Ahadi kumi (10) za mwana TANU na Tanzania yetu ya sasa

-Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja??????? -Nitajielimisha kwa kadri ya uwezo wangu na kutumia elimu yangu kwa faida ya wote????? KWELI MWANATANU KATUPWA KAPUNI.

binadamu wote ni sawa kila mtu aheshimiwe.
ashiriki sawa katika ujenzi wa taifa.
 
Kwani wakati wa Nyerere ilikuwa hamna rushwa? huyo aliye ziandika hizo ndiye aliyepalilia rushwa kuwepo Tanzania.
 
Kwani wakati wa Nyerere ilikuwa hamna rushwa? huyo aliye ziandika hizo ndiye aliyepalilia rushwa kuwepo Tanzania.

asubuhi namna hii pombe za nini? piga supu, chai nzito na akili itakaa sawa!
 
Kwani wakati wa Nyerere ilikuwa hamna rushwa? huyo aliye ziandika hizo ndiye aliyepalilia rushwa kuwepo Tanzania.

Bila shaka rushwa ilikuwepo Ribosome lakini sio katika kiwango cha sasa. Inatisha!! Bila kujali kuwa rushwa ilikuwepo zamani au la, hitaji la nchi yetu kwa sasa ni viongozi wenye maadili ambao wataweza kutumia rasilimali tulizonazo kwa ajili ya manufaa ya wananchi wote. Viongozi hao tuwatengeneze, tuwaweke madarakani, halafu tuvune tulichopanda.
 
1) Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja,
2) Nitaitumikia nchi yangu na watu wake wote;
3) Nitajitolea nafsi yangu kuondoa umasikini,ujinga,magonjwa na dhuluma,
4) Rushwa ni adui wa haki.Sitapokea wala kutoa rushwa,
5) Cheo ni dhamana,sitakitumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu,
6) Nitajielimisha kwa kadri ya uwezo wangu na kutumia elimu yangu kwa faida ya wote,
7)
Nitashirikiana na wenzangu wote kuijenga nchi yetu,na;
8) Nitasema kweli daima,fitina kwangu mwiko.

Waache mipasho mjengoni watoe hoja za kujenga na sio kwenda nje ya mada.CCM wamekuwa na tabia ya kufrastrate wabunge wa upinzani ili watoke nje ya mada na muda wa kujadili unakwisha bila hoja za msingi na mwishowe kupitisha bajeti mbofu mbofu.

Nchi ni ya kwetu wote sio CCM ,CDM au vinginevyo ,Tushirikiane wote bila kujali itikadi ya vyama katika Kujadili mambo ya yanayohusu mustakabali wa nchi yetu.

Peoples power
 
Umenikumbusha darasa la tatu. Ilikuwa ni lazima kuahidi hizi ahadi "mstarini" kabla hamjaingia darasani!
 
Wakuu
Hizi ni ahadi kumi (10) za TANU ambazo zinatumiwa na wana ccm na bado wanajivunia kuwa nazo

1. Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja.

2. Nitaitumikia nchi yangu na watu wake wote

3. Nitajitolea nafsi yangu kuondoa umaskini, ujinga, magonjwa na dhuluma.

4. Rushwa ni adui wa haki. Sitapokea wala kutoa rushwa.

5. Cheo ni dhamana. Sitakitumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu.

6. Nitajielimisha kwa kadiri ya uwezo wangu na kutumia elimu yangu kwa faida ya wote.

7. Nitashirikiana na wenzangu wote kuijenga nchi yetu.

8. Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko.

9. Nitakuwa mwanachama mwaminifu wa TANU na raia mwema wa Tanganyikana
Afrika.

10. Nitakuwa mtiifu na mwaminifu kwa Rais wa Serikali ya Tanganyika.

Ahadi hizi zingetekelezwa hata kwa asilimia kumi (10%) tu, naamini Tanzania ingekuwa mbali sana.

ANGALIA ZINAVYO VUNJWA.

Hapa ni mnyambulisho wa uhalisia wa kinachofanyika sasa. Ni mawazo ya nguli Mobhare Matinyi.

1.
Binadamu wote ni ndugu zangu
na Afrika ni
moja...............hapana, angalia
dini kwanza.

2.
Nitaitumikia nchi yangu na watu
wake wote..... nitaitumikia
familia yangu na washikaji
zangu wote.

3.
Nitajitolea nafsi yangu kuondoa
umaskini, ujinga, magonjwa na
dhuluma..........................kuondoa
maadili yote ya taifa hili.

4.
Rushwa ni adui wa haki.
Sitapokea wala kutoa
rushwa..............rushwa ni
sehemu ya maisha, nitapokea
na kutoa kila ninapopata nafasi.

5.
Cheo ni dhamana. Sitakitumia
cheo changu wala cha mtu
mwingine
kwa faida yangu..............Cheo ni
ulaji; watanikoma.

6.
Nitajielimisha kwa kadiri ya
uwezo wangu na kutumia elimu
yangu
kwa faida ya
wote.....................nitaiba vyeti
na kugushi majina.

7.
Nitashirikiana na wenzangu
wote kuijenga nchi
yetu................nitashirikiana na
wageni kuibomoa nchi.

8.
Nitasema kweli daima, fitina
kwangu mwiko......nitasema
uongo, nitakuwa mfitini,
nitapenda majungu, na nitakuwa
mzushi.

9.
Nitakuwa mwanachama
mwaminifu wa TANU na raia
mwema wa Tanganyika na
Afrika.....................nitakuwa
mwanachama mwaminifu wa
makundi ya mafisadi na raia
mwizi.

10.
Nitakuwa mtiifu na mwaminifu
kwa Rais wa Serikali ya
Tanganyika..............................nitakuwa
mtiifu kwa wanaonihonga.

Maskini nchi yetu! Tuipiganie
sasa!

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums.
 
Ikumbukwe pia kuwa Mzee Ediwn Mtei mwanzilishi wa chadema alikataa kushirikia katika harakati za TANU za kutafuta Uhuru wa Tanganyika. Alikuwa mtumishi mtiifu wa serikali ya wakoloni na aliona kupigania uhuru ni kuharibu utawala unaompa mshahara kila mwezi.

Kwahiyo kiufupi ni kwamba mwanzilishi wa chadema mzee Mtei aliona ahadi hizo za TANU hazina manufaa.
 
Hapana. Nadhani aliona zimevurugwa badala ya kuzienzi na kuziboresha

You are missing a point. Mtei alikuwa kijana ambaye alipaswa kushiriki kuiboresha TANU. Yeye alikataa kwa sababu zake binafsi. Aliona utawala wa mkoloni unavumilika na kwamba TANU haina manufaa. Wasomi walikuwa wachache sana Mtei akiwa mmoja wao, lakini alilitelekeza taifa.

Baada ya Uhuru alipewa ajira na serikali. Hali ya uchumi ilivyoyumba kutokana na vita ya Uganda akalitelekeza taifa tena.

Yaani muasisi wa chadema mzee Edwin Mtei, kila pale taifa lilipomuhitaji alilitelekeza. Yeye alifurahi ajira ya mshahara mnono toka serikali si kufunga mkanda kujenga nchi.
 
We ZeMarcopolo, cdm itakupasua kichwa, unalala kweli?

Huu ni mjadala wa TANU na vijana waliokuwepo enzi za TANU. Sio mjadala wa chadema.

Mzee Mtei alipata fursa ya kulidhihirishia taifa kuwa anajali maslahi ya taifa, lakini alionyesha opposite.

Malengo yake siko zote hayajawa mazuri. Ndio maana amekuwa akitoa kauli zinazoonyesha his true colours. Kauli ambazo chama chake cha chadema kimefedheheshwa nazo kiasi cha kutoa matamko ya kujitenga nazo.

Chadema ikiendelea kuwa chini ya influence ya Mzee Edwin Mtei haiwezi kuwa na lengo la kuleta ustawi kwa watanzania wote. Mwananchi USILAGHAIKE...
 
You are missing a point. Mtei alikuwa kijana ambaye alipaswa kushiriki kuiboresha TANU. Yeye alikataa kwa sababu zake binafsi. Aliona utawala wa mkoloni unavumilika na kwamba TANU haina manufaa. Wasomi walikuwa wachache sana Mtei akiwa mmoja wao, lakini alilitelekeza taifa.

Baada ya Uhuru alipewa ajira na serikali. Hali ya uchumi ilivyoyumba kutokana na vita ya Uganda akalitelekeza taifa tena.

Yaani muasisi wa chadema mzee Edwin Mtei, kila pale taifa lilipomuhitaji alilitelekeza. Yeye alifurahi ajira ya mshahara mnono toka serikali si kufunga mkanda kujenga nchi.

Kwa kifupi mzee mtei alikuwa ni bepari toka enzi za ujana wake aliamini ubepari mwanzo mwisho hizi sera za TANU na mlengo wake wa kijamaa kwa mtei aliona kabisa zitamuondolea ulaji. Ndio maana akijirimbikizia mali mpaka kupata uwezo wa kuanzisha chama...ni hayo tu kwa leo.
 
Ndio maana nawashangaa vijana wanaotoka katika jamii masikini wanaolaghaika kuwa chadema imeanzishwa kwa ajili ya kuwasaida kimaisha!

Vijana hawa wanajiingiza kwenye mtego ambao wakinasa watajuta mno...
 
Mkuu genekai hebu mwache ZeMarcopolo niongee naye. Kwa bahati nzuri nina bundle zangu za kutosha leo na muda wa kubishana naye ZeMarcopolo ninao.

We ZeMarcopolo, cdm itakupasua kichwa, unalala kweli?

You are missing a point. Mtei alikuwa kijana ambaye alipaswa kushiriki kuiboresha TANU. Yeye alikataa kwa sababu zake binafsi. Aliona utawala wa mkoloni unavumilika na kwamba TANU haina manufaa. Wasomi walikuwa wachache sana Mtei akiwa mmoja wao, lakini alilitelekeza taifa.

Baada ya Uhuru alipewa ajira na serikali. Hali ya uchumi ilivyoyumba kutokana na vita ya Uganda akalitelekeza taifa tena.

Yaani muasisi wa chadema mzee Edwin Mtei, kila pale taifa lilipomuhitaji alilitelekeza. Yeye alifurahi ajira ya mshahara mnono toka serikali si kufunga mkanda kujenga nchi.

Context ya Kipindi cha Mtei ipo kama ifuatavyo. Wasomi walikuwa wachache kweli. Nyerere na Mtei wakiwapo katika kundi hili la wasomi wachache. Nyerere alikuwa mmoja katika Watanganyika wenye vipaji vya uongozi wakati huo. Lakini hakuwa peke yake mwenye kipaji.

Maelezo yako yenye mapungufu ni pamoja na haya: Kwamba Mtei aliona utawala wa mkoloni unavumilika. Haya ndiyo unayoyasema wewe ZeMarcopolo. Na kwamba kila pale taifa lilipomuhitaji alilitelekeza. Hali ya uchumi ilivyoyumba kutokana na vita ya Uganda akalitelekeza taifa tena.

Maelezo yako wewe ZeMarcopolo yanatuambia wasomaji wako kwamba hujui historia, hujui dhana ya ushindi katika vita hutegemea falsafa zipi.

Hakuna Mtanganyika aliyekubali kuwa ukoloni ulikuwa unavumilika. Wewe ZeMarcopolo huna ushahidi popote kuonesha kuwa Mtanganyika mmoja kwa jina la Edwin Mtei alitaka ukoloni uendelee. Kama unao ushahidi huo uweke hapa. Tukio la Mtei kufanya kazi katika Shirikia la Kimataifa haliwezi kuwa kigezo cha kuvumilia ukoloni kwa kuwa Shirika alilofanya kazi nalo malengo yake hayakuwa kuendeleza ukoloni. Malengo yake yalikuwa kusaidia kujenga mfumo wa kiuchumi ulio bora zaidi katika dunia. Na upo ushahidi kuwa malengo ya shirika hilo yanafanikiwa katika kila nchi inayofuata mfumo huu ambao umejitofautisha na mifumo mingine ambayo imekufa, ama imeshindwa kushindana vizuri na huo mfumo.

Tunamsifu Mwalimu Nyerere kwa mazuri aliyoyafanya. Tunafukia mabaya kwa sababu si akili nzuri kukuza madhaifu ya mtu mwenye mengi mazuri. Wewe unanilazimisha kujadili mabaya ya Nyerere ili nikuoneshe kuwa "withdrawal" katika eneo la utawala ambao unashindwa kukubaliana nao katika kila kitu si kukimbia vita. Withdrawal inawezekana kabisa ikawa tactical; ni sahihi kabisa mtu kuondoka eneo la mabishano ampatie mbishani wake nafasi ya kushindwa, ili wazo lake lipate nafasi ya pili na kuthibisha alikuwa na wazo bora zaidi. Wewe ulitaka Mtei afanye nini wakati mawazo yake yanakataliwa.

Edwin Mtei ni mzalendo aliyekuwa na wazo zuri ambalo ndo hilo tunalitekeleza sasa. Pengine yeye binafsi atakuwa na maelezo tofauti na haya kuelezea sababu zake za kutoweka katika vipindi unavyovieleza, lakini ninachojua ni kwamba alifanya vizuri kumwacha Nyerere kutekeleza wazo lake ambalo halikuwa likikubalika na Mtei kwa asilimia zote, hadi pale lilipofikia kuonesha halikuwa wazo sahihi kwa asilimia 100.

Angalizo ni maneno haya: Tactical Withdrawal, na hii inaruhusiwa katika mazingira ya mabishano.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom