AG amemdhalilisha Halima Mdee bungeni

AG amemdhalilisha Halima Mdee bungeni

Verified

Senior Member
Joined
Apr 11, 2013
Posts
117
Reaction score
380
Ni jambo la aibu kwa Mwanasheria Mkuu wa serikali kutumia muda wa takriban dakika tatu kuelezea tofauti kati ya woman, Lady na Gentleman na kusema kwamba anashindwa kujua kama Halima Mdee ni Lady au Gentleman.

Kwa kweli kuangalia Bunge ni kichefuchefu tupu na hizi Ndioooooooooooo zao!!

MWANASHERIA Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema, ameshindwa kutambua jinsia ya Mbunge wa Kawe kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Halima Mdee, kutokana na kuingilia mazungumzo yake.

Sintofahamu hiyo iliibuka juzi jioni, bungeni Dodoma, wakati wa kikao cha mjadala wa bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria, ambapo Mdee alichangia kwamba Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), isipobadilisha mfumo uliowezesha kupatikana mabaraza ya Katiba watakwenda kuwashitaki kwa wananchi.

"Mheshimiwa Mwenyekiti, hili jambo msiliweke kichama, hebu tuangalia maslahi ya taifa, kama ninyi hamtaki kubadilisha huu mfumo tukigawana hapa sisi tutoke twende kwa wananchi na kuwaeleza hoja hii hapatatosha," alisema Mdee.

Akifafanua hoja hiyo ambayo iliibuliwa pia na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, ilimfanya AG kutoa ufafanuzi ambapo wakati anaendelea kuzungumza sauti ya Mdee ilisikika.

Kitendo cha Mdee kuzungumza wakati AG akiendelea kutolea ufafanuzi hoja ya mabaraza ya katiba, kilimfanya ahoji jinsia ya Mbunge huyo, kutokana na baadhi ya makabila mengi nchini wanawake huheshimu pale mwanaume anapoongea.

"Unajua kule kwetu mwanaume akisimama na kuzungumza wanaume wanasikiliza, kinamama au wasichana wanafunga midomo..lakini sasa mimi ninapozungumza ndugu yangu Mdee unafunua mdomo sijui nikuweke kwenye kundi gani la ‘Lady au Gentlemen," alisema AG Werema.

Kauli hiyo iliibua vicheko miongoni mwa wabunge, huku Mdee mwenyewe akiangua kicheko sambamba na kuzunguka kwenye kiti alichokikalia.
 
Akizidisha fujo amshtaki kwa Basha wake Ahmed Shabiby mbunge wa Gairo CCM amchape the dudu Kinyamkera Chake kipoe!
 
Huyu jamaa kichwa boksi kinoma yaani. Mi hata simuelewi mkurya gani kilaza kama huyu
 
Mwongozo wa spika!waziri afute kauli ndani ya siku saba
 
mwanamke moja mwanachadema ni sawa na akili 20 za wavulana waccm, na anashindwa kumtofautisha na mwanaume kwani hoja anazozitoa ni zaidi ya wavulana wa ccm bungeni
 
ha ha ha yani huyu jamaa ni mkurya mwenzangu rakini uwezo wake ni finyu sana...mura weito pore sana sasa cha kufanya kwa sababu unapingana na mchakato wa kupata katiba mpya basi itabidi urudi tarime kwenu kwa sbabu najua ungejitahidi sana tupate katiba mpya ingesaidia hata watoto wetu pare tarime wasitairiwe ha ha ha ha ha ha broken toking werema mura wa bhairighe or bharenchoka
 
Kutoka bungeni AG anasema kutokana na kukosa ustaarabu wa Halima Mdee anashindwa kumtofautisha na mwanamume.

That was another disgrace statement toka kwa mtu kama yeye .Typical CCM na Spika kimya hajaomba kufutwa kitu na iko kwenye hansard .Ila watanzania they are watching Elimu kubwa katoa Lissu hakika na kesho utaona matokeo yake .You just sit and wait
 
AG Werema ni mwanasheria mkuu bogus kuliko wote niliopata kuwashuhudia. Kiukweli ndugu yangu werema hata katika tasnia ya sheria ni mwepesi sana.

Niliwahi kuwa nae katika bodi ya uongozi ya taasisi moja ya elimu ya juu akiiwakilisha wizara ya mambo ya sheria na katiba ndipo nilimfahamu vizuri, kwamba yuko shalow sana.

Kuwapiga vijembe wabunge wa Chadema badala ya kutoa muongozo na ufafanuzi wa kisheria ni dalili ya wazi kuwa majukumu aliyokabidhiwa ni makubwa kuliko uwezo wake.
 
Ag unatutia aibu wakurya wenzako tutaona aibu kujivunia ukurya wetu kwa akili zako na mchama wako magamba
 
Wakati akichangia hoja ya sheria na katiba bungeni huku baadhi ya wabunge wakinongona,mwanasheria mkuu amemumshambulia kwa maneno makali mbunge wa Kawe Halima Mdee,amwambia hajui amweke ktk kundi la lady or gentle man.Maneno haya angeambiwa upande wao ingezua balaa na miongozo ingekua mingi bungen,hata ivo mwanasheria aliposkia muongozo aligomea kumskiliza aliyeomba muongozo kwa kusema hakuna cha muongozo hapa huku speaker akishabikia yote yaliyokua yakitokea wakati mkuu huyo anachangia!!!!!Je siku akinyanyuka Halima mdee akatoa maneno kama hayo bungeni kwa mwanasheria mkuu au waziri mtamvumilia km yeye alivyowavumilia!!!
 
Nawaza kwa sauti "Ingekuwaje
Tundu Lissu angehoji kama Ester
Bulayo (MB-CCM) ni lady au
gentleman." maana AG ilikuwa poa
tu
 
MWANASHERIA Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema, ameshindwa kutambua jinsia ya Mbunge wa Kawe kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Halima Mdee, kutokana na kuingilia mazungumzo yake.

Sintofahamu hiyo iliibuka juzi jioni, bungeni Dodoma, wakati wa kikao cha mjadala wa bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria, ambapo Mdee alichangia kwamba Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), isipobadilisha mfumo uliowezesha kupatikana mabaraza ya Katiba watakwenda kuwashitaki kwa wananchi.

“Mheshimiwa Mwenyekiti, hili jambo msiliweke kichama, hebu tuangalia maslahi ya taifa, kama ninyi hamtaki kubadilisha huu mfumo tukigawana hapa sisi tutoke twende kwa wananchi na kuwaeleza hoja hii hapatatosha,” alisema Mdee.

Akifafanua hoja hiyo ambayo iliibuliwa pia na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, ilimfanya AG kutoa ufafanuzi ambapo wakati anaendelea kuzungumza sauti ya Mdee ilisikika.

Kitendo cha Mdee kuzungumza wakati AG akiendelea kutolea ufafanuzi hoja ya mabaraza ya katiba, kilimfanya ahoji jinsia ya Mbunge huyo, kutokana na baadhi ya makabila mengi nchini wanawake huheshimu pale mwanaume anapoongea.

“Unajua kule kwetu mwanaume akisimama na kuzungumza wanaume wanasikiliza, kinamama au wasichana wanafunga midomo..lakini sasa mimi ninapozungumza ndugu yangu Mdee unafunua mdomo sijui nikuweke kwenye kundi gani la ‘Lady au Gentlemen,” alisema AG Werema.

Kauli hiyo iliibua vicheko miongoni mwa wabunge, huku Mdee mwenyewe akiangua kicheko sambamba na kuzunguka kwenye kiti alichokikalia.
 
Jaji werema kamdhalilisha Mbunge wa kawe Mh Halima Mdee pia na wapiga kura wa kawe!

Amuombe radhi mdee na wapiga kura wake! Sitaki kuamini werema ni jaji uchwara anayetumia "masaburi" kufikiria.
 
Udhalilishaji wa KIJINSIA sio lazima hadi MTU apigwe, KWA kweli amedhalilisha wanawake wote wakiwemo na mabinti zake
 
Jamaniiii ni utani tuu

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom