Ahadi kumi (10) za mwana TANU na Tanzania yetu ya sasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ahadi kumi (10) za mwana TANU na Tanzania yetu ya sasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mwankuga, Dec 25, 2010.

 1. mwankuga

  mwankuga JF-Expert Member

  #1
  Dec 25, 2010
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Chama cha TANU ni chama kilichosaidia sana katika harakati za kuikomboa nchi yetu katika makucha ya ukoloni chini ya Uongozi madhubuti wa Hayati Julius K. Nyerere.

  Malengo makubwa ya chama hiki ilikuwa ni ukombozi wa nchi yetu lengo ambalo kwa kiasi kikubwa lilitimia.Kinachonofurahisha sana ni jinsi viongozi wa TANU walivyokuwa na dhamira za kweli na kujitolea kwa hali na mali katika kuikomboa nchi yetu.

  Lengo kubwa la post hii, ni kuwakumbusha wana JF Ahadi za Mwana TANU, na kama bado ni relevant kwa wakati huu ambapo Tanganyika(Tanzania) imefikisha miaka 49 ya uhuru, zifuatazo ni ahadi za Mwana TANU enzi hizo:

  F25663D5-A6EC-4E4C-B4C1-122C4D9214A6.jpeg

  1. Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja.

  2. Nitaitumikia nchi yangu na watu wake wote

  3. Nitajitolea nafsi yangu kuondoa umaskini, ujinga, magonjwa na dhuluma.

  4. Rushwa ni adui wa haki. Sitapokea wala kutoa rushwa.

  5. Cheo ni dhamana. Sitakitumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu.

  6. Nitajielimisha kwa kadiri ya uwezo wangu na kutumia elimu yangu kwa faida ya wote.

  7. Nitashirikiana na wenzangu wote kuijenga nchi yetu.

  8. Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko.

  9. Nitakuwa mwanachama mwaminifu wa TANU na raia mwema wa Tanganyika na Afrika.

  10. Nitakuwa mtiifu na mwaminifu kwa Rais wa Serikali ya Tanganyika.​

  Je, ahadi hizi za Mwana TANU zimeendelezwa na CCM au ndio zimepigwa dafrao?

  Sisi kama Taifa hatuwezi kuziendeleza na kuzitekeleza ahadi hizi na kuzifanya kuwa ni za kitaifa kuliko kuwa za chama?

  Lengo la post hii ni kuchochea mjadala ili kuona namna gani nchi yetu inaweza kujikwamua kutoka katika umasikini huu tulionayo kama taifa.

  Naomba kuwasilisha wadau
   
 2. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #2
  Dec 25, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Umefanya vizuri kutukumbusha mambo hayo. Unaonaje tukashirikiana kuanzisha chama cha siasa kwa jina la C.C.M- HALISI ambacho tofouti na ccm maslahi ya sasa kitazingatia kwa kauli na vitendo meme yote ya TANU.
   
 3. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #3
  Dec 25, 2010
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  KWA MTAZAMO WANGU...ujumbe umeenda sawia kabisa...ila ikafika mahali ukamtafuta mchawi wako na ukampata(CCM ),........ILA UKITOA KIPENGELE CHA CCM......KWANGU ITAKUWA NI KATI YA POSTI BORA ZA KIZALENDO ZENYE KUJENGA UMOJA NA KULETA MWAMKO WA KIZALENDO KWA NCHI NA SI CHAMA....!
   
 4. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #4
  Dec 25, 2010
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  hapo kwenye bold ingetoka ili mjadala uwe moto
   
 5. mwankuga

  mwankuga JF-Expert Member

  #5
  Dec 25, 2010
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Watanzania tufike mahala tutambue matatizo yanayotukabili.Kimsingi tukubaliane kuwa CCM kama chama cha siasa kimeshindwa katika kukabiliana na maadui wetu watatu ambao ni ujinga,maradhi na magonjwa,na rushwa (nyongeza).Serikali imebaki kuwa gulio la watu wenye hamu ya kuishi peponi ilihali wako peponi.Cheo ni dhamana tena bali ni zawadi,vyeo vinagawiwa kwa marafiki,vimada na wote wanaochangia mkuu kupata madaraka.

  Kimsingi hatuhitaji kuwa na utitiri wa vyama vya siasa ambavyo mipango madhubuti ya kushika dola na kufanya mambo ambayo chama tawala kimeshindwa.Ni vyema tukaunga mkono harakati zinazofanywa na vyama vya upinzani.Kwa sasa,na wala sio siri kwamba CHADEMA ndicho kinaonekana chama mbadala(Kwa mtazamo wangu).
   
 6. mwankuga

  mwankuga JF-Expert Member

  #6
  Dec 25, 2010
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Lengo kuu la post hii ni kujaribu kuwakumbusha japo kidogo wana JF kule tulikotoka.Kuitaja CCM haiwezi kuwa dhambi,na sijaitaka kama nai-praise bali TANU na CCM ni sehemu ya historia yetu.Na hapa ni kwamba CCM kama cha tawala kimeshindwa kutimiza ndoto za watanzania.Viongozi wa sasa ni viongozi masirahi,ambao hawaguswi moja kwa moja na matatizo ya wananchi.Tuungane kwa pamoja katika harakati za kuwaondoa hawa makabulu(CCM)
   
 7. mwankuga

  mwankuga JF-Expert Member

  #7
  Dec 25, 2010
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Dhana ya kufikiri na kujiuliza(the art of thinking and reasoning) ni muhimu sana katika taifa letu hili ambalo kwa miaka 49 ya uhuru bado mambo yetu dolo sana.Nimeuliza kuwa kwa kiasi gani CCM imetimiza malengo ya uanzishwaji wake.Jibu liko wazi lakini ili kuufanya mjadala kuwa wazi zaidi sikutaka kuhitimisha.Lakini nashukuru kwa mchango wako.
   
 8. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #8
  Dec 26, 2010
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  MWANKUNGA.....THAT MEANS MCHAWI WA MAENDELEO NI CCM......na si ahad za mwana-TANU......NI ANTI-CCM POST na sio post ya kutafuta wapi kama taifa tulikosea na wapi kama wananchi watiifu wa taifa letu tumepotoka...CCM kama CCM wao sio manesi, madaktari, wafanyabiashara, watoza ushuru (TRA), sumatra,tanesco,dawasco, PCCB,JWTZ,POLISI,MAGEREZA,MAHAKAMA,TUME YA UCHAGUZI,UHAMIAJI,JKT,WALIMU, MAJEMBE,ISP(INTERNET),DAR EXPRESS, SCANDINAVIA, WAUZA DUKA,VIBAKA, WAPATA AJALI(MAJERUHI) the list is long.........!
  Kama taifa na watu wa makundi yatoayo huduma haijalishi mtu ni CCM ama lA.......AHADI ZA MWANA TANU NI ZA MTU BINAFSI KUTEKELEZA SIO CCM MKUBWA......UKITEKELEZA AHADI HIZO UTAKUWA UMEIFANYIA VYEMA NCHI YAKO NA SIO CCM.....NA UKISHINDWA KUTEKELEZA SIO CCM NDO IMESHINDWA.....BUT IT REMAINS THE BEST ANT-CCM POST THAN WHAT IT SEEMS TO BE
   
 9. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #9
  Dec 26, 2010
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Wengi wetu tunafuata maslahi kwa ajili ya matumbo yetu hata kama ni kusema uongo.
   
 10. mwankuga

  mwankuga JF-Expert Member

  #10
  Dec 26, 2010
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Mkuu nimekusoma,mchaango wako ni mzuri,kimsingi tuko pamoja katika harakati za ukombozi wa nchi yetu kutoka mikononi mwa watu wachache(mafisadi)
   
 11. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #11
  Dec 26, 2010
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  nadhani mwankuga na mahesabu mna hoja nzito sana, mkiziunganisha tukapata hoja katika set moja, mie niko tayari hata kuchukua kadi namba moja ya hicho chama kipya kitakachoanzishwa
   
 12. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #12
  Dec 26, 2010
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Hizi ahadi kakobe alisha zipinga kwenye kipindi chake cha rushwa na kusema ni usanii. Kakobe alisema ccm imepoteza mwelekeo wa maadili na kukumbatia wafanya biashara wala rushwa
   
 13. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #13
  Dec 26, 2010
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135

  Huyo Kakobe ndie msanii namba moja! Mafisadi anawajua na wengine ni watoa sadaka wakubwa kanisani kwake!

  Hizi ahadi zilikuwepo hata kabla ya huo ufisadi unaolitafuna taifa letu, sana sana ni mafisadi wenyewe ndio wasiopenda kuzisikia.
   
 14. M

  Makyomwango JF-Expert Member

  #14
  Jul 9, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 323
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tafadhali nape na wanamagamba wengine rejeeni kusoma ahadi aliyokuwa anatoa mwnanachama wa TANU mara baada ya kumaliza mafunzo ya kujiunga na chama na kila mmojawenu ajihoji mwenyewe na aangalie position ya wanamagamba wengine.
  (1) Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja
  (2) Nitaitumikia nchi yangu na watu wake wote
  (3) Nitajitolera nafsi yangu kuondosha umaskini, ujinga, magonjwa na dhuluma.
  (4) Rushwa ni adui wa haki, sitapokea wala kutoa rushwa.
  (5) Cheo ni dhamana, sitatumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu.
  (6) Nitajielimisha kwa kadri ya uwezo wangu na kuitumia elimu yangu kwa faida ya wote.
  (7) Nitashjirikiana na wenzangu wote kujenga nchi yetu.
  (8) Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko.
  (9) Nitakuwa mwanachama mwaminifu wa CCM na raia mwema wa Tanzania na Afrika.


  Baada ya kujihojini kwa kigezo cha ahadi mlizozirithi kutoka TANU fanyenin maamuzi sahihi. Naamini kama akili zenu ni timamu, si za kifisadi na kibinafsi, kamwe hamtabaki katika chama cha majambazi (CCM) ambao kukicha wanawapora masikini watannganyika rasilimali zao na kuzipeleka ughaibuni kama kisiwa cha jersey uingereza
   
 15. Mkwawa

  Mkwawa JF-Expert Member

  #15
  Jul 9, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,290
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 160
  Unajua wazee waliokufa miaka ya tisini walikuwa wazalendo sana. Hizo ahadi zilikuwa na mashiko, utu na kujali nchi na vizazi vyote. Wazee tulioachiwa sisi ni waajabu sana, wezi, wafitini, hawana busara, hakuna cha kujifunza kutoka kwao zaidi ya Rushwa, dhuluma, uongo, uhujumu, ukosefu wa nidhamu na madhila yote.

  Hizo ahadi aziwahusu kwani watakwambia wao sio Tanu ni CCM mpya, CCM-Magamba. Hawafai wala hawazitaki hizo ahadi.

  Nimezipenda hizo ahadi isipokuwa ya Mwisho siitaki wala kuiona.
   
 16. B

  Bijou JF-Expert Member

  #16
  Oct 13, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,177
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Hii wanajamii kesho ni kumbukumbu ya miaka 12 tangu baba wa taifa afariki dunia, katika kumbukumbu hiyo, kila mmoja wetu kama ni mtumishi wa umma, sekta binafsi, mjasiriamali na hata mkulima, hebu tutafakari ibara ya 5 ya mwana tanu:-

  "cheo ni dhamana sitakitumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa ajili ya manufaa yangu"


  je kati yetu kwa moyo mweupe kabisa na akijua mwenyezi mungu anamuangalia toka juu, atasema nini kwa ukweli wake kabisa??????


  Tuchangie
   
 17. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #17
  Oct 13, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Hiyo ililelenga kweli.............Siku hizi wanatumia vyeo vyao kujinufaisha na ndugu zao wananufaika pia...............!
   
 18. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #18
  Apr 27, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,672
  Trophy Points: 280
  1 Nitasema kweli daima.2 Sitatoa wala kupokea rushwa.3 Sitatumia cheo changu kwa manufaa yangu binafsi.4 Nitaheshimu utu wa mtu. . . . .Leo ahadi hizi zimekua kama ndoto fulani uliota na sasa umestuka hakuna kitu!Kwa mtindo ulivyo sasa hata Mungu ameshatuchoka!
   
 19. CHUAKACHARA

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #19
  Apr 27, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,825
  Trophy Points: 280
  Mawziri wa Kikwete wasimame msitari mmoja warudie maneno hayo! Nani kati yao atasimama kama siyo hukumu ya shetani kumwangukia. Ezekiel Maige upio?
   
 20. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #20
  Apr 27, 2012
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  -Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja???????
  -Nitajielimisha kwa kadri ya uwezo wangu na kutumia elimu yangu kwa faida ya wote?????
  KWELI MWANATANU KATUPWA KAPUNI.
   
Loading...