Ule ban kwa lipi la maana ulilosema zaidi tu ya kuthibitisha kumbe unaongozwa na ushabiki kwa JPM!!! Yaani wewe unaamini TIBA ni bora kuliko KINGA... maajabu sana haya!! Sasa mtu hata akitumbuliwa wakati ameshaiba mamilioni ya pesa kuna faida gani?! Sasa hilo la tiba ndilo lisilotakiwa na badala yake inahitajika kinga!!Asikudanganye mtu TIBA ipo ndugu yangu. kuna PAC etc ndo maana utaambiwa fulani katumbuliwa watu wanadhani ameonewa! Utakuta odita akija mhasibu anasema ukweli kwa kuonyesha maandishi kuwa nilimshauri akakataa. Tuache cheap politics za kumzonga JPM. Akikosea tumnange lakini akifanya kweli tumpongeze. Hivi unajua ugomvi wa JPM na ndugu zetu ni nini? Amewabana kimaslahi ndizo hizo chuki zote. Wakati wa JK walivuna kweli hasa akina .... (nakuomba niilishie hapo sitaki BAN mie)
Yaani we jamaa ama bado ni mwanafunzi wa accounting kwahiyo wala hufahamu kwamba huyo Auditor watu hawamuogopi na kama ni mfanyakazi basi una uelewa mdogo sana kwenye msuala ya fedha!!! Yaani naona hoja yako imejikita sana kwenye auditors wakija watagundua kwamba kuna magumashi yamefanyika... so what?!Nilichotaka kueleza ni kuwa fedha yote ikiingia katika taasisi inayopewa ruzuku na serikali ni ya serikali. PST ndiye mwenye hiyo pesa. Hivyo PST mwisho wa mwaka anatuma maodita kwenda koditi kila kitu na wahasibu na kama kuna mapungufu mhasibu mkuu anasukuma hiyo kasheshe kwa Accounting Officer ambaye anawajibishwa kisawasawa. Hivyo ni hoja mufilisi kufikiria kuwa Mhasibu akiwa ni Polisi ndiye anatapokea amri na kutekeleza (kwa vile ni Polisi). La hasha hata uraiani mhasibu akiambiwa lipa na mwajiri wake analipa ila odita akija kibao kinamgeukia huyo mwajiri. Nadhani umenipata
Umenifurahisha mkuu, hivi wewe ni Mungu kujua roho ya unayemuweka kama kiongozi? Kwa vile hatujui ya mbele katika maisha kinga si 100%. Kinga zipo za Vetting etc ila kama nilivyosema huwezi kujua kwa asilimia zote kama unayemwamini anaaminika. Hivyo TIBA ya mapema ni muhimu nayo ni kutumbuliwa kabla ya kumaliza kipindi chake. Heri nusu shari kuliko.... (malizia)Ule ban kwa lipi la maana ulilosema zaidi tu ya kuthibitisha kumbe unaongozwa na ushabiki kwa JPM!!! Yaani wewe unaamini TIBA ni bora kuliko KINGA... maajabu sana haya!! Sasa mtu hata akitumbuliwa wakati ameshaiba mamilioni ya pesa kuna faida gani?! Sasa hilo la tiba ndilo lisilotakiwa na badala yake inahitajika kinga!!
Naona umepinda kweli! Zamani mtu akikuuliza so wati unamjibu so dasti. Pole sana haya ninayoyaeleza yanakuzidi kimo naomba niishie hapaYaani we jamaa ama bado ni mwanafunzi wa accounting kwahiyo wala hufahamu kwamba huyo Auditor watu hawamuogopi na kama ni mfanyakazi basi una uelewa mdogo sana kwenye msuala ya fedha!!! Yaani naona hoja yako imejikita sana kwenye auditors wakija watagundua kwamba kuna magumashi yamefanyika... so what?!
Pentagon, Kuna Wafanyakazi Raia iwe Tz? Nyerere na Kisomo chote cha Ukweli, Mkapa na Uwezo wake Mkumbwa Kiutawala Tangu Nyerere Hakuliona! Mwishoni Utasikia Naaatangaza Kuiondoa Tanzania UN! Uingizaji wa Magari Nchini Mpaka Nitoe Kibari iri Mpande daradara Kupunguza Foreni za barabara! Hiri ra kupunguza Uingizaji Magari arinishauri Mwanangu Makondi, Baada ya Kiasi cha dora kupungua hazina, na Ra Kujitoa UN, Kanishauri kaka yangu Kagame, Nitakataaje Na Wake zetu Majina yao yanafanana, Hiri Nimeona nirichomeke. msg sent and derivadi, msemakweri ni mpezi wa ....
Nasikia Harufu ya ukurupukwajiAgizo la Magufuli laibua utata
Jamhuri September 15, 2016 Agizo la Magufuli laibua utata2016-09-15T09:59:21+00:00 Habari za Kitaifa
Agizo la Rais John Magufuli la kuwaondoa watumishi raia katika majeshi ya ulinzi na usalama, limeanza kutekelezwa, huku Wizara ya Utumishi wa Umma ikiendelea kupitia muundo.
Taarifa ambazo JAMHURI limezipata, zinasema kuwa tayari kazi hiyo imekamilika katika Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), huku Jeshi la Polisi likiwa tayari limeshafikisha orodha ya watumishi hao kwa mamlaka husika.
Akizungumza na JAMHURI, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi, Angela Kairuki, anasema tayari kazi hiyo imeshakamilishwa na Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, huku akikiri ofisi yake kupokea orodha ya wafanyakazi wengine kutoka kwa Inspekta Generali wa Polisi nchini, (IGP), Ernest Mangu.
“Tayari ofisi yangu imeshapokea majina kutoka ofisi ya IGP Mangu…lakini zoezi kama hilo limeshakamilika ndani ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Sasa tunaendelea kupitia muundo na kuangalia maeneo yenye mahitaji,” anasema Waziri Kairuki.
Waziri huyo anasema baada ya kupokea orodha hiyo, wameanza kufanya uchambuzi wa sifa za watumishi hao kabla ya kuanza kuwasambaza kwenye maeneo yeye mahitaji ndani ya idara na taasisi za Serikali, anasema orodha ya majina hayo ni zaidi ya watumishi 100.
“Tuliagizwa na Rais na sisi kazi yetu ni kutekeleza maagizo hayo…sasa tunachambua sifa za watumishi hao pamoja na kupitia muundo wa utumishi kabla ya kuwapangia maeneo mengine,” anasema Kairuki.
Akizungumza na JAMHURI, IGP Mangu anasema, hawezi kutoa taarifa zaidi za watumishi wasiokuwa askari ndani ya Jeshi la Polisi, badala yake akalitaka gazeti hili kuwasiliana na Wizara ya Utumishi.
“Kuhusu hao wafanyakazi raia ndani ya Jeshi la Polisi, naomba ziulizwe mamlaka za watumishi hao raia…tafadhali naomba muwatafuate watu wa Wizara ya Utumishi,” anasema IGP Mangu.
Julai, mwaka huu Rais Magufuli alipokuwa anawakamisheni Makamishna na Makamishna Wasaidizi wa Jeshi la Polisi, alitoa agizo la kuwaondoa watumishi raia katika majeshi.
Rais Magufuli alihoji sababu za kuwapo watumishi raia katika majeshi, ikiwa ni pamoja na Polisi na kuagiza watumishi watakaoajiriwa wawe ni askari, akilenga kupeleka nidhamu ya jeshi kwenye idara ya uhasibu.
“Hao watumishi ambao ni raia, muwapeleke Utumishi, kwani hakuna polisi ambao wamesomea uhasibu, uhandisi pamoja na masuala ya utawala? Matatizo ya wizi wizi pamoja na yale ya watumishi hewa, kama yanaletwa na raia, IGP kaorodheshe majina yao wote watoke,” alinukuliwa Rais Magufuli.
Baada ya kutoa agizo hilo, Jeshi la Polisi lilianza kuangalia njia za kutekeleza agizo hilo. Kada ya wahasibu ilionekana kulengwa zaidi kwani wao ni waajiriwa wa Hazina.
Habari kutoka ndani ya Jeshi hilo zinasema baada ya tafakuri, iliamuriwa wahasibu wote ambao ni raia wapelekewe kwenye mafunzo katika Chuo cha Polisi Moshi.
Wahusika wote walipewa taarifa wakitakiwa wajiandae kwenda kwenye mafunzo ya kijeshi. Hata hivyo, wakati hayo yakiendelea, viongozi waandamizi wa polisi walipitia miongozo mbalimbali na kubaini kuwa na wahasibu ambao ni askari kungeleta mtanziko mkubwa kwenye kazi za kihasibu.
Kwa mujibu wa mtoa taarifa wetu, kuajiriwa kwa wahasibu raia kulilenga kuwawezesha ‘kuwabishia’ viongozi wa polisi ambao wangeonekana kutumia zaidi amri badala ya kanuni na miongozo ya fedha.
“Mwongozo wa kwanza kabisa kwa askari ni utii, ukiwa na mhasibu askari, kama koplo, hawezi kukataa au kuhoji amri ya mkuu wake inayomtaka atoe fedha.
“Mhasibu askari anapokaidi maagizo au amri anaadhibiwa kijeshi, lakini kwa raia hiyo haiwezekani,” kimesema
Chanzo chetu.
Inaelezwa kuwa uamuzi wa kuwafanya wahasibu wawe waajiriwa Hazina ulifikiwa tangu uongozi wa awamu ya kwanza kwa lengo la kuleta nidhamu za kihasibu kwenye matumizi ya fedha.
“Wakubwa wetu (viongozi wa polisi) hili jambo linawasumbua sana, hawajui wamweleze nini mheshimiwa, lakini ukweli ndiyo huo kwamba wanaona uzito kuwa na wahasibu ambao ni askari.
“Wakati fulani uamuzi kama huu ulijaribiwa kwenye vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama na kwa kweli kulitokea matatizo makubwa sana kwenye matumizi ya fedha, ikaamuriwa utaratibu wa kuwatumia wahasibu ambao ni raia, uendelee,” kimesema chanzo chetu na kuongeza:
“Kwa uelewa wangu mdogo nadhani kuwekwa watumishi raia kwenye majeshi ilikuwa ni kuwadhibiti hawa wanaojiita afande hususani katika amri zao.
“Mfano RPC anamfuata mhasibu na kumwambia lipa haya malipo, na kanuni ya Jeshi ni tekeleza kwanza ndiyo uhoji baadaye.
“Watumishi raia walikuwa na nafasi ya kuhoji anachoona hakielewi, askari huwa hawana.”
Mpwa ulipigwa ban nyengne...!?sichangii niko na maumivu ya GEREZANI.
swissme
Umri wako unakuruhusu kuandika uliyoyaandikaMkuu BAK with due respect naona chanzo chako cha habari hakisemi ukweli wa jambo hili. Masuala yote ya kijeshi hata utoaji amri yanafuata utaratibu. Amri zitatolewa vipi, na nani na kwa namna gani vyote viko kwenye utaratibu huo na Amri zilizotajwa kwenye utaratibu ni zile zinaoitwa "AMRI HALALI" na siyo kila amri, hivyo ni upotoshaji kwamba eti afande anaweza akamwambia mhasibu ambaye ni mwanajeshi kwamba "Lipa malipo haya na akalipa" hiyo si kweli hata kidogo. Pia ni vizuri ukafahamu kuwa katika Jeshi kuna utaratibu mzuri tu uliyowekwa kwa mwanajeshi kuhoji amri ambayo anafikiri si halali.
Huo ni uongo uliopitiliza...muhasibu yeyote akishajua dili inaela atatoa tu hayo malipo...tunawaona huku kwenye maofisi..suala hapa siyo ujeshi au uraia ndugu yangu...ni uwezo wa mtu kuzingatia ethics za kaz yake...Oh! Kwahiyo kumbe haina haja ya kuweka kinga kwavile tiba ipo!!!!
Hilo la Tanzania kujiondoa UN....kama naliona vile!!Pentagon, Kuna Wafanyakazi Raia iwe Tz? Nyerere na Kisomo chote cha Ukweli, Mkapa na Uwezo wake Mkumbwa Kiutawala Tangu Nyerere Hakuliona! Mwishoni Utasikia Naaatangaza Kuiondoa Tanzania UN! Uingizaji wa Magari Nchini Mpaka Nitoe Kibari iri Mpande daradara Kupunguza Foreni za barabara! Hiri ra kupunguza Uingizaji Magari arinishauri Mwanangu Makondi, Baada ya Kiasi cha dora kupungua hazina, na Ra Kujitoa UN, Kanishauri kaka yangu Kagame, Nitakataaje Na Wake zetu Majina yao yanafanana, Hiri Nimeona nirichomeke. msg sent and derivadi, msemakweri ni mpezi wa ....
Weee kwa mwendo huu Iri wafuzu waritakiwa wawe na mafunzo ya miaka isiyopungua kumi na miwiri, na wajue ku-butcher KilengerezaSiwangewapeleka kozi miezi sita ya upolisi .wanarudi kupiga kazi
Usiishie kusoma title ya thesis, soma problem statement, justification, general objective, specific objectives, research questions /hypothesis, literature review , methodology na kadhalika .ukibahatika kupitia chapisho hilo katika ngazi hizo utaweza kuja na tathimini sahihi ya ulazima wa kuwepo chapisho hilo. Vinginevyo msimamo wako wa sasa ni ishara kuwa na "mtimanyongo" kwa muandaa chapisho, na usipokuwa makini "utakondeana kwa stress"Habari ya PHD za kununua!, "Mafuta ya Korosho yanazuia Kutu!" The hell, mafuta yoyote yanazuia Kutu! why should it be a news?