Agizo la Magufuli laibua utata

Agizo la Magufuli laibua utata

Hili lilishajadiliwa kwa kina sana umuhimu wa RAIA ndani ya majeshi na kumbuka wengine sio tu RAIA kisa amevaa kiraia ila wengine ni RAIA wa kijeshi na ngumu kumtambua kwa jinsi walivyopikwa na kuiva ktk mafunzo.

Athari za kuwaondoa raia jeshini zitakuja kuonekana mbele ya safari

Ushauri,tuangalia upya namna ya kutekeleza agizo la Mh Rais ili huo mpango mpya usilete madhara.
Umuhimu wa raia ni upi na hizo effects ni zipi? Kwani mwanajeshi alosomea uhasibu na raia alosomea uhasibu tofauti yao ni nini? Kanuni sheria wanazofanyia kazi ni tofauti? Au wanajeshi wana bodi yao ya uhasibu na raia wana bodi ya uhasibu inayoshughulikia ethics? Acheni siasa katika ukweli
 
Hivi jeshi linatumia standing order au halitumii? Ni sehemu gani ambayo inamruhusu kiongozi wa kijeshi kutumia vibaya madaraka yake eti kwa sbb haojiwi? Utumishi wa umma gani unatoa amri kwa mdomo? Acheni kupotosha mambo, awe mwanajeshi awe nani hakuna ambaye yuko juu ya sheria, kama sheria inakataza kula rushwa maana ake inaaply kote kote,
Hahaha zipo linatumia tena kali kushinda za uraiani, kuhusu kutoa amri zipo za maandishi unazozijua na za mdomo ipi itumike situation will tell
 
Amri yoyote ya ya mkuu ni AMRI HALALI kwa wakati huo! Ndiyo maana polisi wanapoambiwa wamiminie waandamanaji risasi huwa hawana ruhusa ya kuhoji,japo wanajua kuwa katiba inakuhusu maandamano ya Amani! Pia mkuu wa mkoa si askari kicheo,bali ni askari wa ngazi ya juu kabisa kisiasa!! Ndiyo maana ana uwezzo wa kumwamrisha Rpc kufanya chochote! Hata kumweka ndani mtu bila sababu yoyote!
Hakuna sheria inamruhusu kumueka ndani mtu bila makosa, no one is above the law,
 
Agizo la Magufuli laibua utata

Jamhuri September 15, 2016 Agizo la Magufuli laibua utata2016-09-15T09:59:21+00:00 Habari za Kitaifa

Agizo la Rais John Magufuli la kuwaondoa watumishi raia katika majeshi ya ulinzi na usalama, limeanza kutekelezwa, huku Wizara ya Utumishi wa Umma ikiendelea kupitia muundo.

Taarifa ambazo JAMHURI limezipata, zinasema kuwa tayari kazi hiyo imekamilika katika Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), huku Jeshi la Polisi likiwa tayari limeshafikisha orodha ya watumishi hao kwa mamlaka husika.

Akizungumza na JAMHURI, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi, Angela Kairuki, anasema tayari kazi hiyo imeshakamilishwa na Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, huku akikiri ofisi yake kupokea orodha ya wafanyakazi wengine kutoka kwa Inspekta Generali wa Polisi nchini, (IGP), Ernest Mangu.

“Tayari ofisi yangu imeshapokea majina kutoka ofisi ya IGP Mangu…lakini zoezi kama hilo limeshakamilika ndani ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Sasa tunaendelea kupitia muundo na kuangalia maeneo yenye mahitaji,” anasema Waziri Kairuki.

Waziri huyo anasema baada ya kupokea orodha hiyo, wameanza kufanya uchambuzi wa sifa za watumishi hao kabla ya kuanza kuwasambaza kwenye maeneo yeye mahitaji ndani ya idara na taasisi za Serikali, anasema orodha ya majina hayo ni zaidi ya watumishi 100.

“Tuliagizwa na Rais na sisi kazi yetu ni kutekeleza maagizo hayo…sasa tunachambua sifa za watumishi hao pamoja na kupitia muundo wa utumishi kabla ya kuwapangia maeneo mengine,” anasema Kairuki.

Akizungumza na JAMHURI, IGP Mangu anasema, hawezi kutoa taarifa zaidi za watumishi wasiokuwa askari ndani ya Jeshi la Polisi, badala yake akalitaka gazeti hili kuwasiliana na Wizara ya Utumishi.

“Kuhusu hao wafanyakazi raia ndani ya Jeshi la Polisi, naomba ziulizwe mamlaka za watumishi hao raia…tafadhali naomba muwatafuate watu wa Wizara ya Utumishi,” anasema IGP Mangu.

Julai, mwaka huu Rais Magufuli alipokuwa anawakamisheni Makamishna na Makamishna Wasaidizi wa Jeshi la Polisi, alitoa agizo la kuwaondoa watumishi raia katika majeshi.

Rais Magufuli alihoji sababu za kuwapo watumishi raia katika majeshi, ikiwa ni pamoja na Polisi na kuagiza watumishi watakaoajiriwa wawe ni askari, akilenga kupeleka nidhamu ya jeshi kwenye idara ya uhasibu.

“Hao watumishi ambao ni raia, muwapeleke Utumishi, kwani hakuna polisi ambao wamesomea uhasibu, uhandisi pamoja na masuala ya utawala? Matatizo ya wizi wizi pamoja na yale ya watumishi hewa, kama yanaletwa na raia, IGP kaorodheshe majina yao wote watoke,” alinukuliwa Rais Magufuli.

Baada ya kutoa agizo hilo, Jeshi la Polisi lilianza kuangalia njia za kutekeleza agizo hilo. Kada ya wahasibu ilionekana kulengwa zaidi kwani wao ni waajiriwa wa Hazina.

Habari kutoka ndani ya Jeshi hilo zinasema baada ya tafakuri, iliamuriwa wahasibu wote ambao ni raia wapelekewe kwenye mafunzo katika Chuo cha Polisi Moshi.

Wahusika wote walipewa taarifa wakitakiwa wajiandae kwenda kwenye mafunzo ya kijeshi. Hata hivyo, wakati hayo yakiendelea, viongozi waandamizi wa polisi walipitia miongozo mbalimbali na kubaini kuwa na wahasibu ambao ni askari kungeleta mtanziko mkubwa kwenye kazi za kihasibu.

Kwa mujibu wa mtoa taarifa wetu, kuajiriwa kwa wahasibu raia kulilenga kuwawezesha ‘kuwabishia’ viongozi wa polisi ambao wangeonekana kutumia zaidi amri badala ya kanuni na miongozo ya fedha.

“Mwongozo wa kwanza kabisa kwa askari ni utii, ukiwa na mhasibu askari, kama koplo, hawezi kukataa au kuhoji amri ya mkuu wake inayomtaka atoe fedha.

“Mhasibu askari anapokaidi maagizo au amri anaadhibiwa kijeshi, lakini kwa raia hiyo haiwezekani,” kimesema

Chanzo chetu.

Inaelezwa kuwa uamuzi wa kuwafanya wahasibu wawe waajiriwa Hazina ulifikiwa tangu uongozi wa awamu ya kwanza kwa lengo la kuleta nidhamu za kihasibu kwenye matumizi ya fedha.

“Wakubwa wetu (viongozi wa polisi) hili jambo linawasumbua sana, hawajui wamweleze nini mheshimiwa, lakini ukweli ndiyo huo kwamba wanaona uzito kuwa na wahasibu ambao ni askari.

“Wakati fulani uamuzi kama huu ulijaribiwa kwenye vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama na kwa kweli kulitokea matatizo makubwa sana kwenye matumizi ya fedha, ikaamuriwa utaratibu wa kuwatumia wahasibu ambao ni raia, uendelee,” kimesema chanzo chetu na kuongeza:

“Kwa uelewa wangu mdogo nadhani kuwekwa watumishi raia kwenye majeshi ilikuwa ni kuwadhibiti hawa wanaojiita afande hususani katika amri zao.

“Mfano RPC anamfuata mhasibu na kumwambia lipa haya malipo, na kanuni ya Jeshi ni tekeleza kwanza ndiyo uhoji baadaye.

“Watumishi raia walikuwa na nafasi ya kuhoji anachoona hakielewi, askari huwa hawana.”


Kwa sasa hata raia wakikataa amri ya afande wataitwa wachochezi na kufunguliwa mashitaka!
 
Hahaha zipo linatumia tena kali kushinda za uraiani, kuhusu kutoa amri zipo za maandishi unazozijua na za mdomo ipi itumike situation will tell
Amri za mdomo lakini wakiwa katika maandamano au mapigano, lakini si katika mambo kama uhasibu au ya kiofisi,
 
Unayosema ni kweli kwamba ingawaje kiutaratibu jeshi linaendeshwa kiamri na aliye chini hawezi kuhoji amri kutoka juu lakini hapa tuwe wakweli pia! Hivyo ulivyosema NDIVYO INATAKIWA KUWA! Hata kama mimi ni Koplo, wewe Major hauna mamlaka ya kijeshi ya kuniamrisha NIKAKULETEE DEMU wako... ukifanya hivyo; maadili ya kijeshi yananipa nguvu ya kukukatalia! Hivyo ndivyo INAVYOTAKIWA! But when we go to the real world... I mean to the real military world, hali ni tofauti! Ni askari wachache sana tena sana wenye ubavu wa kuhoji amri zisizo halali... ni almost HAKUNA! Ni ngumu sana kwa junior officer kuhoji amri isiyo halali ya Brigerdia ingawaje anayo haki hiyo! Ikiwa hata huku uraian watu wanaingia matatizoni kv tu walitii tena shingo upande amri za mabosi raia wenzao, seuze majeshini?!

Lakini tukirudi kwenye mada kuu; Mhasibu Raia ana uwezo wa kutotii amri ya Mheshimiwa mwenye manyota si tu kwa sababu hawajibiki kwenye military chain of command lakini vile vile yeye si mwajiriwa ama wa jeshi au wizara husika ya ulinzi. Hii ndiyo sababu ambayo pia miaka takriban 8 iliyopita wakati serikali inaajiri Internal Auditors; ikaonekana hawa wasiwe waajiri wa halmashauri moja kwa moja bali wa Hazina.
Nataka kujua tofauti ya mhasibu raia na mhasibu mwanajeshi, kwamba wanajeshi wana bodi yao ya uhasibu inatumia sheria zao tofauti na NBAA ama? Kwamba ethics zao ni tofauti?
 
Usidanganye, amri halali kwa sheria za kijeshi ni amri zile zinazoweza kutekezeka na wala haimaanishi usahihi wa jambo uliloamriwa.

Ukiambiwa sukuma nyumba ni amri halali japo kiusahihi huwezi kuisukuma nyumba. Lakini sukuma nyumba mpaka ianguke, hiyo siyo amri halali lakini itabidi uoneshe utii kwa kuisukuma japo unajua kuwa haitaanguka. Mhasibu mwanajeshi akiambiwa fanya malipo haya kwa huyu na haya mengine usifanye kwa sasa, hiyo itakuwa ni amri halali, hawezi kubisha hata kama aliyeamriwa alipwe pengine hakutimiza vigezo vya kulipwa.

Hili la kuwaondoa wahasibu raia jeshini likitekelezwa, kitakachowasaidia hao wahasibu ni kuomba maelekzo kutoka kwa makamanda kwa maandishi ili huko mbeleni wasiishie jela.

Mkuu BAK with due respect naona chanzo chako cha habari hakisemi ukweli wa jambo hili. Masuala yote ya kijeshi hata utoaji amri yanafuata utaratibu. Amri zitatolewa vipi, na nani na kwa namna gani vyote viko kwenye utaratibu huo na Amri zilizotajwa kwenye utaratibu ni zile zinaoitwa "AMRI HALALI" na siyo kila amri, hivyo ni upotoshaji kwamba eti afande anaweza akamwambia mhasibu ambaye ni mwanajeshi kwamba "Lipa malipo haya na akalipa" hiyo si kweli hata kidogo. Pia ni vizuri ukafahamu kuwa katika Jeshi kuna utaratibu mzuri tu uliyowekwa kwa mwanajeshi kuhoji amri ambayo anafikiri si halali.
 
Nataka kujua tofauti ya mhasibu raia na mhasibu mwanajeshi, kwamba wanajeshi wana bodi yao ya uhasibu inatumia sheria zao tofauti na NBAA ama? Kwamba ethics zao ni tofauti?

Tofauti kubwa ni kuwa mhasibu mwanajeshi, kazi yake namba moja ni 'uanajeshi', uhasibu ni ziada. Kwa hiyo kimsingi, cha kwanza anatakiwa kutii sheria za kijeshi kabla ya taratibu za uhasibu. Kwa hiyo mhasibu mwanajeshi anaongozwa na ethics za kijeshi, mhasibu raia anaongozwa na ethics za kihasibu.

Ni sawa na kule Kanisa Katoliki, unaweza kuwa na mtawa mhasibu. Mtawa mhasibu, cha kwanza kinachotazamwa ni utawa wake na siyo uhasibu. Kwanza itabidi afuate kanuni za utawa, uhasibu baadaye. Na askofu anaweza kumwondoa mtawa mhasibu kwenye uhasibu bila kuhojiwa maana aliingia kwenye kanisa kwaajili ya utawa na siyo uhasibu.
 
Nataka kujua tofauti ya mhasibu raia na mhasibu mwanajeshi, kwamba wanajeshi wana bodi yao ya uhasibu inatumia sheria zao tofauti na NBAA ama? Kwamba ethics zao ni tofauti?
Are you seriously talking of ethics?! Anyway, kukujibu swali lako, professionally there's no different!! Naamini ulitaka kujenga hoja... am waiting!
 
Management Control systems...wamefanya makusudi kutoweka mfumo wa kumfanya DED amuajiri Internal Auditor...maana ataishia kuwa mtiifu kwa DED na kuficha madudu, maana ndio mwajiri wake,
...system kama hiyo inasaidia kupunguza ubadhilifu kama aliyewaweka (serikali na CAG) ana nia ya dhati ya kuwatumia...na kuwaadhibu wakiachia madudu yatendeke bila kutoa taharifa

Wewe ni mgumu wa kuelewa!! Nilichokuambia ni kwamba, wapo wengi tu wanaotii amri kwa ajili tu ya kumuogopa mwajiri wake lakini si kwa sababu anapata mgao au ameiba yeye mwenyewe! Kila mtu ana sababu yake. Sasa basi, miongoni mwa hizo sababu, mtu hana sababu ya kumuogopa huyu mwajiri wa kuazima kv sio mwajiri wake! Kwahiyo atamuogopa labda kwa sababu tu hajiamini na si vinginevyo... au labda kv amepata mgao wake! Ndio maana nikatoa hata mfano wa Internal Auditors. Internal Auditor hana sababu ya kuogopa kumtumbua DED wake kv sio mwajiri wake hata kama anatumia majengo yake! Akishindwa kumtumbua basi itakuwa ni kwa kutojiamini tu! Tofauti kama ingekuwa huyo DED ndo kakuajiri.

But all in all, hakuna nilipozungumzia suala la ufanisi! Ufanisi ni kitu kingine kabisa!
 
Ha
Umuhimu wa raia ni upi na hizo effects ni zipi? Kwani mwanajeshi alosomea uhasibu na raia alosomea uhasibu tofauti yao ni nini? Kanuni sheria wanazofanyia kazi ni tofauti? Au wanajeshi wana bodi yao ya uhasibu na raia wana bodi ya uhasibu inayoshughulikia ethics? Acheni siasa katika ukweli
Hapo hakuna siasa ni taratibu zilizowekwa kwa umakini wa hali ya juu sana.

Hayo yote uliyocomment yaliangaliwa ila juwa kuwa kuna sababu za msingi kwa RAIA kufanya kazi Jeshini si Tanzania tu Hata huko nje iko hiyo.
 
Duuuuh aiseee shida iliyopo ni kubwa sana.
Lakini bado najiuliza, nani atamfunga paka yule kengele?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Management Control systems...wamefanya makusudi kutoweka mfumo wa kumfanya DED amuajiri Internal Auditor...maana ataishia kuwa mtiifu kwa DED na kuficha madudu, maana ndio mwajiri wake,
...system kama hiyo inasaidia kupunguza ubadhilifu kama aliyewaweka (serikali na CAG) ana nia ya dhati ya kuwatumia...na kuwaadhibu wakiachia madudu yatendeke bila kutoa taharifa
That's right na hicho ndicho hasa nilikuwa namwambia!
 
sichangii niko na maumivu ya GEREZANI.

swissme

Duh!Pole,ulipata matibabu ya kuvunjwa huo Mkono?Tumekumiss sana.Usiogope tumia tu lugha nyepesi lakini hakikisha inapenya kisawasawa
 
Back
Top Bottom