Agizo la Magufuli laibua utata

Agizo la Magufuli laibua utata

Hivi ni nani amekudanganya kwamba zile bodi zipo pale kuwafanya watu wasiibe?! Hizi bodi zipo kwenye taaluma nyingi tu lakini kanuni na miiko ya kazi kama inavyofundishwa na bodi husika inavunjwa kila leo!! Swali linalobaki ni nini visababishi vya uvunjwaji wa miiko hiyo... ndio hasa tunazungumzia hapa!!
Kitaaluma maana ake nn? Mhasibu anapoiba unadhan nani anampa adhabu? Kama sio bodi kwa either kumfungia au kumfutia uanachama? Ukishafungiwa unafanya kazi wapi tena? Go n google kazi za hizo bodi utaelewa zaid kuliko unavyobishabisha hap
 
Do u have th evidence kwamba hakuna wahasibu askar au mwanajeshi since uhuru? Maana nimesoma na askari weng sasa sijui hua wanaenda wapi
Watunza mahesabu wanaweza kuwa wengi tatizo CPA...nasikia huwezi jiita mhasibu bila CPA (mi siyo field yangu...nasikia tu)

Sasa kwa askari CPA inaweza isiwe priority kama mafunzo ya kijeshi...ukishakuwa na degree CPA ya nini na wewe ni askari?
 
Mkuu BAK with due respect naona chanzo chako cha habari hakisemi ukweli wa jambo hili. Masuala yote ya kijeshi hata utoaji amri yanafuata utaratibu. Amri zitatolewa vipi, na nani na kwa namna gani vyote viko kwenye utaratibu huo na Amri zilizotajwa kwenye utaratibu ni zile zinaoitwa "AMRI HALALI" na siyo kila amri, hivyo ni upotoshaji kwamba eti afande anaweza akamwambia mhasibu ambaye ni mwanajeshi kwamba "Lipa malipo haya na akalipa" hiyo si kweli hata kidogo. Pia ni vizuri ukafahamu kuwa katika Jeshi kuna utaratibu mzuri tu uliyowekwa kwa mwanajeshi kuhoji amri ambayo anafikiri si halali.
mkuu kama ww sio mwanajeshi Kama kimya tuu! amri za kijeshi hazina kuhoji tekekeza uhoji baadae
 
Kitaaluma maana ake nn? Mhasibu anapoiba unadhan nani anampa adhabu? Kama sio bodi kwa either kumfungia au kumfutia uanachama? Ukishafungiwa unafanya kazi wapi tena? Go n google kazi za hizo bodi utaelewa zaid kuliko unavyobishabisha hap
We bhana hoja zako zinachekesha sana!! Let's be honest hapa! Unafanya kazi au bado mwanafunzi?! I am so concerned kwa sababu hoja zako ni za kishule mno!!!
 
Mada hii tayari imejikita kwenye amri zisizo halali... kwahiyo suala la ethics hapo tayari limeshatupwa nje ya mjadala! Mimi sio Mhasibu na wala sina taaluma hiyo! But labda niongee as ex banker linapokuja suala la ethics na tunachozungumzia!

Kwanza, it doesn't matter ikiwa una nyota 7, 5, au 3!! Ukija benki kwa mfano, kisha ukaomba Bank Statement ya mkeo au mwanao nitakunyima so long as you're not a signatory wa account husika na hata power of attorney hauna! Ethics za kibenki zinanikataza kufanya unachotaka! And it doesn't matter hata kama 100% ya deposits za akaunti husika zinafanywa na wewe... SITAKUPA! Na wewe huwezi kunifanya chochote.
Kinyume chake, assume bank ya serikali wafanyakazi wa kiraia wameondolewa na kuletwa wafanyakazi maaskari! In no time, anakuja mjomba Mwamunyange hadi kaunta ambako kuna Sajenti wa JWTZ! Mjomba Mwamu anataka statement ya mkewe ingawaje yeye sio signatory na hata power of attorney hana!!Hivi kabisa unaamini huyu Sajenti atakuwa na ubavu wa kumkatalia mjomba Mwamu?husu sheria za uhasibu zipo pale pale bila kujali ikiwa wewe ni raia au mjeda! Tatizo linakuja na msukumo wa kuvunja hiyo miiko ya uhasibu!
Ethics kutupwa nje au wewe ndo hutak kukubali ukweli? Huwez kuongelea kazi za kihasibu ukaacha ethics ndugu, na kama ingekua hvyo humu maofisini ingekua ni vurugu tu maana kila familia ya bosi ingekua inakupa amri, au mawaziri na makatibu wakuu wangekua wanafanya watakavyo si ni mabosi? Lakini mbona wakivunja sheria wanawajibishwa? No one is above the law hata uwe nani, ndo mana kuna sheria na taratibu, hakuna kitu kimafanyika bila sheria na utaratibu hata iweje ndo mana kila mtu na fani yake, mhasibi atakua mhasibu, mgavu atakua mgavi, na katik utumishi wa umma hakuna amri ya bila maandishi km hujui unless unajipa kesi bure, watu wanafanya kazi kwa mafaili sio mdomo,
 
We bhana hoja zako zinachekesha sana!! Let's be honest hapa! Unafanya kazi au bado mwanafunzi?! I am so concerned kwa sababu hoja zako ni za kishule mno!!!
Lakini zinakutoa kamasi unashindwa kuzijibu unakimbilia defensive mechanism eti hoja za shule, yes hoja za shule koz nimeenda shule, zijibu,
 
Hili swala la wahasibu raia liko kikanuni,kiwaraka kama si kisheria kwa hiyo ili liondoke kama alivyoagiza Mh Rais ni lazima hizo taratibu zilizopo zibadilishwe kwanza na zilwetwe taratibu mpya kulingana na agizo hilo.Kwasababu wahasibu raia waliopo ndiyo wanaotambuliwa na Hazina kwa taratibu,kanuni,nyaraka na sheria zilizopo kwa sasa si jambo rahisi sana kama inavyoweza kusemekana.
 
Mkuu BAK with due respect naona chanzo chako cha habari hakisemi ukweli wa jambo hili. Masuala yote ya kijeshi hata utoaji amri yanafuata utaratibu. Amri zitatolewa vipi, na nani na kwa namna gani vyote viko kwenye utaratibu huo na Amri zilizotajwa kwenye utaratibu ni zile zinaoitwa "AMRI HALALI" na siyo kila amri, hivyo ni upotoshaji kwamba eti afande anaweza akamwambia mhasibu ambaye ni mwanajeshi kwamba "Lipa malipo haya na akalipa" hiyo si kweli hata kidogo. Pia ni vizuri ukafahamu kuwa katika Jeshi kuna utaratibu mzuri tu uliyowekwa kwa mwanajeshi kuhoji amri ambayo anafikiri si halali.
You're talking about the IDEAL, but you're too far from the REALITY
 
Mmmh!! Hii nchi inamambo mengi sana! Marais watano wa chama kimoja ila sera na malengo ni tofauti kabisa as if niwapinzani. Tatizo ni kubwa kuliko tunavyofikiri!
Tatizo la hii nchi yetu ni kwamba hatuna "NATIONAL PRIORITIES" hiki chama chakavu kinaendesha nchi kwa mihemko;
 
Mada hii tayari imejikita kwenye amri zisizo halali... kwahiyo suala la ethics hapo tayari limeshatupwa nje ya mjadala! Mimi sio Mhasibu na wala sina taaluma hiyo! But labda niongee as ex banker linapokuja suala la ethics na tunachozungumzia!

Kwanza, it doesn't matter ikiwa una nyota 7, 5, au 3!! Ukija benki kwa mfano, kisha ukaomba Bank Statement ya mkeo au mwanao nitakunyima so long as you're not a signatory wa account husika na hata power of attorney hauna! Ethics za kibenki zinanikataza kufanya unachotaka! And it doesn't matter hata kama 100% ya deposits za akaunti husika zinafanywa na wewe... SITAKUPA! Na wewe huwezi kunifanya chochote.

Kinyume chake, assume bank ya serikali wafanyakazi wa kiraia wameondolewa na kuletwa wafanyakazi maaskari! In no time, anakuja mjomba Mwamunyange hadi kaunta ambako kuna Sajenti wa JWTZ! Mjomba Mwamu anataka statement ya mkewe ingawaje yeye sio signatory na hata power of attorney hana!!

Hivi kabisa unaamini huyu Sajenti atakuwa na ubavu wa kumkatalia mjomba Mwamu?!

Kuhusu sheria za uhasibu zipo pale pale bila kujali ikiwa wewe ni raia au mjeda! Tatizo linakuja na msukumo wa kuvunja hiyo miiko ya uhasibu!

Kuna tofauti kubwa ya mfano wako ukiwa banker na ukiwa Mwanajeshi. Unatakiwa ujiulize, kwa mhasibu mwanajeshi, ni nini kinatangulia? Ni uhasibu wake au uanajeshi? Jeshi halifanyi recruitment ya wahasibu au madaktari bali linafanya recruitment ya askari. Kimsingi ajira yako siyo uhasibu bali ni uaskari. Ukiwa askari, sasa unaangaliwa mgawanyo wa kazi ndani ya jeshi ukiwa askari, mwingine anaenda kwenye mizinga, mwingine kwenye upilot, mwingine udaktari, mwingine uhasibu, mwingine kilimo, n.k. Lakini hawa wote ni askari. Wote wanaoongozwa na kanuni za jeshi. Kanuni za profession yako zinakuwa na nguvu Jeshini pale to zinapokuwa adopted na kutambulika kuwa ni kanuni za jeshi.

Mathalani, kwa kanuni za jumla za jeshi, a non doctor full Colonel angeweza na uwezo wa kumwambia Daktari mwenye cheo cha Major kuwa sitaki askari apewe ED zaidi ya siku 3. Lakini uwezo huo hana kwa sababu ipo kanuni ya Jeshi inayosema kuwa Uamuzi wa Daktari kuhusiana na masuala ya afya ni wa mwisho. Kwa hiyo kutokana na kanuni hiyo, hata Mkuu wa Kikosi hawezi kuupinga uamuzi wa daktari mwenye cheo cha chini kuliko chake.

Ili kanuni za Uhasibu ziweze kuheshimika ndani ya Jeshi ni lazima Kanuni hizo ziwe adopted na Jeshi na kuzifanya kuwa zake. La sivyo hakuna uwezekano wa kanuni za uhasibu kuprevail over kanuni za Jeshi. jeshi ni Taasisi ina sheria zake, utamaduni wake na kanuni zake ambazo haziwezi kuzidiwa nguvu na kanuni za profession mpaka pale kanuni za profession zinapotambulika na kufanywa kuwa ni sehemu ya kanuni zake.
 
Utetezi wa kipolitics...siamini kwamba kwa kuwa muhasibu raia basi akipewa amri ya kufanya malipo atambishia bosi wake...mi naamini katika ethics za taaluma yenyewe...haijalishi ni raia au polisi..mtu akifuata ethics hawez kufuata maelezo yanayo compromise taaluma yake...kwani tangu wawemo hao raia wamelisaidia jeshi la polisi kitu gani....si ndiyo hao hao waliofanya malipo hewa na manunuzi ya ajabu ambayo yametia hasara nchi.....
Jamani tuzitumie akili zetu vizuri..tuziziparalize kwa mambo ya siasa matope...
Hakuna Askari wa kukataa Amri ya Mkubwa wake,

Yaani Askari awe radhi kufukuzwa kazi Kisa anatetea taaluma..... Utamlisha wewe?
 
Ethics kutupwa nje au wewe ndo hutak kukubali ukweli? Huwez kuongelea kazi za kihasibu ukaacha ethics ndugu, na kama ingekua hvyo humu maofisini ingekua ni vurugu tu maana kila familia ya bosi ingekua inakupa amri, au mawaziri na makatibu wakuu wangekua wanafanya watakavyo si ni mabosi? Lakini mbona wakivunja sheria wanawajibishwa? No one is above the law hata uwe nani, ndo mana kuna sheria na taratibu, hakuna kitu kimafanyika bila sheria na utaratibu hata iweje ndo mana kila mtu na fani yake, mhasibi atakua mhasibu, mgavu atakua mgavi, na katik utumishi wa umma hakuna amri ya bila maandishi km hujui unless unajipa kesi bure, watu wanafanya kazi kwa mafaili sio mdomo,
Tatizo unachanganya na ku-generalize mambo! Hapa wanazungumziwa watu ambao tayari hawafuati hizo ethics na wapo vinginevyo hii mada isingekuwepo na hata hao ambao waliona umuhimu wa kuajiri raia wasingefanya hivyo! Na ndio maana tangu zamani nikakuambia hoja zako zimejikita katika ni namna gani mambo yalipaswa kuwa lakini sio jinsi yalivyo kwenye field!! Hizo bodi unazotaka usidhani zipo kwenye taaluma ya uhasibu peke yake... taaluma nyingi zina bodi zake na miiko yake ikielezea ni namna gani kazi zinatakiwa kufanywa lakini ukienda field unakuta mambo ni tofauti! Ugumu upo wapi hapa kuelewa?! Hata yule mchungaji na sheikh moja ya miiko yao ni kutozini... hivyo ndivyo ilipaswa kuwa lakini ukiingia kwenye real world, kinachofanyika ni kinyume chake! Hakuna aliyesema hawafuati maadili lakini hakuna, NARUDIA KWA HERUFI KUBWA, HAKUNA ANAYEACHA KUIBA ETI KWA KUOGOPA SIJUI BODI NA MAMBO KAMA HAYO; HAKUNA!
 
Lakini zinakutoa kamasi unashindwa kuzijibu unakimbilia defensive mechanism eti hoja za shule, yes hoja za shule koz nimeenda shule, zijibu,
Usilete vichekesho! Hoja yako ipi nimeshindwa kujibu wakati nimeshakuambia hoja zako zimekaa kiuanafunzi zaidi but they don't work in a real worl!!! Na kwa hoja yako hii kumbe nilikuwa sahihi kwamba wewe ni mwanafunzi na hujui what's going on in field ndo maana unafikia kuamini mtu ataacha kuiba eti kv atafutiwa uanachama!! Hushangai ilikuwaje nikakushitukia!!!! NITAJIE HIYO HOJA AMBAYO SIJAIJIBU!!!
 
Pia napata wasiwasi kuwa hata Baraza la Mawaziri halishirikishwi kwenye haya matamko na maamuzi.

Usipate wasiwasi mkuu, kwani hi serekali ni ya nani? Tangu kampeni si tuliambiwa itakuwa serekali ya JPM? Wateuliwa wake wote wanatakiwa kumsaidia atekeleza yale aliyoahidi na miongozo yake, period.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Huu msamiati wa "kijeshi" kwa polisi sijui maana yake nini? Halafu waandishi ni makanjanja sana! Habari inahusu polisi waovwanasema majeshi. Hivi wanajua wanachokiandika kweli?
Hata swala la kuondoa watumishi raia, lilikuwa ni agizo la rais kwa jeshi la polisi.sijui wanajeshi liliwahusu nini kujihusisha nalo.hapa kosa sio la waandishi ni la jeshi la ulinzi.
 
Back
Top Bottom