Agizo la Rais ni amri

Hajui halmashauri zinatofautiana rasilimali zipo zenye madini,za mpakani,zenye kilimo na zipo kame zisizo na rasilimali! Kwani kizimkazi inachangia sawa na kahama?
Kutoa fedha kulingana na mapato ni kuvuruga umoja wa nchi na nikubaguana kirasilimali...
Tusiharibiana swaumu kwamaneno mabaya yaubaguzi
 
Juzi Mhe. Rais akiwaapisha Wateule wake alikemea sana wizi unaofanyika Serikalini na baadaye akasema kuwa kuanzia sasa Halmashauri zitapewa fedha kutoka Serikalini kutokana na makusanyo yake.

Mfano kama halmashauri itakusanya 50% basi Serikali itawapa pia 50%.. Agizo la Mhe. Rais ni amri lakini kwa ukweli uanzishwaji wa baadhi za Halmashauri hazikufuata vigezo na hivyo kupelekea kuwa na makusanyo madogo sana.

Tuchukue mfano wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda ambapo ilimegwa na kuanzishwa Halmashauri ya Mji wa Bunda na kupelekea mapato yake kupungua kwa kasi kubwa. Pato kubwa la Halmashauri ya Bunda ni samaki.

Kusema ukweli samaki katika Ziwa Victoria ni kama wamekwisha kabisa na hivyo Halmashauri ya Bunda ni mojawapo ya Halmashauri maskini katika nchi hii na hivyo tunamwomba Mhe. Rais kuwa utafiti wa agizo hili ufanyike kwanza ili kufikia uamuzi wa agizo alilolitoa.

Halmashauri kama Bunda, Rorya, Bumbuli n.k. zitaathirika sana. Mwisho, kuanzia sasa uanzishwaji wa Halmashauri ufuate vigezo vinavyotakiwa na siyo kwa tamaa za wachache kupata ubunge.
Mambo ni mengi,kule Duniani kulikoanzishwa local Government za ukweli Ili kuepuka na tatizo la uendeshaji wa Hamashauri zinafanyiwa tathimini za gharama za kuendesha Hamashauri,yaani Mfano Ili Hamashauri ya Wllaya ijiendedhe inatakiwa iwe na mapato ya bilioni Moja na milioni mia mbili,Sasa kwa zile Hamashauri zisizoweza kukusanya kiasi hicho zinapewa ruzuki na CentralGoverrnment(equalization grants).zinazokusanya zaidi kuvuka ndizo zinapewa top up grants.kama ulivyoeleza Hamashauri zetu zimeanzishwa tu,sio independent,Zina man power hafifu,bajeti zake sio releable,hesabu zake ni za mezani,majukumu yake ni mengi na yanachanganya kwasababu vyanzo vya mapato vinatofautiana kati ya Hamashauri na Hamashauri, wizi mwingi,hizo package/mifumo ya ukusanaji mapato ni dhaifu na vulnerable kwa kuwa inaweza kuchezewa bila ya administrator kutambua.kazi bado ipo sana.
 
Nchi gani Rais wake akiwa madarakani alishtakiwa na kufungwa? Moja!
Rais Richard Nixon wa Marekani alishtakiwa katika scandal ya Watergate akalazimika kujiuzulu vinginevyo angefungwa. Mwingine ni Bill Clinton wa Marekani katika scandal ya ngono na mfanyakazi wa Ikulu Monica Lewinsky ingawa hakufungwa. Joe Biden pia alichunguzwa kwa kuwa na nyaraka za siri za Ikulu.
 
Back
Top Bottom