African ladies hair

Jasusi

JF-Expert Member
May 5, 2006
11,551
5,434
nh151009_1.jpg
Kibaki and Karua

Samahani kama nitawakwaza dada zangu wa Kiafrika. Kila ninapotazama picha za wanawake wa siku hizi naona mtindo wa nywele ni zile zilizokaangwa au zile zinazoonekana kama singa za mkia wa farasi. Mfano ni hii picha ya mgombea urais mtarajiwa wa Kenya Martha Karua.
Wanawake wa Kiafrika wana nywele nzuri tu (natural) lakini naona kuna complex na hisia kuwa nywele za kiulaya ulaya ndizo zinazopendeza zaidi.
Ukiangalia picha za walimbwende wengi Dar utakuta ni hizi nywele za kupachikia au nywele zilizokaangwa. Mara chache sana nakutana na mabinti wenye nywele fupi za asili na zinapendeza kwamba I have to take a double look. Kama nilivyosema samahani kama nitawakwaza dada zangu kwa topic hii.
 
Mkuu Jasusi
Bora umelianzisha maana kuna mtu wa karibu sana ana haya manywele, huwa siyapendi ila basi natafuta namna ya kumwambia nashindwa
 
Mambo ya globalization hayo, wanawake nao hatupo nyuma.Wengi siku hizi wanabadilisha nywele zao, wengine watasukia weaving kichwani,watavaa wig, kuna wale wanaweka relaxers.

Kuna baadhi ya wanaume hawapendi wanawake zao kuwa na natural hair, akiwa na natural hair mkewe ataonekana mshamba hiyo nayo inachangia baadhi ya wanawake kuweka artificial hair. Wanaume na nyie huwa mnasifia sana hizi artificial hair, mdada akiwa na hizi nywele bandia umependeza huwa zinakuwa nyingi.
 
nh151009_1.jpg
Kibaki and Karua

Samahani kama nitawakwaza dada zangu wa Kiafrika. Kila ninapotazama picha za wanawake wa siku hizi naona mtindo wa nywele ni zile zilizokaangwa au zile zinazoonekana kama singa za mkia wa farasi. Mfano ni hii picha ya mgombea urais mtarajiwa wa Kenya Martha Karua.
Wanawake wa Kiafrika wana nywele nzuri tu (natural) lakini naona kuna complex na hisia kuwa nywele za kiulaya ulaya ndizo zinazopendeza zaidi.
Ukiangalia picha za walimbwende wengi Dar utakuta ni hizi nywele za kupachikia au nywele zilizokaangwa. Mara chache sana nakutana na mabinti wenye nywele fupi za asili na zinapendeza kwamba I have to take a double look. Kama nilivyosema samahani kama nitawakwaza dada zangu kwa topic hii.

Wewe shauri yako....utaitwa mshamba sasa hivi...

Halafu usiache kumnunulia mkeo hivi viatu na yeye aende na wakati...

Mkuu Jasusi
Bora umelianzisha maana kuna mtu wa karibu sana ana haya manywele, huwa siyapendi ila basi natafuta namna ya kumwambia nashindwa

Kama huzipendi bora umwambie ili ajue huzipendi.Maana yeye atazidi kuwa busy na nywele anafikiri unafurahia.
 
Wewe shauri yako....utaitwa mshamba sasa hivi...

Halafu usiache kumnunulia mkeo hivi viatu na yeye aende na wakati...

Huwezi jua labda ni mtu wa enzi zileeeeee!! Hajui sasa ni 21 century.
 
Wewe shauri yako....utaitwa mshamba sasa hivi...

Halafu usiache kumnunulia mkeo hivi viatu na yeye aende na wakati...

Julius,
Duh! Hivyo viatu mbona ataanguka? Itabidi aende shule ya kujifunza kutembea.
 
Kama huzipendi bora umwambie ili ajue huzipendi.Maana yeye atazidi kuwa busy na nywele anafikiri unafurahia.

Kweli yuko busy, maana kila akipanga kwenda kutengeneza na akirudi lazima anijulishe na mimi huwa sioni tofauti. Napanga namna ya kiungwana ya kumwambia, ila kwa ubize wake najua nitamchanganya sana. Kama kawa lazima nipange matokeo
 
Mara nyingi ni INFERIORITY complex ndio inawasumbua wadada,hata kama mtu ni mzuri kiasi gani lakini bado anakuwa hajiamini alivyo mpaka ajifiche uhalisia wake kwa vitu vingine.
 
Acheni kuwa biased! mbona hamjasema kwamba mnakuwa natural msipovaa nguo, maana nijuavyo mie zamani watu walikuwa wanavaa vimajani kidogo tu. mbona mnvaa nguo mloletewa na wazungu, mbona mnatumia simu za mkononi, mbona mnashave, tena wengine kwa kutumia cream., sasa what is the difference/ si muwe natural na nyie, acheni bla bla and leave women alone, confidence or no confidence they have the right to decide what they want and how they want to look like, mwenye hasira aite polisi.
 
Mmh, lakini sijui kama wote tunajua athari za hizi nywele au huu urembo wa bandia wa kutumia madawa kama yale ya kubadilisha maumbile asilia. ingekuwa vyema tujulishwe athari pengine mtu anaweza kufanya uamzi maana siku hizi humjui yupi mwaume, yupi mwanamke kwa ajili ya huo urembo bandia. yaani ngoma droo.

mmh hatari!
 
vipi kuhusu nywele zilizowekwa dawa? wengine wanakuwa na nywele za kiafrika haswaa zimejaa si mchezo nzito kiama akieka dawa angalau aneza chana zikakaa smart au na hao hawakuvutii????
 
Wewe shauri yako....utaitwa mshamba sasa hivi...

Halafu usiache kumnunulia mkeo hivi viatu na yeye aende na wakati...

kwi kwi kwei
hahahahahahah una hatari mwenzio kasema nywele we unamuongezea catalogue ya viatu
 
Back
Top Bottom