PatriotMzalendo
Member
- Jan 17, 2011
- 28
- 6
Lissu ni mtaalam wa sheria za mazingira, na si mtaalam wa sheria za katiba, upo hapo ? kwa minajili hiyo basi utajua Lissu ni limbukeni wa sheria, na ni mpayukaji tu, kwa nyie mnaopenda hata mmeisha ingia upofu
Kwenye taaluma ya sheria hakuna mtu ambaye ni mtaalam wa eneo moja tu. Kunaweza kuwepo mgawanyiko tu wa masuala ya kisheria ya kushughulikia. Sheria ya Katiba ni somo la wanasheria wote kama ilivyo kwa sheria ya jinai, sheria ya ushahidi, sheria ya utawala, sheria ya dhara (tort) na nyingine. Hakuna sheria ya mazingira kama somo bali ukishakuwa mwanesheria (shahada moja kwenda juu) unakuwa na tools of analysis, skills of statutory interpretation na jurisprudence ambavyo kwavyo unaweza kushughulika na sheria yoyote, ikiwemo hiyo ya mazingira, ya SUMATRA, ya Dawasco na yoyote ile very effectively na ndiyo maana hakuna wakili anayeshindwa kusimamia kesi inayohusu sheria yoyote ile.
Tunaweza kujadili mambo kwa ushabiki na kwa jazba lakini ni vizuri tuepuke kupotosha yale ambayo hatuyajui.