ZeMarcopolo
Platinum Member
- May 11, 2008
- 14,017
- 7,220
Mkuu genekai hebu mwache ZeMarcopolo niongee naye. Kwa bahati nzuri nina bundle zangu za kutosha leo na muda wa kubishana naye ZeMarcopolo ninao.
Context ya Kipindi cha Mtei ipo kama ifuatavyo. Wasomi walikuwa wachache kweli. Nyerere na Mtei wakiwapo katika kundi hili la wasomi wachache. Nyerere alikuwa mmoja katika Watanganyika wenye vipaji vya uongozi wakati huo. Lakini hakuwa peke yake mwenye kipaji.
Maelezo yako yenye mapungufu ni pamoja na haya: Kwamba Mtei aliona utawala wa mkoloni unavumilika. Haya ndiyo unayoyasema wewe ZeMarcopolo. Na kwamba kila pale taifa lilipomuhitaji alilitelekeza. Hali ya uchumi ilivyoyumba kutokana na vita ya Uganda akalitelekeza taifa tena.
Maelezo yako wewe ZeMarcopolo yanatuambia wasomaji wako kwamba hujui historia, hujui dhana ya ushindi katika vita hutegemea falsafa zipi.
Hakuna Mtanganyika aliyekubali kuwa ukoloni ulikuwa unavumilika. Wewe ZeMarcopolo huna ushahidi popote kuonesha kuwa Mtanganyika mmoja kwa jina la Edwin Mtei alitaka ukoloni uendelee. Kama unao ushahidi huo uweke hapa. Tukio la Mtei kufanya kazi katika Shirikia la Kimataifa haliwezi kuwa kigezo cha kuvumilia ukoloni kwa kuwa Shirika alilofanya kazi nalo malengo yake hayakuwa kuendeleza ukoloni. Malengo yake yalikuwa kusaidia kujenga mfumo wa kiuchumi ulio bora zaidi katika dunia. Na upo ushahidi kuwa malengo ya shirika hilo yanafanikiwa katika kila nchi inayofuata mfumo huu ambao umejitofautisha na mifumo mingine ambayo imekufa, ama imeshindwa kushindana vizuri na huo mfumo.
Tunamsifu Mwalimu Nyerere kwa mazuri aliyoyafanya. Tunafukia mabaya kwa sababu si akili nzuri kukuza madhaifu ya mtu mwenye mengi mazuri. Wewe unanilazimisha kujadili mabaya ya Nyerere ili nikuoneshe kuwa "withdrawal" katika eneo la utawala uambao unashindwa kukubaliana nao katika kila kitu si kukimbia vita. Withdrawal inawezekana kabisa ikawa tactical; ni sahihi kabisa mtu kuondoka eneo la mabishano ampatie mbishani wake nafasi ya kushindwa, ili wazo lake lipate nafasi ya pili na kuthibisha alikuwa na wazo bora zaidi.
Edwin Mtei ni mzalendo aliyekuwa na wazo zuri ambalo ndo hilo tunalitekeleza sasa. Pengine yeye binafsi atakuwa na maelezo tofauti na haya kuelezea sababu zake za kutoweka katika vipindi unavyovieleza, lakini ninachojua ni kwamba alifanya vizuri kumwacha Nyerere kutekeleza wazo lake ambalo halikuwa likikubalika na Mtei kwa asilimia zote, hadi pale lilipofikia kuonesha halikuwa wazo sahihi kwa asilimia 100.
Angalizo ni maneno haya: Tactical Withdrawal, na hii inaruhusiwa katika mazingira ya mabishano.
Kumbe wewe ndiye usiyejua historia. Hujui kuwa Edwin Mtei alikuwa mtumishi mtiifu wa serikali ya mkoloni.
Hujui kuwa Edwin Mtei alikataa kusaidia kazi za kuendeleza TANU. Na wala hujui kuwa machief wengi hawakuipenda TANU.
Kukubali serikali ya mkoloni sio lazima asimame jukwaani na kusema "jamani mimi naivumilia serikali ya mkoloni", kitendo cha yeye kutokushiriki shughuli yoyote ya kuondoa ukoloni na kuitumikia serikali ya mkoloni kwa utiifu ni kuikubali tosha.
HAKUNA jambo alilofanya Mzee Edwin Mtei kwa kujitolea. Kila alichokifanya alilipwa mshahara mnnono. Huo si uzalendo, ni kutafuta ajira tu kama jinsi mtanzania anavyoweza kwenda leo Afrika Kusini kutafuta kazi haimaanishi anaipenda Afrika Kusini.
Swala la Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuwa na mapungufu yake haliwezi kuwa sababu tosha ya Mzee Mtei kulitelekeza Taifa. Inamaana Mzee Mtei alivumilia mapungufu ya Mwalimu mpaka siku nchi ilipopatwa na ugumu wa uchumi uliotokana na vita ndio akashindwa kuvumilia! Mtei alilitelekeza taifa, hakutaka elimu yake ilinufaishe taifa. Mzee Mtei ni mbinafsi wa kupindukia na historia ya maisha yake inadhihirisha hilo.
Ndio maana nawatahadharisha vijana kuwa chadema haijaanzishwa na mtu mwema kwa taifa na HAWEZI kuwa na malengo mema kwa taifa. Vijana msikubali kulaghaika...