Usidanganye, amri halali kwa sheria za kijeshi ni amri zile zinazoweza kutekezeka na wala haimaanishi usahihi wa jambo uliloamriwa.
Ukiambiwa sukuma nyumba ni amri halali japo kiusahihi huwezi kuisukuma nyumba. Lakini sukuma nyumba mpaka ianguke, hiyo siyo amri halali lakini itabidi uoneshe utii kwa kuisukuma japo unajua kuwa haitaanguka. Mhasibu mwanajeshi akiambiwa fanya malipo haya kwa huyu na haya mengine usifanye kwa sasa, hiyo itakuwa ni amri halali, hawezi kubisha hata kama aliyeamriwa alipwe pengine hakutimiza vigezo vya kulipwa.
Hili la kuwaondoa wahasibu raia jeshini likitekelezwa, kitakachowasaidia hao wahasibu ni kuomba maelekzo kutoka kwa makamanda kwa maandishi ili huko mbeleni wasiishie jela.