ndugu yangu acha ushabiki kwa sababu aliyesema ni tundu lissu wa chadema, na ni vyema mkachanbua na kutathimini ipasavyo alichosema tundu lissu.kama mtu kasikiliza hotuba hiyo, ,hawezi kusema kwa kutamka kama ulivyosema wewe.Hoja aliyosema tundu lissu ina mantiki na wala wakuwadharau majaji, wewe unayesema hivyo ndo unawakumbatia udhaifu wao.majaji si miungu ni binadamu kama wengine.Mhimili huu una maadili yake na uteuzi wake una vigezo muhimu, lakini kwa sasa kumeibuka maswali kwenye uteuzi huo, na kuhoji kama kweli vigezo vilizingatiwa.Kigezo ni weledi, uzoefu, uadilifu na umri.Kuna baadhi ya majaji weledi wao kwenye hukumu zao umekuwa na mawaswali mengi.na kuhoji kama vigezo vilizingatiwa.Pia inatia shaka kama ni kwanni rais ateue jaji ambaye umri wake wa kustaafu umefika, hapa swali la umri linakuwa halikuzigatiwa.maswali yanakuwa kuwa," anapewa fadhila ya kupata marupurupu ya kustaafu bila kuwa na muda aliofanya kazi uanotosha ipasavyo.na je kwenye uteuzi huo hakukuwa na wanazuoni wakisheria wenye umri mzuri wakuteuliwa ili kupewa nyazifa hizo?Juzi kuna mdada alikuwa na fanya kazi kwenye law firm ya riz ameteuliwa kuwa jaji,watu wengi walikuwa na maswali mengi kuhusu hilo.Kwahiyo tundu lisu kama mbunge na pale kulikuwa mahala pa kupitisha bajeti hiyo ya utendaji huo, hakuwa na kosa kuhoji hayo.Sisi watanzania tunakosea sana kukaa kimya kutohoji masuala yanayokera wananchi kama hayo, na pia wanaofichua kero hizo husakamwa wasifanye kwa giriba na hila kama hizo.Hoja ni vyema muhimili wa mahakama uwe na uadilifu kama mihimili mingine.Na kero zilizopo kutozihoji kwa kuwa ni majaji watadharauliwa ni kuficha uozo ambao rais anaufanya na kwa mamlaka aliyopewa kusimamia.Asante kwa hojaTuache ushabiki wa kivyama kwenye masilahi umma, mahakama ni muhimili muhimu sana.
Soma na hili kituko cha Werema;
Alipoulizwa kuhusu utekelezaji wa hatua hiyo jana, Mkuu wa Serikali Jaji Fredrick Werema alisema kuwa siyo lazima kwa Watanzania kufahamu hilo."Nilipozungumza jana (juzi) sikuzungumza na Watanzania bali nilizungumza na Bunge, hivyo siyo lazima Watanzania kufahamu jambo hilo na wala sioni sababu za kwa nini liandikwe magazetini,'' alisema Jaji Werema.
source Mwananchi .
Lissu sasa matatani ; Sunday, 15 July 2012 10:28 a friend
Alafu watu wengine wanaleta maoni ya kubwabwaja na kumuunga mkono mtu kama huyu na kumsifia eti msomi!
Kwa kauli kama hii anafaa kuwajibishwa maana anasahau kuwa aliyemteua ameajiriwa na watanzania na kwamba Mh.Lissu na Bunge ndiyo watanzania wenyewe wawapo Bungeni.Ila labda kauli na Mbiu ya kuwa Raisi ni Dhaifu ndiyo inayompa Jeuri.