Africans are "misplaced human beings" in this planet

Africans are "misplaced human beings" in this planet

Asante ila hapo panazidi kuchanganya.Je Mzungu wa Africa kusini ni mwafirika au Caucasian?mtu wa misri,Morocco au Algerian ni mwafirika au Caucasian? Kwa mtizamo uliotoa Mzungu ni race.Je tunaweza mchanganua mwafirika kama ulivyomchanganua Mzungu?sina uhakika lakini labda tukienda ki genetic tunaweza mchanganua mwafirika ni nani?
Mzungu wa Afrika Kusini au Mmorocco au Algerian ni Mwafrika by nationality lakini Caucasian genetically. Ni kama hata ukikaa Ulaya au Marekani miaka 300 bado utakuwa "Negroid". Kwa hiyo ndio maana kuna African Americans, Afro Brazilians, n.k.

Mwafrika naye ana tofauti zake. Kuna Wabantu kama Wasukuma, Wachaga, Nilotes kama Wajaluo na Wamasai, Kushites hao sijui ni Wabarbaig, Wahabeshi na Wasomali, (ambao walihamia kutoka Uarabuni mamia ya miaka iliyopita).
 
Sawa, mbona tuko nyuma kimaendeleo sasa?!
unafikiri wazee wetu walikuwa na akili mbovu kama tulizo nazo leo? kizazicha watu wasio fikiri wanaodhani kuwa ili wao waishi wanahitaji huruma ya mzungu,tumebeza historia yetu ndo maana leo tuko hapa,ndo maana wazee wa zamani walimpinga mkoloni na aliondoka,au alijua kuwa hawa watu hawanitaki kwa kuwa naharibu mfumo wao wa maisha,sisi tumekubali wazungu watawale fikra zako,
 
Tuache maneno mengi tujadili huu mfano mdogo tu hapa:

Nchi za kiafrika tumezungukwa na mito,maziwa na vyanzo vingine vingi tu vya maji.Lakini jiulize uwezo wetu wa kumudu kutumia vyanzo hivi vya maji kwa kilimo cha umwagiliaji ukoje kulinganisha na watu katika mabara mengine?

Kwanini kila siku sisi tu ndo tunaolia njaa na ukame?Mbona wenzetu wanazalisha mpaka ziada kwa kutumia kilimo hikii cha umwagiliaji na kutusaidia sisi Waafrika?

Unahitaji ushahidi gani kusema mwafrika ana tatizo katika kumudu mazingira yake yake ili aweze ku-survive?
Nakubaliana na hoja yako to the point, kwa sababu Waafrika tunang'ang'ania hii dhana ya kuwa na rasilmali, lakini rasilmali bila elimu au ujuzi haisadii chochote.

Hii ndio ule mjadala wa nurture or nature. Waafrika tuko hivi kwa sababu tumeumbwa hovyo au tumezoezwa hovyo. Mimi nina submit ni kwa sababu tumezoezwa hovyo, badala ya kukabili mazingira tunataka shortcuts za kikombe cha babu, kufanya maombi, kupiga ramli. Hamna muujiza utakao toka popote, binadamu ni master of his/her own destiny. Na uozo wa viongozi wetu ndio unaosisitiza ujinga huo.

Nakumbuka nilivyokuwa chuo nachukua darasa moja la Calculus na msichana mmoja wa Kichina. Alikuwa mkare kwa sababu kila mtihani alikuwa wa kwanza. Akawa anasema wakati mwingine Wazungu wanamkera kwa sababu wana assume tu kwa sababu yeye ni MAsia basi hesabu inapanda tu. Akawa anasema kila akifika nyumbani ni kufanya homework na kurudia kusoma tena mara nyingi. Siyo kwamba alizaliwa na gene ya hesabu na sayansi, akijikuna tu anapata material.

Kwanini Haiti(nchi ya watu weusi huko Amerika ya Kaskazini) ndio wanaokufa na kipindindupindu tu?
Nimegusia kidogo huko juu sababu za Haiti kuwa maskini. Watumwa walitolewa Afrika kwenda kufanya kazi kwenye mashamba ya miwa. Wakawatimua mabwana wao Wafaransa karne ya kumi na nane, Marekani na Ufaransa wakawawekea vikwazo vya uchumi. Sasa hivi ni kisiwa kilichojaa watu, msongamano, hamna ardhi ya kulima au kufanya lolote, na hata huo mji wao mkuu Port au Prince ni kama Dar es Salaam nzima ikiwa Uwanja wa Fisi. Na kipindu pindu kinapenda sehemu yenye msongamano.

Hicho kisiwa hakikutakiwa kiwe nchi, lakini siyo kama waliamua wenyewe.
 
unafikiri wazee wetu walikuwa na akili mbovu kama tulizo nazo leo? kizazicha watu wasio fikiri wanaodhani kuwa ili wao waishi wanahitaji huruma ya mzungu,tumebeza historia yetu ndo maana leo tuko hapa,ndo maana wazee wa zamani walimpinga mkoloni na aliondoka,au alijua kuwa hawa watu hawanitaki kwa kuwa naharibu mfumo wao wa maisha,sisi tumekubali wazungu watawale fikra zako,
Kitendo cha kukubali wazungu watawale fikra zetu ni dhahili kwamba wanatuzidi kiakili.
 
Asante ndugu. Nimetafuta jibu kama lako. Kidogo ningekata tamaa. Hakuna kitu kinacho nisikitisha kama kutokujua historia yetu. Bahati mbaya elimu yetu inafundisha zaidi historia ya utumwa na biashara. Ninaamini kabisa waafrika tuliweza kuishi vizuri, kwa teknolojia iliyoakisi mazingira yetu; bila kuharibu mazingira kama teknolojia nyingi za siku hizi. Tulikuwa na dawa za mitishamba zilizoweza kupatikana na mtu yeyote bila kujali ana hela ya kununulia au la.

Tulikuwa na matatizo yetu pia na ukomo wa ujuzi lakini hatukuwa mbumbumbu kama tunavijalaumu huku. Shida kubwa hatukuwa na namna ya kuweka rekodi vizuri kama wenzetu na nyingi zilizokuwepo ziliharibiwa makusudi. Kutokujua historia yetu vizuri ndio tatizo kubwa la kutokufahamu thamani yetu.

Nashukuru kwa vitabu. Nitaenda kuvitafuta.
Mkuu hongera kwa kukiri kwako na Mungu Atakubariki,record zipo,ila zimeharibiwa,ndio maana Egypt kitovu cha historia na Nigeria hasa kuhusu masula ya civilization,hawa jamaa wameharibu hizo sources either kwa vita,au kuamisha makumbusho zetu,ndo maana watu wanaamini kuwa muisraelwa kweli,ni mtu mweusi sio wayahudi coz hao ni watu wa egypt waliohama kipind cha faraoh
 
Unawezaje kuyatawala mazingira yako kama unaweza kupata muda wa kukakaa chini, kufikiri na kuandika upuuzi mrefu hivyo. Kwanini usitumie hata nusu tu muda huo kuangalia jinsi ya kuboresha maisha yako binafsi! Maisha yako hayafai na unatumia muda zaidi kuandika ili ku-justify kuwa maisha yako hayafai.
 
Unawezaje kuyatawala mazingira yako kama unaweza kupata muda wa kukakaa chini, kufikiri na kuandika upuuzi mrefu hivyo. Kwanini usitumie hata nusu tu muda huo kuangalia jinsi ya kuboresha maisha yako binafsi! Maisha yako hayafai na unatumia muda zaidi kuandika ili ku-justify kuwa maisha yako hayafai.
Kipi cha uongo hapo?
 
Unawezaje kuyatawala mazingira yako kama unaweza kupata muda wa kukakaa chini, kufikiri na kuandika upuuzi mrefu hivyo. Kwanini usitumie hata nusu tu muda huo kuangalia jinsi ya kuboresha maisha yako binafsi! Maisha yako hayafai na unatumia muda zaidi kuandika ili ku-justify kuwa maisha yako hayafai.
Mleta post ana uchungu jinsi tusivyoweza kuyatawala mazingira yetu. Maisha tunayoishi tangu kunapambazuka hadi jua linazama yana mkono wa huyo 'mzungu!'

Kwa nini hatuwezi kuendesha vitu vikubwa?!
 
Kitendo cha kukubali wazungu watawale fikra zetu ni dhahili kwamba wanatuzidi kiakili.
Na siyo kwamba Wazungu wanajali sana nani kavumbua hiki au nani kavumbua kile. Ni Waafrika tu ndio tunashikilia hili. Wao wanajali kuwa sasa hivi unafanya nini. Ndio maana Wachina au hata Wajapani hawaoni aibu kukopi teknolojia ya Mzungu, kwa sababu cha muhimu ni kama inasaidia jamii yako. Lakini sisi Waafrika hatutaki kusonga mbele kwa sababu ya kutokujiamini.
 
Hilo ndiyo tatizo la waafrika wengi na wewe ukiwemo: kujidharau na kubeza viongozi wako. Hatuendelei hadi tuongozwe na madkteta kama hawakuuawa kwa kigezo cha haki za binadamu. Naamini kuna nchi mpya na mbingu mpya najishughulisha nayo kuliko hii iliyochoka
 
Hilo ndiyo tatizo la waafrika wengi na wewe ukiwemo: kujidharau na kubeza viongozi wako. Hatuendelei hadi tuongozwe na madkteta kama hawakuuawa kwa kigezo cha haki za binadamu. Naamini kuna nchi mpya na mbingu mpya najishughulisha nayo kuliko hii iliyochoka
Ok, rudia msokoto wako. Utakuta rafiki yako amemaliza kuvuta bangi yote.
 
Kitu kikubwa mi nalaumu ni mitaala yetu,ukisoma historia ya mwafrika anaonekana kuwa wakat mzungu anakuja mwafrika alikuwa amelala anamsubir mzungu amfundishe kuandika,kitu amabcho sio kweli,waafrika walikuwa wamekwenda mbali sana kimaendeleo,hebu angalia jinsi watu wa waliokuwa pembezoni mwa mto nile walivyoudhibit mto mafuriko yake kwa ajili ya matumiz yao,soma dawa za ki afrika zilizokuwa zinatumika kuhifadhia maiti zaid ya miez mitatu bila kuharibika,ona Dr Livingstone baada ya kufa kwake alivyo hifadhiwa na kusafirishwa kwao bila tatizo,
Wakat akina Vasco wanakuja kutafuta njia ya kwenda India,aliwakuta tayari waafrika wanafika north sea na kwendahadi nchi za asia kufanya biashara,bidhaa zilizomfanya Vasco apate na shauku ya kufuatilia hivo vitu vinatoka wapi? aliwakuta tayar waafrika wanacheza na biashara kama kawaida,na walim regard kama mfanya biashara wa kawaida kama wa asia,ndipo alipoenda kuwakomba wamisionari na hapo ndo sura ya vasco kama mkoloni ilipoanza kujionyesha,
Mpaka leo hii tunavyoongea wazungu wanakubali kuwa tiba asili kutka Afrika na Asia ndio rafiki wa afya ya binadam,sasa tumekuwa brainwashed mpaka tunaamin kunywa dawa za asili ni uchawi,magonjwa karibia 99% yanatibika kwa dawa za asili
 
Mkuu Uliza Bei sio kwamba tunajidharau ila inabidi ifike hatua tukubali tu,

Inafikia hatua unajiuliza hawa watu wanafikirije?
 
Mpaka leo hii tunavyoongea wazungu wanakubali kuwa tiba asili kutka Afrika na Asia ndio rafiki wa afya ya binadam,sasa tumekuwa brainwashed mpaka tunaamin kunywa dawa za asili ni uchawi,magonjwa karibia 99% yanatibika kwa dawa za asili
Hata dawa za hospital huwa base yake ni tiba asili, lakini jamaa kabla ya kunywa akikwambia uchinje kuku mweusi na kuzunguka mbuyu mara saba, inabidi umkimbie.
 
Badala ya kukasirika na kuvimba kwa nitakachokiandika,jipe muda kwanza wa kuyatafakari maneno yangu kabla ya kunihukumu na pengine kutukana n.k.

Hivi wewe mwafrika mwenzangu una amini kweli sisi waafrika tulipaswa kuishi katika hii sayari?

Mnyama ana kitu kinaitwa "adaptation" kinachomwezesha kuyakabili na kuyamudu mazingira anayoishi.Je,unafikiri sisi Waafrika tunayamudu na kuyatawala mazingira tunayoishi ili tuishi vizuri kama viumbe wengine?

Mnyama akila akashiba inatosha kabisa na anakuwa ameridhika na ninaweza kusema anamudu mazingira yake.Lakini,je na wewe binadamu hali ni hiyo?

Hebu turudi kidogo kwenye historia.Historia inatufundisha kuwa watu kutoka mabara mengine: wazungu,waarabu, n.k, walikuja Afrika kutafuta maliasili kwa ajili ya viwanda vyao huko ulaya na pia kutafuta masoko kwa ajili ya bidhaa wanazozalisha huko Ulaya na kwingineko.

Maswali ya kujiulizi:

Sisi Waafrika tuligundua kuwa tuna hizi maliasili kabla ya ujio wa hawa wageni kutoka mabara mengine?

Kama tulikuwa hatujui umuhimu wala thamani ya hivi vitu,je unaamini viliumbwa kwa ajili yetu?

Kama kweli viliumbwa kwa ajili yetu, inakuwaje hata tu uwezo na maarifa ya kutambua kuwa hii ni maliasili muhimu inakuwa ni tatizo?

Kingine cha kujiuliza,kama kweli hizi maliasili ziliumbwa na mungu(nature) kwa ajili ya mtu mweusi, inakuwaje mungu huyo huyo atunyime sisi Waafrika uwezo wa kuwa na teknolojia ya ku-process maliasili hizi na badala yake uwezo huo akawapa tu watu kutoka mabara mengine?

Je,huu si ushahidi kuwa sisi tuko katika hii sayari kimakosa tu na wala hatukusatahili?

Kama tulistahili kuishi katika hii dunia na wakati huo huo tumenyimwa maarifa(teknolojia n.k),je huu si ushahidi kuwa ilipangwa tutawaliwe na watu wengine wenye maarifa kutuzidi?Je,huu si ushahidi kuwa hata ukoloni ulikuwa ni mpango wa mungu(nguvu za asili)?

Uongozi na kujitawala:
Ukiangali asili ya mwafrika kujitawala,utagundua tuliumbiwa kujitawala katika ngazi za koo au makabila tu na si kwa ngazi ya leo hii kinachoitwa nchii au Mataifa ya kiafrika.Kabla ya ujio wa Wakoloni hatukuwa na kitu kinachoitwa Tanganyika,Uganda,Zimbabwe, n.k na ndio maana mpaka leo hii Waafrika demokrasia kwa ya kujitawala wenyewe imetushinda.Haya mambo tumelazimishwa tu tulistahili kutawaliwa na machifu na wafalme tu wa makabila yetu.

Maradhi:
Inakuwaje sisi Waafrika tuletwe katika hii dunia yenye maradhi mengi ili hali hatukupewa uwezo wa kukabilana na maradhi haya kama kweli tulitakiwa kuishi katika hii sayari?Kuna dawa gani ya asili leo hii inayoweza kutibu ugonjwa kama kipindupindu?Matibabu ya upasuaji bila wageni tungeyaweza wapi?

Kitu kingine.Jiulize ni kwanini samaki anaweza kuishi baharini tu na si nchi kavu na ni kwanini wewe huwezi kuishi baharini bali nchi kavu tu?Kuna uhusiano mkubwa sana kati ya mazingira tunayoishi na uwezo wa kuyatumia/kuyamudu mazingira haya ili tuweze kuishi.

Hiyo ni mifano michache tu ila swali kubwa na la muhimu hapa ni kuwa,kama Waafrika tulipangiwa kuishi katika hii sayari,ni kwanini basi tumenyimwa uwezo wa kuyamudu mazingira haya ili tuweze kuishi katika hii sayari bila msaada wa watu kutoka mabara mengine?

Binafsi nina majibu mawili hapa:

Mosi,hii sayari haikuumbiwa mtu mweusi na pengine tuliletwa hapa duniani kimakosa tu ila kuna sayari ambayo ilitufaa sisi watu weusi isiyo na changamoto hizi ambazo bila wageni tusingeweza hata kuishi.

Pili,kama sisi Waafrika tuliletwa ili tuishi katika hii dunia,basi ni mpango wa mungu(nature) tuishi kwa kutegemea uwepo wa watu wengine na ndio maana mpaka leo hii bado wanatutawala na wataendelea kututawala tu kwa miaka mingi.

Vile vile huenda ilipangwa kuwa tutatawaliwa na kuongozwa na wageni kutoka nje ya bara la Afrika mpaka pale tutakapoweza kujitegemea mithili ya mtoto mdogo anavyolelewa na mzazi wake mpaka aje apate akili na uwezo wa kujitegemea.
CC: Robot la Matope
 
Back
Top Bottom