Afrika Kusini: Wakristo na baniani waandamana wakitaka adhana

Alwaz

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
6,830
10,364
Baada ya mahakama nchini Afrika Kusini kumpa ushindi mtu aliyetaka kupigwa marufuku kwa sauti ya adhana katika eneo analoishi,wananchi wa madhehebu mbali mbali na imani tofauti kwenye eneo la Isabingo jijini Durban wameandamana wakiwaunga mkono waislamu wakitaka adhana iendelee kama kawaida.

Kiongozi wa harakati hizo ambaye si muislamu,Rivaaj Ramdas akizungumza kupitia akaunti yake ya facebook mubaashara saa moja kabla ya kuongoza maandamano hayo amesema adhana ni wito mzuri na si kwa ajili ya waislamu peke yao,na ni sauti nzuri ambayo kila mtu anapaswa kuipenda.

Zaidi akasema waislamu nchini Afrika kusini walijitoa muhanga ili kukomesha ubaguzi wa rangi sasa itakuwa na maana gani kwamba baada ya kufanikiwa hilo wanabaguliwa na ibada zao.

Pamoja na hayo akasema mpaka sasa waislamu wanaendelea kuhudumia jamii kwa kuwalisha na kuwahudumia wenye shida kote nchini humo.Kutokana na hilo akasema yeye na wenzake wengi wameamua kujitolea kwa lolote linaloweza kuwapata ilimradi adhana iendelee kwenye eneo lao.

Msimamo wake huo ulionekana kweli si utani kwani muda mfupi baadae mamia ya watu kwa miguu na kwenye magari wakiwa wamebeba mabango walijitokeza barabarani kuzunguka mitaani na spika zikiwa zinatoa adhana kwa sauti zake mbali mbali.

1599461105844.png
 
Attachments

  • 1599460968665.png
    1599460968665.png
    177.6 KB · Views: 13
Nyumba za ibada zisiwe chanzo cha kelele zisizo na tija.

Wafunge maspika yao ndani na kelele zisitoke nje.

Utakuta kanisa moja linapiga kelele mtaa mzima au msikiti mmoja wanapiga kelele mpaka mtaa wa 3 unasikia.

Hii tabia ikome.
Adhana hua inachukua muda gani? Sidhani hata kama inafika dakika 4
Vipi kuhusu makelele yanayopigwa kwenye ma Bar?
Kama hutaki makelele nenda ukaishi peke yako huko porini,kelele ni dalili ya uhai na haziepukiki.
 
Nadhani adhana haiwezi kuingia kwenye kundi la makelele.Sijui kamusi la kiswahili linasemaje lakini naona kama makelele ni maneno yasiyo na mpangilio maalum wala faida yoyote kwa anayesikiliza.
 
Nyumba za ibada zisiwe chanzo cha kelele zisizo na tija.

Wafunge maspika yao ndani na kelele zisitoke nje.

Utakuta kanisa moja linapiga kelele mtaa mzima au msikiti mmoja wanapiga kelele mpaka mtaa wa 3 unasikia.

Hii tabia ikome.
Yaarab tunakuomba waja wako uwaangalie kwa jicho la huruma viumbe wako hawa wanaoikadhibisha dini.

Yaajaalal binadamu hawa wamejisahau sana kiasi cha kuanza kuzitikisa mamlaka zako.
 
Kuna nguvu kubwa za kuvuruga BRICS. Ndiyo maana unaona Brazil, South Africa na India zina Yumba! Hata hivyo, watayapita magumu haya.
 
Adhana hua inachukua muda gani? Sidhani hata kama inafika dakika 4
Vipi kuhusu makelele yanayopigwa kwenye ma Bar?
Kama hutaki makelele nenda ukaishi peke yako huko porini,kelele ni dalili ya uhai na haziepukiki.
Ana mapungufu ya akili huyo ,sasa wafunge vitu kerere zisitoke nje je anaelewa nini lengo la adhana au anaongea uchizi ? Na alaaniwe
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom