Afukuza mke na kichanga usiku wa manane | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Afukuza mke na kichanga usiku wa manane

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Nov 13, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Nov 13, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  MWANAUME mmoja ambaye jina lake linaendelea kuhifadhiwa, ameonyesha kitendo cha ukatili cha kumfukuza usiku wa manane mkewe akiwa na kichanga baada ya kumkuta na boksi la mipira ya kiume Mwanaume huyo dereva wa shule moja maarufu jijini alimfukuza mkewe baada ya kupata hasira ya kumkuta na boksi la mipira kwa kudhani anaitumia katika ufuska na wanaume wengine bila kujua

  Imedaiwa na mwanamke huyo kuwa, siku tatu nyuma alikwenda kliniki kwa ajili ya kujiunga na njia za uzazi wa mpango na kudai aliogopa kutumia njia nyingine zikiwemo sindano ,vidonge na kadhalika na manesi walimshauri atumie mipira kwani nayo ni njia moja wapo ya njia ya uzazi


  Hivyo alivyokubali kutumia njia hiyo manesi walimpatia boksi la mipira hiyo ili aweze kutumia njia hiyo kwa kupanga uzazi


  Mwanamke huyo amedai kuwa, alirudi nayo nyumbani na siku hiyo mume wake alitoka nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam na kurudi kesho yake ambayo ni juzi na hakupata muda mzuri wa kutosa kumueleza mume wake kuhusiana na hilo


  Amedai jana mume wake alipekua katika mifuko yake na kukuta boksi hilo la mipira na kuanza varangati na fujo kwa kudhani mipira hiyo huwa naitumia kwa wanaume wengine na alipojaribu kumueleza hakumuelewa na kwa hasira alimamua kumwambia aende kwao kwa muda na hakufanya hivyo nay eye kutoa na aliporudi usiku alinikuta ndipo alisema niondoke usiku huo wka ni alimkera sana wka kumuonyesha dharau ya hali ya juu

  Amedai alijaribu kumbembeleza mumewe bila mafanikio na ndipo mwanamke huyo alitoka nyumbni kwake hapo wka kuona anakaribia kupata kipigo na kuomba msa kwa jirani alale ili asubuhi apate ustaarabu kwa kuondoka kwao
  Tukio hili limetokea maeneno ya Yombo Vituka jijini Dar es salaam

  Hata hivyo NIFAHAMISHE inafanya juhudi kupata mahojiano mawili matatu na mume huyu ili kujua ukweli wa kina kuyhusiana na tukio hilo
   
 2. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #2
  Nov 13, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,047
  Likes Received: 7,507
  Trophy Points: 280
  Family Planning Method imezua balaa, ndiyo maana tukaona kuwa kuna umuhimu mkubwa sana na hivyo kuanzisha kampeni ya male involvement katika masuala ya clinic.
  Ila hapo inabidi councilors toka kituo husika wataarifiwe ili wawezse kumkabili na kumuelimisha mume wa huyo dada.
  Ni suala dogo tu, ila litakuwa ni kubwa kama watadhani ni mambo ya kuwaita wazee wasuluhishe.
   
 3. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #3
  Nov 13, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Kumtimua mke na kichanga usiku wa manane si sawa hata kidogo.

  Ila pia mke naye kwa nini hakuwasiliana na mumewe kuhusu huo mpango wa uzazi? Huyo mke kama angeyajadili hayo na huyo mumewe kabla ya hata kwenda kliniki hayo yaliyomtokea pengine wala yasingetokea.

  Hapo ndo umuhimu wa mawasiliano unapoonekana wazi. Na kama chote kilichoripotiwa kwenye hiyo habari ndicho hasa kilichojiri basi huyo mke naye hana common sense.

  Hivi kweli yeye katika akili yake alidhani kuwa mumewe asingewaka baada ya kuziona hizo condom? SMH!
   
 4. v

  valid statement JF-Expert Member

  #4
  Nov 13, 2011
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 2,737
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Angekuwa anamshirikisha mumewe mambo hayo, mmewe asingekurupuka kumtimua.
  Tatizo mme wala hana habari kuwa mke anataka kutumia njia ya uzazi wa mpango, na anataka kutumia condom kama njia bora kwao!
  Jamaa naye mkurupukaji kweli.... Labda anamjua mkewe.
   
 5. Dr.Chichi

  Dr.Chichi JF-Expert Member

  #5
  Nov 13, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 2,336
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Aisee mawasiliano muhimu sanasana inapokuja kwenye vitu nyeti kama hivyo..au jamaa alikuta box limefunguliwa ku indicate kuwa zimeshatumika?
   
 6. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #6
  Nov 13, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Kulikua na njia nyingi tu za kuweza kuprove kama ni kweli! Huyo mama kama alitaka kutumia condom kwingine,alihitaji box na kulileta home?
  Mawasiloiano takes two jamani! Kuna mtu unamuambia kitu 5 times, anaitika tu ' mhhh?' Unarudia hadi unaamua mwenyewe! Angekua mwanaume wa haja walau angepeleka mkewe hosp!
   
 7. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #7
  Nov 13, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  You never knows with women! Habari za upande Mmoja huenda jamaa anajua anamegewa
   
 8. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #8
  Nov 13, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,135
  Likes Received: 3,327
  Trophy Points: 280
  Aisee jamaa is very ignorant.
   
 9. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #9
  Nov 13, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Mchungaji,hata kama anajua anasaidiwa si kuna taratibu jamani? Kumfukuza mtu usiku? Kama uliweza kuoa kwa utaratibu, alipaswa ampe na nauli ya kurudi kwao na kuwaambia wazazi. Sasa huko lwa jirani alikolala kama ndo kwa small house?
   
 10. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #10
  Nov 13, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,226
  Trophy Points: 280
  hata kama amehsi kuibiwa ndo umfukuze usiku wa manane? Na kichanga? Hamuhurumii mkewa,basi hata huruma na mtoto hana? Kwanza inaonyesha hyo nyumba haina mawasiliano na huyo mwanaume hana utu wala hajali afya ya mkewe, mwanaume halisi lazima angetaka kujua watatumia njia gani kwa sasahata angesafiri akirudi atataka feedback. Na si kufukuza mke
   
 11. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #11
  Nov 13, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,966
  Trophy Points: 280
  Kumfukuza mke na kichanga usiku wa maanane siliafiki.

  Uzazi wa mpango ni swala linalomgusa Mke na Mume, inakuaje mke achukue uamuzi peke yake?. Hapo kuna kosa lingine la kuchukua uamuzi bila ya kumshirikisha mme wake.
   
 12. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #12
  Nov 13, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  inaonyesha huyo mwanaume sio mzinzi
   
 13. Sabry001

  Sabry001 JF-Expert Member

  #13
  Nov 13, 2011
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 1,064
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  mxxx! Huyo mwanaume angeuliza kwanza na sio kuleta valangati na mkewa hadi kumfukuza tena ucku na katoto kachanga. Unajua wanaume wengi wana akili kiduchu km samaki? Wanaish kwa hisia tu!
   
 14. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #14
  Nov 13, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Wanasema hindsight is 20/20. Kwa sasa tunaweza kumtupia milawama kibao huyo mwanaume kwa sababu jambo lishatokea. Lakini usikute yeye kwa wakati ule alikuwa kazidiwa na hisia na hivyo kuwa vigumu kwake ku-reason.

  Lakini pia mawasiliano kwenye mahusiano ni kitu muhimu sana. Inavyoelekea labda hao wawili hawakuwa na mawasiliano mazuri hususan kuhusiana na hilo la mpango wa uzazi.

  Jambo kama hilo ni vema mwenzako akajua kila kitu.
   
 15. L

  Leliro Member

  #15
  Nov 13, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 83
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama habari hii ndo ilivyo, basi wote wamepungukiwa na hekima. Mama alitakiwa kumfahamu mumewe nini anapendelea na kipi hataki. Baada ya kufanya uchambuzi huo then angefikiria amuelezeje habari za kondom kabla ya kuzichukua. Kwa upande wa mume, hata kama alikosa kwa mtizamo wake, angemwacha ikafika asubuhi na kumwamuru atoke kama alivyofanya lakini si kumfukuza usiku kama mwizi. Siku zote familia zinasambaratika kwa kukosa busara kati ya wanandoa. Nina imani hawa watu watarudiana muda si mrefu kwani maamuzi haya yanaonekana yamefanyika kwa hasira. Pindi huyu bwana atakapoona gap katika familia yake ataona umuhimu wa kumrudisha huyu mama.
   
 16. Tumaini Jipya

  Tumaini Jipya JF-Expert Member

  #16
  Nov 13, 2011
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 380
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0


  Aaaaaah acha Matusi wewe,inawezekana wanaume uliokutana nao wewe ndiyo wana akili ndogo!!
  Huyo Mwanamke ndiye uwezo wake kichwani una Mashaka,kama Mume alikuwa anasafiri kwa siku chache na atarudi kwa nini akusubiri kwenda kwa hao Watu wa Uzazi wa Mpango wakati Mumewe yupo?!!
  Wakati ameshakosea,kwa nini mume aliporudi na kumpokea kwa nn basi hiyo haikuwa taarifa ya Pili kumpa mume baada ya Maamkizi?!! "Mke MPUMBAVU huivunja Nyumba yake Mwenyewe",Upumbavu unaozungumziwa ndiyo kama huo!! Inawezekana kumeshawahi kuwa na mashaka kuhusu uadilifu wa Mke ndiyo maana Jamaa ali-over react!! Hata hivyo Mume alipaswa kuwa Mvumilivu angalau kwa muonea Huruma Mtoto mpaka kukuche!!

  Itoshe tu Kusema,Mke/Mume "Mpumbavu" hutoa nafasi nyingi kwa Misunderstandings kutokea na possibly kuivunja Nyumba!!

  Hekima/intelligence pekee haitoshi kuzuia nyumba isianguke lakini hupunguza sana Uwezekano huo!!
  Kwa mfano katika situation kama hii,Mwanamke Mwerevu angempigia hata simu mumewe kumweleza kwamba atakwenda kupata Ushauri wa namna ya kupanga Uzazi na kisanga hiki kisingetokea!!
   
 17. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #17
  Nov 13, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  naona point hapa, inawezekana jamaa alishamkinai huyu mtoto wa kike. akawa anatafuta sababu!
   
 18. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #18
  Nov 13, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,047
  Likes Received: 7,507
  Trophy Points: 280
  Tusiwe conclusive kiasi hicho, ukiisoma habari ilivyo kwa umakini utagundua kuwa mpaka wake haufiki katika conclution uliyoitoa.
  Unajuaje pengine hata mtoto si wa jamaa na jamaa aligundua na baadaye akaamua tu yaishe sasa kitendo cha kukuta condom kimemkumbusha machungu? Habari ipo very brief haijaingia into details ila ime focus kwenye ends/decisions, hivyo niliongealo linawezekana pia.
  Kama nitakuwa sahihi huoni kuwa hujatenda haki kwa conclution na matusi yako?
   
 19. jamii01

  jamii01 JF-Expert Member

  #19
  Nov 13, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 1,836
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  vitu vya msingi kama hivyo vinahitaji wote wawili na si mahamuzi ya mtu mmoja..
   
 20. m

  mjaumbute Member

  #20
  Nov 13, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hapa tatizo ni ukosefu wa mawasiliano kati yao hasa mama hakufanya jambo zuri kuchukuwa hizo zana wakati Mzee yuko safari. Nyie mnasema tu hayajawapata kuna maumivu makali sana hapo
   
Loading...