souljah meditater
JF-Expert Member
- Oct 15, 2012
- 2,146
- 2,098
Ikumbukwe kwamba waafrika wengi walichukuliwa kinguvu na kimabavu kwenda nchi za ulaya na uarabuni kwa lengo la kutumikishwa kufanya kazi ili kuongeza uzalishaji wa mataifa hayo husika.
Tambua THEY DID NOT TAKE SLAVES but they took Doctors, architects, enterprenuers, astronomers, fathers, mothers, daughters, sons, brothers, sisters and e.t.c AND MADE THEM SLAVES.
Kipindi hicho madini na vito ndio ulikuwa utajiri wa dunia hivyo walifika Afrika na kuchukua mali zetu pamoja na ndugu ambao walikuwa chanzo kikubwa cha maendeleo yao.
Inasikitisha kuona waafrika wengi wanaumizwa na utumwa wa waisraeli uliofanyika misri miaka mingi iliyopita na kusahau utumwa wa mababu na bibi zetu ambao madhara yake yanatuumiza mpaka sasa.
Kiukweli hatuhitaji kuomba misaada nchi za ulaya ila tunatakiwa kudai haki yetu ya kulipwa fidia kwa matokeo ya biashara ya utumwa waliotufanyia waafrika.