical interpreneur ndio utajua ccm ilikuwa ya zamani sio hii.
 
Chama cha TANU ni chama kilichosaidia sana katika harakati za kuikomboa nchi yetu katika makucha ya ukoloni chini ya Uongozi madhubuti wa Hayati Julius K. Nyerere.

Malengo makubwa ya chama hiki ilikuwa ni ukombozi wa nchi yetu lengo ambalo kwa kiasi kikubwa lilitimia.Kinachonofurahisha sana ni jinsi viongozi wa TANU walivyokuwa na dhamira za kweli na kujitolea kwa hali na mali katika kuikomboa nchi yetu.

Lengo kubwa la post hii, ni kuwakumbusha wana JF Ahadi za Mwana TANU, na kama bado ni relevant kwa wakati huu ambapo Tanganyika(Tanzania) imefikisha miaka 49 ya uhuru, zifuatazo ni ahadi za Mwana TANU enzi hizo:

View attachment 652246

1. Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja.​
2. Nitaitumikia nchi yangu na watu wake wote​
3. Nitajitolea nafsi yangu kuondoa umaskini, ujinga, magonjwa na dhuluma.​
4. Rushwa ni adui wa haki. Sitapokea wala kutoa rushwa.​
5. Cheo ni dhamana. Sitakitumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu.​
6. Nitajielimisha kwa kadiri ya uwezo wangu na kutumia elimu yangu kwa faida ya wote.​
7. Nitashirikiana na wenzangu wote kuijenga nchi yetu.​
8. Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko.​
9. Nitakuwa mwanachama mwaminifu wa TANU na raia mwema wa Tanganyika na Afrika.​
10. Nitakuwa mtiifu na mwaminifu kwa Rais wa Serikali ya Tanganyika.​

Je, ahadi hizi za Mwana TANU zimeendelezwa na CCM au ndio zimepigwa dafrao?

Sisi kama Taifa hatuwezi kuziendeleza na kuzitekeleza ahadi hizi na kuzifanya kuwa ni za kitaifa kuliko kuwa za chama?

Lengo la post hii ni kuchochea mjadala ili kuona namna gani nchi yetu inaweza kujikwamua kutoka katika umasikini huu tulionayo kama taifa.

Naomba kuwasilisha wadau
Kwa kuzikumbuka hizi yaonyesha kuwa waweza kuwa ni mzalendo wa kweli tofauti na waganga njaa waliopo sasa hivi, huko kwenu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom