Habari wana JF.
Niko kwenye mahusiano ya kimapenzi na kijana mmoja kwa muda wa miezi takribani minne sasa. Tuko katika kuchunguzana tabia kabla ya kuamua kufunga ndoa. Kwa bahati mpaka sasa tunaendelea vizuri na hakuna mgogoro uliowahi kutokea baina yetu.
Huyu rafiki yangu anatabia ya kunywa pombe mpaka kulewa hasa siku za mwisho wa wiki. Na akishalewa huanza kunisifia kuwa ananipenda sana, anatoa ahadi za kufungua biashara, kufunga ndoa siku za karibuni na ahadi zingine kem kem.
Akiwa hajalewa haongei mambo yote haya, huwa yuko kimya. Mimi nasita kuumuliza kama mambo ambayo huwa anaongea wakati akiwa amelewa anayakumbuka na kama huwa yanatoka moyoni. Nasita kumuuliza kwa sababu sipendi utokee mgogoro kati yetu kipindi hiki.
Nimekuja hapa JF kuomba msaada kwa wenye uzoefu na watu wenye tabia za ulezi wa pombe. Je mambo anayozungumza mtu wakati akiwa amelewa pombe, huwa yanatoka moyoni kwake na ni vema yazingatiwe au ni ya kupuuzwa?
Asanteni kwa ushauri. Samahani kama nitakuwa nimemkwaza mtu katika hili.