Ahadi anazotoa mtu akiwa amelewa pombe

Ahadi anazotoa mtu akiwa amelewa pombe

esterjohn

Senior Member
Joined
Dec 6, 2012
Posts
150
Reaction score
35
Habari wana JF.

Niko kwenye mahusiano ya kimapenzi na kijana mmoja kwa muda wa miezi takribani minne sasa. Tuko katika kuchunguzana tabia kabla ya kuamua kufunga ndoa. Kwa bahati mpaka sasa tunaendelea vizuri na hakuna mgogoro uliowahi kutokea baina yetu.

Huyu rafiki yangu anatabia ya kunywa pombe mpaka kulewa hasa siku za mwisho wa wiki. Na akishalewa huanza kunisifia kuwa ananipenda sana, anatoa ahadi za kufungua biashara, kufunga ndoa siku za karibuni na ahadi zingine kem kem.

Akiwa hajalewa haongei mambo yote haya, huwa yuko kimya. Mimi nasita kuumuliza kama mambo ambayo huwa anaongea wakati akiwa amelewa anayakumbuka na kama huwa yanatoka moyoni. Nasita kumuuliza kwa sababu sipendi utokee mgogoro kati yetu kipindi hiki.

Nimekuja hapa JF kuomba msaada kwa wenye uzoefu na watu wenye tabia za ulezi wa pombe. Je mambo anayozungumza mtu wakati akiwa amelewa pombe, huwa yanatoka moyoni kwake na ni vema yazingatiwe au ni ya kupuuzwa?

Asanteni kwa ushauri. Samahani kama nitakuwa nimemkwaza mtu katika hili.
 
Pombe zinamfanya mtu kujiamini na kujiona kila kitu, iishapo pombe hiyo hali hutoweka na kurudi katika origin yake.
 
ahadi na maneno yanayomtoka mlevi huwa ni ulevi, huishia kwenye ulevi. Usisite kumuuliza akiwa hajalewa ili ujiridhishe lakini hamna kitu hapo.
 
Asante Happiness win kwa ushauri. Nitamuuliza akiwa hajalewa nijiridhishe, liwalo na liwe!
 
Tafuta eneo la biashara,mvizie siku ana hela mleweshe then unambeba mbio mbio hadi eneo la biashara ...mwite mwenye eneo mwambie mzee kaja kulipa leo....ukitoka hapo mbiooo msobemsobe hadi duka la jumla....
 
Asante mkuu Kiteitei!! Ninavyomuelewa Jamaa hata kama hajalewa anaweza tu kufungua biashara. Ila tatizo simwelewi kama ananipenda kwa dhati au la. Kwani huwa anatamka kuwa ananipenda akiwa amelewa, hali akiwa hajalewa huwa hatoei maneno hayo japo bado tuko pamoja na tunaendelea vizuri na uhusiano wetu
 
Tafuta eneo la biashara,mvizie siku ana hela mleweshe then unambeba mbio mbio hadi eneo la biashara ...mwite mwenye eneo mwambie mzee kaja kulipa leo....ukitoka hapo mbiooo msobemsobe hadi duka la jumla....

haaahaahaa! Dah u a so creative! Ila pombe ikiisha ujue mwenzako hana ndoa! We mchuze tu!
 
Ila hzo ni pombe tu mamito! We mngje akiwa mzima ndo umuulize usijiridhshe na pombe zake!
 
Akiwa hajalewa huwa yuko serous ile mbaya!! Akiongea neno moja amemaliza. Anyway nitamuuliza ili nijiridhishe
 
Esther mpendwa 4 months is too early..tena ogopa sana mwanaume anayetoa ahadi akiwa amelewa.

Sijui nikuambiaje ila hii imenicost sana..be careful yasijekukuta yaliyonikuta mimi kwa mtu wa that nature.best of lucky!!!
 
Tafuta eneo la biashara,mvizie siku ana hela mleweshe then unambeba mbio mbio hadi eneo la biashara ...mwite mwenye eneo mwambie mzee kaja kulipa leo....ukitoka hapo mbiooo msobemsobe hadi duka la jumla....

hahaa nimecheka kwakweli ila samahani,NO OFFENSE
 
Ester john nd umekuja knisema hku.
 
Last edited by a moderator:
mapenzi yenu yanaongozwa na pombe, maana bila pombe I LOVE U haipo habari za ndoa hamna nawewe umeridhika tu.

Funguka mamaa kabla hajajitoa ufahamu, mkalishe kitako kuhusu habari ya mapenzi yenu na hizo ahadi, ukimuona mijicho imemtoka bila usemi, jua ni wizi mtupu!!!!!!!!
 
Hapana Mabumbe, sijaja kukusema ila najaribu kupata ushauri kwa wazoefu kwani upendo wako nauona zaidi wakati ukiwa umelewa. Ukiwa sober uko very quite! Any way this is a feedback to you. Work on it sir!
 
Nachojua mimi ...pombe humfanya mtu aongee kitu anachoshindwa kuongea akiwa sober ....kwa kifupi pombe inampa ujasiri wa kutenda au kuongea ......lakini usiiamini sana pombe inawezekana mawazo yake huwa anawaza utamkimbia so anaona noma akiwa mkavu kuanza kukupanga kwa uongo
 
Kitu kingine kilichonisukuma kuja kuomba msaada hapa JF ni kuwa, kwa uzoefu wangu nimeona wanaume wengi walevi huwasumbua wake zao pindi wanapokuwa wamelewa. Wakiwa hawajalewa hali ni shwari. Huyu wangu ni tofauti. Akiwa amelewa upendo unakuwa juu. Akiwa hajalewa anakuwa kawaida sana
 
Dah! mimi sijui nimezeeka sana,
Ukweli ni kwamba mtu asikwambie eti nimelewa ndo maana nimefanya jambo fulan yaani huo uwe ni mwiko kwako bibie. FYI mlevi huwa anasemaga kile kijazacho moyo wake wa wakati huo tena ambacho haweza kukisema akiwa sober. Mathalan huyu anyesema nitakufungulia biashara ana maanisha ila tu wewe ndo hujamjulia njia, mbananishe siku inayofuata juu ya ahadi aliyokuwekea ili umskie anasemaje.


Pia kunatabia ambayo iko mtu anaweza kukutukana na kukugombeza kisha akasingizia ni pombe. weeeeeeeee bi dada uwe makini sio pombe ila alimaanisha alichokifanya. yaani usiahadaiwe eti ni pombe ndo mana anafanya hivyo huo ni mwiko my dear. jua kwamba huyo anamaanisha ila hawez kusema akiwa sober dawa mshkie chini asbh anapoamka.
 
Asante mkuu gfsonwin kwa ushauri mzuri. Nitambana pombe ikimtoka
 
Thanks Anne
Kuna walevi wengine wakiongea kitu wana maanisha. Hiv wewe kwa uzoefu wa kipindi ambacho mmekuwa pamoja ni mangapi ameyaahidi wakati amelewa na ameshayatekeleza? Kama hakuna jiridhishe na kauli zake usije UKACHINJIWA BAHARINI.
 
Back
Top Bottom