Afrika Kusini niijuavyo mimi

Afrika Kusini niijuavyo mimi

Nimeishi South kwa takriban miaka mitano hivi kuanzia 1996 ni mara baada ya Mandela kuachia hatamu na kumkabidhi Thabo Mbeki kijiti.... Kinachotokea sasa huko kina mizizi na ubaguzi wa rangi lakini vilevile kina mizizi na uhuru bila maandalizi mtambuka
Nisirudi nyuma sana kihistoria... Lakini wazungu wahamiaji baada ya kutua kwenye nchi nzuri ya kuvutia ya Africa Kusini, wakaitamani na kupanga mipango ya kuitawala milele.... Hili walifanikiwa kwa kiasi kikubwa mno na wasouth walipokuja kushtuka tayari wakawa kwenye 18 za wazungu
. Wakabaguliwa kwa kila hali
. Wakaundiwa matabaka
. Wakanyimwa elimu
. Wakapenyezewa vibaraka ili wapelelezane wao kwa wao
. Wakanyimwa nafasi za kazi nzuri na maisha yanayomstahili binadamu
. Wale waliogutuka na kutaka kuwakomboa wenzao wakateswa
wakafungwa,
wakazushiwa kesi kubwa kubwa,
wengine wakauliwa na
wengine wakawekwa kizuizini

Binadamu hafugiki kama mnyama... Mapambano ya kudai nchi yao na uhuru wao vikazidi kupamba moto.. Ni katika kipindi hiki wasouth kwa makabila yao yote wakawa kitu kimoja... Ikawa ni mwiko kubaguana
Yakajengwa makambi mengi ya kudai uhuru.. Sauti ikawa moja tu UKOMBOZI NA UHURU basi... Maadili mengine yote yakawekwa kando...
Uadilifu
Utu wema
Upendo
Tafakuri
Maono nknk
Haya yote yakawekwa kwenye kabrasha moja tu UKOMBOZI na UHURU.. Kwahiyo hata wanawake thamani yao ikabaki kwenye kuwahudumia wapigania uhuru...

Hatimaye baada ya mapambano ya muda mrefu sana
Dhuluma nyingi sana
Mateso mengi sana
Ukatili mwingi sana
Vifo vingi sana
UKOMBOZI na UHURU vikapatikana kwa kuachiwa Mandela na kuwa Msouth mweusi wa kwanza kuwa rais... Sasa kazi haikuwa ndogo kuwaheshimisha tena weusi... Kuwapa thamani wanayostahili.. Baada ya kudhauliwa kwa miongo mingi

Mipango mingi ikapangwa... Mojawapo ikiwa ni kuwapatia wasouth wote weusi huduma za msingi bure ama kwa bei nafuu.. Mkakati maarufu ni ule wa nyumba million za Mandela....
Fungate ya UKOMBOZI na UHURU vikawabetesha wengi... Wataliwa wakawa watawala bila maandalizi ya kutosha... Bila elimu ya kutosha bila miiko bila uzalendo vya kutosha...
Kasheshe ikaanzia hapa... Kila Msouth mweusi hakutaka tena kuishi kwenye vibanda... Wakataka nyumba za bure za Mandela.. Bati unanunua mwenyewe.... Nyumba za vyumba vitatu... Basi ikawa mtu akiiipata nyumba, akawa na TV ndani na mziki mkubwa basi huyo kawin maisha hataki chochote tena...

UKOMBOZI na UHURU vikawapa jeuri mbaya sana.. Ile nguvu kazi ya taifa ambao asilimia 90 ni vijana wakawa na nguvu kubwa kwenye maamuzi... Msouth mwisho wake wa kufanya kazi ni Ijumaa mchana... Baada ya hapo mlipe chake akalakale bata mpaka Jumapili jioni... Jumatatu anaamka na nauli tu...
Haya ndio yakawa maisha yao... Ndani ya nchi yao huru.....

Uhuru wa Afrika Kusini ukafungua milango kwa mataifa mengine... Wawekezaji wapya wakaja.. Lakini pia watafuta maisha wengine toka mataifa mengine pia hasa ya kiafrika wakamiminika south.. Hawa wakawa hawana shobo wala maringo.. Hawachagui kazi.. Hawachagui maslahi na wanapiga mzigo hadi Jumapili

Wawekezaji wakaona tofauti kubwa kati ya mgeni na mwenyeji... Wakaona tija ya utendaji wa wageni.... Kidogo kidogo wasouth wakaanza kukosa kazi... Wageni wakawa kimbilio la wawekezaji wengi... Wanasiasa wakachelewa kuliona hili... Wakawa busy na yao

Wasouth kuja kushtuka kazi nyingi zikawa zinafanywa na wageni
Wageni wengi wana maendeleo kuliko wao
Wageni wengi wanapendwa na wawekezaji kuliko wao... Chuki ikaanzia hapo...

Wakaanza taratibu kuwadhibiti wageni
Ukitaka Kuishi nao vizuri fuata watakayo wao
Ukitaka Kuishi nao vizuri usiwe na maendeleo yoyote
Ukitaka Kuishi nao vizuri kila weekend mkale bata
Ukitaka kuishi nao vizuri usimiliki Nyumba nzuri, gari au mwanamke mzuri.....

Ukifanya tofauti na haya
Wanakujengea bifu
Wanatafuta watu wakupore
Wanatafuta watu wakupige
Wanakuhmchongea Uhamiaji
Wanakuroga usifanikiwe

Wageni kuja kugundua haya wakabadili mbinu nyingi.... Sasa miongo imepita... Wageni ndio wenye mafanikio kule... Wenyeji bado wako kwenye mawazo mgando ya UKOMBOZI na UHURU.... Bado wako kwenye fungate wakidhani serikali itawafanyia kila kitu... Sasa hawana aibu tena hawawataki wageni kwasababu ya uvivu wao.... Ni mwendo wa mauaji

#RIP Charles (Mak. ma)
#RIP SundiOmolo
#RIP Makaveli
#RIP Kapinga
# RIP Mandy
My college mates.... Wote hawa vifo vyao vilitokana na mikono dhalimu ya weusi wenzao

Napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru Mungu kwakuwa nilinusurika kifo mara nne nikiwa South
Mara ya kwanza ghetto kwa demu... Nilitoroka kupitia dirisha dogo la chooni wakati jamaa wanavunja mlango waingie wanimalize...
Mara ya pili bar ya Zithobeni niliwahi kuikwepa chupa ya bia in split of seconds nikiwa na demu huyo huyo wa kule ghetto
Mara ya tatu usiku huo huo nilitekwa ila nikafanikiwa kuruka kwenye gari na kujisalimisha kwa police waliokuwa kwenye patrol
Mara ya NNE kwenye kanisa la kuabudu shetani Witbank.... [emoji848][emoji848][emoji144][emoji144][emoji144][emoji144]

Maybe I was left to tell...!!!
Analysis nzuri. SA walipata uhuru 1910
 
Ingia hapa

Kuna Batch ya vijana ilichukuliwa au kuandaliwa na Bhudhist Temple ya Upanga na ilifanyiwa Medical examination enzi hizo St.Mary's Hospital kule Kawe mbele ya daraja la Mlalakuwa, hiyo Medical examination ilisimamiwa na Dr.Madinda nami nilimsaidia. Ilikuwa miaka hiyo 1997 nakumbuka, vijana waliokuwa vizuri kiafya walipelekwa South Afrika.
Nawe ulikuwa miongoni mwao au wewe ulikuwa uliisha tangulia wakati huo?!
Nimekumbuka hao vijana nilishiriki medical examination yao hiyo miaka, kama ni hiyo batch nami nilikufanyia medical exam, wengine walitoroka baada ya kufika South Afrika wakaelekea Australia na wengine Marekani ya U.S.A.
 
Kuna Batch ya vijana ilichukuliwa au kuandaliwa na Bhudhist Temple ya Upanga na ilifanyiwa Medical examination enzi hizo St.Mary's Hospital kule Kawe mbele ya daraja la Mlalakuwa, hiyo Medical examination ilisimamiwa na Dr.Madinda nami nilimsaidia. Ilikuwa miaka hiyo 1997 nakumbuka, vijana waliokuwa vizuri kiafya walipelekwa South Afrika.
Nawe ulikuwa miongoni mwao au wewe ulikuwa uliisha tangulia wakati huo?!
Nimekumbuka hao vijana nilishiriki medical examination yao hiyo miaka, kama ni hiyo batch nami nilikufanyia medical exam, wengine walitoroka baada ya kufika South Afrika wakaelekea Australia na wengine Marekani ya U.S.A.
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]dah umenikumbusha mbali sana... Nilikuwa mmojawapo lakini ndio nilikuwa kiongozi .... Walioko nje ya nchi nawajua ila siwezi kuwataja hapa...
Yes ulinihudumia ila siwezi kukukumbuka nawe huwezi kunikumbuka nina hakika... Kweli maisha duara.. Thanks JF
 
Hapana kuna wabongo wa kila aina south
Waganga wa kienyeji feki
Wauza bidhaa mitaani
Madalali
Wapagazi
Wafanyakazi kwenye taasisi
Wafanyakazi kwenye makampuni
Makuwadi
Mashoga
Wauza madawa
Wafanyabiashara nknk
Kuna kijana nahisi kweli ni shoga huko, kwasababu alipokuwa akifanya kazi Sea Cliff hotel enzi hizo, alianza kujichubua ngozi na akawa mweupe, na alikuwa na mke na walikuwa na mtoto mmoja, lakini alibadirika ghafla na minong'ono ikaenea kwamba ni shoga, ghafla akatuambia amepata nafasi ya masomo ya upishi huko South Afrika, lakini wafanyakazi wenzake Sea Cliff wakatuambia kuna beberu lililo kuwa likihisiwa kumfanyia ujangili huo ndio lilimpeleka huko South Afrika haikujulikana kufanya nini, alitoroka familia yake na mpaka leo hakuna hajuaye alipo, hivyo kuna hisia alipelekwa huko kama kuficha watu, wasifahamu lakini pia inawezekaa ndiyo biashara yake huko, maana hana mawasiliano na familia yake huku nyumbani.
Sasa sijui haya machafuko yeye atarudia au kesha kubali kupambania hali yake huko aliko.
 
imebidi nicheke badala ya kuhuzunika, pole sana kwa kuruka vihunzi vyote ,una maisha marefu. Ona unavyotupa elimu kuhusu ulimwengu wa roho, hungekuwepo tungepata wapi hiyo elimu?
 
Mkuu...unakumbuka ile thread ya kwamba wewe ni Agent wa shetani..? Aisee hakuna tusi nilikosa mule..leo umesema ulikua kwenye kumuabudu shetani wanashangaa....yaani wanashangaa mpare na samaki?
 
imebidi nicheke badala ya kuhuzunika, pole sana kwa kuruka vihunzi vyote ,una maisha marefu. Ona unavyotupa elimu kuhusu ulimwengu wa roho, hungekuwepo tungepata wapi hiyo elimu?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji123][emoji123][emoji123]
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]dah umenikumbusha mbali sana... Nilikuwa mmojawapo lakini ndio nilikuwa kiongozi .... Walioko nje ya nchi nawajua ila siwezi kuwataja hapa...
Yes ulinihudumia ila siwezi kukukumbuka nawe huwezi kunikumbuka nina hakika... Kweli maisha duara.. Thanks JF
Basi ni siku nyingi bali nimekumbuka hilo kundi, kama ulivyosema siwezi kukumbuka, ila nilimsaidia Dr.Madinda yeye na Mkewe Dr.Madinda mjamaika.
Kuna baadhi walirudi nilikutana nao walinipa story za baada ya kufika kule ile university na walikaa kidogo, kisha waliingia mitini, hao wao walikuwa Astralia wakatia huo.
Dunia duara, ila naweza kukufahamu nikikuona maana kumbukizi zangu huwa za ajabu, hao jamaa nilikutana nao 2010 na niliwakumbuka, ila wao hawakunikumbuka mpaka nilipowakumbusha nao walishangaa sana tangu 1997 nimewakumbukaje.
Pia nimemkumbuka mmoja wenu tulimkatalia jina nalikumbuka majina yake yalikuwa S.S utanielewa.
 
Biashara ni biashara tu, hakuna uharamu wowote. Asipouza yeye wengine watauza, na hata asipouza yeye watumiaji wapo tu, yeye ana fanya biashara kama wengine tu.
Sina namna ya kukusaidia
 
Umewasahau masela wa kitanga waliojaa cape Town
Wanasema mnauza drugs, mnawaingiza mabinti zao kwenye ukahaba, pia human trafficking mnahusika ndo mana hawawataki. Ila kusema ukweli wapo wabongo wachache wana kazi zinazoeleweka south ila kiukweli asilimia kubwa wabongo ni wauza drugs south, tena wamejaa watoto wa magomeni, ilala, na kinondoni kibao tuu ndo wame control biashara ya drugs south kuzidi hata wanigeri. Wabongo kushirikiana na wa Pakistani wanaongoza kuuza heroin south africa. Acha tu wapigwe.
 
Nasikia mji wa Pretoria WTZ kule wamekumiliki KAMA kwao! mishe mishe zoote KUANZIA ngada, bange, ujambazi wao NI ma-godfather HAWANA mpinzani! NI territory yao![emoji44] kuna ukweli Mkuu Mahaba Jr [emoji50]
Kama kweli wanafanya matendo hayo acha washughulikiwe tu.
 
Warudi waje kuuzia drugs wanetu!
Wabaki huko huko wawauzue wazulu na wa Xhosa
kwa taarifa tu asilimia 95% ya watanzania walioko afrika kusini wanauza madawa ya kulevya, biashara wanazofanya kama saluni, maduka ya nguo ndio vituo vyao vya kuuzia madawa, waambieni warudi nyumban la sivyo watauwawa kama kuku
 
Duh,kumbe kuna matukio sana aisee.
Inawezekana walipigwa repatriation halafu wakaishia jela za Msumbiji
Aloyce Kapinga ambaye kwasasa ni marehemu aliwahi kupitia hiyo hali... Baada ya kukamatwa kule mahabusu akakutana wa wajuzi wakamwambia asiseme anatoka bongo kwakuwa atarudishwa kwa ndege bali aseme anatokea Msumbiji ambapo safari ni kwa train
Kwanini safari ya train ni nzuri? Kwa vile kuna chances za kutoroka...
Yeye alifanya hivyo na train ilipofika huko katikati mbugani kwenye kona kali ikapunguza mwendo kuepusha ajali hapa ndio maaskari wasindikizaji huwatangazia wale waliokamatwa mwenye RAND 100 atoe apewe nafasi ya kuruka kabla treni halijamaliza kona na kuongeza mwendo
Kapinga na vijana wengine wawili wakatoa... Lakini baada tu ya kutoa wakasachiwa tena na kuchukuliwa pesa zao nyingine kisha wakaruhusiwa kuruka
Kapinga aliruka na kutua salama lakini kijana mmoja alivunjika niguu yote.. Hapo hakukuwa na kusaidiana kila mmoja alijua lwake
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]dah umenikumbusha mbali sana... Nilikuwa mmojawapo lakini ndio nilikuwa kiongozi .... Walioko nje ya nchi nawajua ila siwezi kuwataja hapa...
Yes ulinihudumia ila siwezi kukukumbuka nawe huwezi kunikumbuka nina hakika... Kweli maisha duara.. Thanks JF
Duh nami nimekumbuka nimeanzia mbali sana kikazi. Sasa enzi hizo ndiyo nilikuwa kuleee kama junior staff hahaha, unanielewa.
 
Back
Top Bottom