Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,195
- 10,929
Baada ya mahakama nchini Afrika Kusini kumpa ushindi mtu aliyetaka kupigwa marufuku kwa sauti ya adhana katika eneo analoishi,wananchi wa madhehebu mbali mbali na imani tofauti kwenye eneo la Isabingo jijini Durban wameandamana wakiwaunga mkono waislamu wakitaka adhana iendelee kama kawaida.
Kiongozi wa harakati hizo ambaye si muislamu,Rivaaj Ramdas akizungumza kupitia akaunti yake ya facebook mubaashara saa moja kabla ya kuongoza maandamano hayo amesema adhana ni wito mzuri na si kwa ajili ya waislamu peke yao,na ni sauti nzuri ambayo kila mtu anapaswa kuipenda.
Zaidi akasema waislamu nchini Afrika kusini walijitoa muhanga ili kukomesha ubaguzi wa rangi sasa itakuwa na maana gani kwamba baada ya kufanikiwa hilo wanabaguliwa na ibada zao.
Pamoja na hayo akasema mpaka sasa waislamu wanaendelea kuhudumia jamii kwa kuwalisha na kuwahudumia wenye shida kote nchini humo.Kutokana na hilo akasema yeye na wenzake wengi wameamua kujitolea kwa lolote linaloweza kuwapata ilimradi adhana iendelee kwenye eneo lao.
Msimamo wake huo ulionekana kweli si utani kwani muda mfupi baadae mamia ya watu kwa miguu na kwenye magari wakiwa wamebeba mabango walijitokeza barabarani kuzunguka mitaani na spika zikiwa zinatoa adhana kwa sauti zake mbali mbali.