Afrika: Nchi 10 zenye barabara nzuri Tanzania haimo, Hayati Magufuli alikuwa anafanya nini?

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,895
Salaam Wakuu,

Huwa nasikia watu wanamsifia Magufuli eti ni Baba wa Barabara/Mabarabara, hakutaka Demokrasa Nchini eti yeye ni Hapa kazi tu.

Lakini hakuna kazi hata moja alofanya inatambulika kwa watu wenye akili zao wanaojua nzuri na au maendeleo ni nini.

Hayati Magufuli alivyokuwa anajisifia hadi kujiita Askari wa Mwamvuli kwa kufanya kazi ya barabara vizuri

Umasikini Ujinga na Maradhi; Kundi la Wajinga likapumbaza Taifa eti Hayati ni Mchapa kazi kajenga barabara, sijui Nchi iliibiwa sana hivyo kaongea na Barrick watalipa Kodi trilioni zaidi ya 347, huku bajeti ya nchi kwa mwaka ikiwa haifiki trilioni 40.

Haya mambo ya kumsifia hayati Magufuli tuwaachie Wananchi wa Chato japo hajawahi kuwa hata balozi wao wa nyumba kumi.

Mungu anajibu maombi.
IMG_20221010_062649_067.jpg

Top 11 African Countries With Quality Road🛣

1: Namibia🇳🇦 (score 5.2) world ranking 23

2: Egypt 🇪🇬(Score 5.0)world ranking 28

3: South Africa🇿🇦 (score 5.0) world ranking 29

4: Rwanda🇷🇼 (score 5.0) world ranking 31

5: Ivory Coast🇮🇪 (score 4.7) world ranking 42

6: Mauritius🇲🇺 (score 4.7) world ranking 44

7: Morocco🇲🇦 (score 4.4) world ranking 55

8: Kenya🇰🇪 (score 4.2) world ranking 61

9: Botswana🇧🇼 (score 4.1) world ranking 64

10: Cape Verde🇨🇻 (score 4.1) world ranking

11: Senegal🇸🇳 (score 4.0) world ranking 71

🌐Source: World Economic Forum’s Global Competitiveness Report Index
 
Aibu sana sana kwa nchi yetu speed kuwa 80 kwa zaidi ya 90% ya barabara zetu,yan hata kimara-kibaha highway eti unakuta vibao vya speed 50!tanroad pale sijui wazee wengi ambao hata nje ya nchi hawajatoka kuangalia wenzetu wanavyofanya kwenye barabara!yan tuta tuta na speed limit 80 wanachojua wao!
 
Uliyemtaja ni awamu ya 5 ,umesema hajafanya kitu,hao wengine mbona huwazungumzii?Nchi ulizotaja hapo hizo barabara zilijengwa ndani ya awamu moja au mbili?Ujenzi wa nchi ni mchakato.Siyi jambo la kuamka na mtu mmoja ghafla tu na kutimiza.Sema chama Tawala kwa zaidi ya miaka 40 na awamu zaidi ya nne bado inasua sua katika ujenzi wa nchi kulinganisha na nchi nyingine Afrika.
 
Kwa maana ya quality roads, Tanzania haiwezi kuingia kabisa. Hizi barabara zinazojengwa na Wachina zinazojaa mashimo baada ya mwaka mmoja (nyingine chini ya miezi 6), utaziingiza kwenye quality roads?

Barabara ambayo angalao ilikuwa na kiwango cha juu ni ile iliyojengwa na Denmark (Mikumi to Mafinga) lakini baadaye tena imekuja kuharibiwa kwa kuweka matuta. Uliona wapi highway inakuwa na matuta?

Hizo nchi zote na baadhi ambazo hazimo kwenye hizo 10 best, mijini wana flyovers hasa, siyo yale madaraja yetu ya Ubungo na TAZARA ambayo ukiwa kwenye barabara moja huwezi kubadili kwenda barabara nyingine.

SHIDA YA CHAWA, MAFANIKIO KIDOGO, SIFA INAKUWA KAMA VILE SISI TUMEFANYA MAMBO YA AJABU KULIKO DUNIA NZIMA. TANZANIA KATIKA MAMBO MENGI, BADO TUPO NYUMA.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom