Afrika Kusini: Mchungaji Alph N Lukau afufua maiti na kuacha gumzo kubwa

Hili jambo limewatia aibu karibu walokole wote duniani

View attachment 1032982

Bila shaka walokole wa Tanzania mna cha kujifunza
Walokole wamefanya miujiza ndio Yesu wao. wanadai bila miujiza hakieleweki. Mungu awasaidie waelewe utapeli unaoendelea kwa muda mrefu kwenye makanisa yao. Ukisikia kanisa halina mfumo wowote na linamilikiwa na mtu binafsi anayejiita nabii na mtume au mtume au nabii ,jihadhari nalo. Huyo ana maslahi binafsi
 
Kuna jambo sisi kama wakristo tunakosea sana. Ni pale tunapoacha kumtumainia kristo na kuhangaika na hawa manabii wa kishetani. Mimi binafsi siupingi ulokole lakin kuna baadhi ya walokole hawajielewi. Mtu anakuambia ameokoka lakini mategemeo yake yote yapo kwa mchungaji na sio kwa YESU. Yaan kuna baadi ya walokole wanadhani ulokole ni kutenda miujiza ya ajabu kiasi hiki.

sent using
 
Maandiko yanasema tuyaonayo haya sisi kuomba sana maana mwisho u karibu mno, hatuna haja ya kumpinga wacha atimize maandiko 2 moto wa msubiri milele
 
Kale ndo katapeli kakubwa.
Mtu anatembea angani kwa lengo gani?
Mungu sio wa showoff.
Kwani ile video inaonyesha upandeupande. Ni chizi tu ataamini kuwa pale Bushiri anatembea angani.
Makaika ni invisible, na wakiamua kujidhihirisha kwako basi macho yako ya kiroho ndiyo yatafumbuliwa kwanza ili uwaone. Je, camera ya kanisa lile ilifunguliwa macho ya rohoni?
Je, watazamaji wa YouTube walioiona ile video macho yao yalifunguliwa?
Nina mavideo yake mengi tu ya kitapeli
Mbona hata Gwajima wetu naye huwa anafufua? Na kurudisha misukule?

Ukristo umeingiliwa haki ya nani. Na kale kajamaa kengine katapeli kanakoitwa sijui Bushiri kalikojifanya eti kuelea angani na kanisa lake kutembelewa na malaika wakati ibada ikiendelea. Hovyo kabisa !!!
 
Nimewaza kwamba huu ni mtego aliwekewa maana kwa jisni scenario ilivyo nahisi wa south wamemiwekea mtego .Pstor huyu ni mkongoman na wasaouth awataki kabisa watu kutoka mataifa maengine ya afrika kuwa juu yo ,mfano wamemtengenezea bushiri jungu mpka katolewa sasa nadhani ilikuwa ni huyu kabakia sababu ukiangalia pastor alikuwa anaendelea na ibada mara akaambia nje kuna mwili ulikuwa unapitishwa ila kufika maeneo haya ukaanza kupumua, so pastor akaamua kutoka nje so baada ya tukio hili wasouth waliiomba serikali ndio mana SBC waliamua kwenda Mortuary kuuuliza kwamba je kuna mwili ulikuwa huku wakakataa wakasema hamna ,so hii nahisi ilikuwa mtego na wamefanikiwa

Sent using Jamii Forums mobile app
Bodafasta mtumishi wa Mungu hawezi kuingizwa mtego wa kishetani namna hii. Kama wamemtega kweli wanajua ni mtumishi mwongo. Tena watakuwa wamefanya vema kwani maandiko yanasema tuzijaribu hizo roho tuone kama zimetoka kwa Mungu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Walokole wamefanya miujiza ndio Yesu wao. wanadai bila miujiza hakieleweki. Mungu awasaidie waelewe utapeli unaoendelea kwa muda mrefu kwenye makanisa yao. Ukisikia kanisa halina mfumo wowote na linamilikiwa na mtu binafsi anayejiita nabii na mtume au mtume au nabii ,jihadhari nalo. Huyo ana maslahi binafsi
100%
 
walokole wa kweli ni wale wa zamani waliokuwa WANALIA hawa waliokuja na technolojia ya upako ni wawekezaji wa sadaka na wanamazingaumbwe,
umenikumbusha mbali sana wale walokole wa enzi za mwalimu walikuwa wanalia ibada nzima yaani full kulia
 
Anointing is not the issue. The issue is the source of the anointing...

"Mtawatambua kwa matunda yao..."
Mkuu umenena kweli. Mbona manabii wa zamani kwenye biblia walikuwa wakichaguliwa kuwa manabii walikuwa wagumu kukubali wito .Angalia hapa chini Musa alivyovutana na Mungu hadi kukubali kufanya kazi yake.

Kutoka 4:10-17''Sasa Musa akamwambia Yehova: “Ee Yehova, niwie radhi, lakini sijawahi kuwa msemaji mwenye ufasaha, tangu zamani na hata baada ya wewe kuzungumza nami mtumishi wako, kwa maana mimi si msemaji mzuri* na ulimi wangu ni mzito.”+ 11 Yehova akamuuliza: “Ni nani aliyemuumbia mwanadamu kinywa, au ni nani anayewafanya wawe bubu, viziwi, waone vizuri, au wawe vipofu? Je, si mimi, Yehova? 12 Basi nenda sasa, nami nitakuwa pamoja nawe utakapokuwa ukizungumza,* nami nitakufundisha unalopaswa kusema.”+ 13 Lakini akasema: “Ee Yehova, niwie radhi, tafadhali, mtume yeyote unayetaka kumtuma.” 14 Ndipo hasira ya Yehova ikawaka dhidi ya Musa, akasema: “Namna gani ndugu yako Haruni,+ Mlawi? Ninajua kwamba anaweza kuzungumza vizuri sana. Na sasa yuko njiani anakuja hapa kukutana nawe. Atakapokuona, moyo wake utashangilia.+ 15 Basi unapaswa kuzungumza naye na kuweka maneno hayo kinywani mwake,+ nami nitakuwa pamoja nawe na yeye pia mnapozungumza,+ nami nitawafundisha jambo la kufanya. 16 Atazungumza na watu kwa niaba yako, naye atakuwa msemaji wako, nawe utakuwa kama Mungu kwake.*+ 17 Nawe utachukua fimbo hii mkononi mwako na kuitumia kufanya zile ishara.”+
 
Back
Top Bottom