Massenberg
JF-Expert Member
- Jun 4, 2011
- 1,173
- 1,373
Kiongozi, usiwe kama huishi Tanzania au huifahamu nchi yetu; unataka kusema amri zote zinazotolewa huko majeshini huwa ni za halali tu? Kwenye nchi corrupted kama hii kinachoangaliwa ni cheo kwanza, uhalali wa amri tupa kule.
Mkuu BAK with due respect naona chanzo chako cha habari hakisemi ukweli wa jambo hili. Masuala yote ya kijeshi hata utoaji amri yanafuata utaratibu. Amri zitatolewa vipi, na nani na kwa namna gani vyote viko kwenye utaratibu huo na Amri zilizotajwa kwenye utaratibu ni zile zinaoitwa "AMRI HALALI" na siyo kila amri, hivyo ni upotoshaji kwamba eti afande anaweza akamwambia mhasibu ambaye ni mwanajeshi kwamba "Lipa malipo haya na akalipa" hiyo si kweli hata kidogo. Pia ni vizuri ukafahamu kuwa katika Jeshi kuna utaratibu mzuri tu uliyowekwa kwa mwanajeshi kuhoji amri ambayo anafikiri si halali.