Africa amka, anza kutengeneza majina yako

Africa amka, anza kutengeneza majina yako

mkome

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2017
Posts
378
Reaction score
237
Ndugu wana jamvi,

Nimekaa nikafikiria sana hivi kwanini Africa hatutaki kutumia majina yetu ya asili, ama hivi kweli tumekosa watafiti ama maprofesa ambao wangeweza kutembea nchi nzima kila kabila wakatafiti majina ya asili na maana zake wakatengeza kama kitabu kikubwa cha majina ya asili na maana zake ambayo yangeweza kutumika kiujumla kwa mtu yoyote bila kupata usumbufu wa kuita jina alafu hujui maana yake hiyo ingetupa heshima sisi waafrica.
 
Ukienda kwa wenzetu hutoweza kupata mzungu anaitwa juma , onyango, ama, Mkome, lakini mtu atajiona Wa maana sana kuita jina la kizungu kuanzia jina la kwanza kati hadi la mwisho
 
Tukipata watafiti wakafanya research kwa makabila yote Tanzania kwa kutafsiri majina yenye maana nzuli na kuyaandika angeuza kitabu hicho sana naomba mwenye mawazo mbadala atoe maoni yake
 
Nenda kwa wanyakyusa,wasukuma,wajaluo bado hawajavamiwa kabisa kabisa na utamaduni wa kupachika watoto majina ya kizungu.
 
Majina ndiyo yanakwamisha maendeleo?
Ni moja ya sababu hata bidhaa ikiiywa "diamond" inawezakuuzika sana ila hiyohiyo bidhaa iite"almas" hupati wateja.

Nasibu anajiita "diamond" inatofauti gani na "almas" ulimbukeni ni sehemu ya umaskini wa fikira.

Umasikini siyo wa kipato tu hata fikra
 
Ukienda kwa wenzetu hutoweza kupata mzungu anaitwa juma , onyango, ama, Mkome, lakini mtu atajiona Wa maana sana kuita jina la kizungu kuanzia jina la kwanza kati hadi la mwisho
Wazungu wengi ni wakristo, wanatumia majina ya kikristo ambayo yana asili ya Uyahudi au mashariki ya kati.

Kwa hivyo unaweza kusema katika hili wao ni sawa na sisi tu.

Sema jingine.
 
Si tulibatizwa jina moja waafrika wote "Shitholes"
 
Lengo haswa la Uzi huu ni kufufua majina ya asili na maana yake ili anaependa kuita jina asipate shida kujua maana yake, ama Mimi nataka kuita jina la kinyakyusa isinipe shida kujua maana ya hilo jina
 
Kitengenezwe kitabu maalumu cha kiswahili kama dictionary za majina ya asili ya makabila ya Tanzania na maana zake ili kukuza na kuthamini utu wetu na uwaafrica wetu
 
Una maana gani uzwazwa Mkuu dadavua maada
 
Nani akubali kuitwa majina kama
"cheusi mangara"
"shida sijaona mzuzuri"
"majuto mjukuu""
"masumbuko njaanjaa"..

Ntaendelea kuitwa John James na Mwanangu ataitwa "Angel James John".
 
Nani akubali kuitwa majina kama
"cheusi mangara"
"shida sijaona mzuzuri"
"majuto mjukuu""
"masumbuko njaanjaa"..

Ntaendelea kuitwa John James na Mwanangu ataitwa "Angel James John".
 
Nani akubali kuitwa majina kama
"cheusi mangara"
"shida sijaona mzuzuri"
"majuto mjukuu""
"masumbuko njaanjaa"..

Ntaendelea kuitwa John James na Mwanangu ataitwa "Angel James John".
 
Wazungu wengi ni wakristo, wanatumia majina ya kikristo ambayo yana asili ya Uyahudi au mashariki ya kati.

Kwa hivyo unaweza kusema katika hili wao ni sawa na sisi tu.

Sema jingine.
Wazungu wa wapi unaowazungumzia?
 
Hapana sizungumzii mtu kuitwa cheusi mangara Nina maana kua kuna baadhi ya majina ya kiafrika yana maana nzuli yani utafiti ufanywe yale majina mazuli yenye maana nzuli yatengenezewe kitabu kikubwa ili mtu anaetaka kuita aite,
 
Majina ya kiswahili
Masumbuko
Tabu
Mateso
Matatizo
Dhiki
Nk

Majina
NNgonyani
Katembo
Dindiri
Mbawala
Komba

Majina yetu kwa kifupi yanachekesha sana ukijua the meaning or origin ya majina ya kiafrica na kabadili hili ni ngumu maana u have to mess with some peoples culture ndio maana watu kuondoa hii kero wanajiingiliaga tu google kumaliza mzozo
 
Pamoja na usumbufu huo research ikifanywa Africa ina vitu vingi vimetelekezwa majina yapo mengi yenye maana nzuli , naomba tujikite kwenye point ya msingi ni vipi pakitengenezwa kamusi ya majina ya kiafrica ili kwa yule anapenda jina la kihaya, sukuma, kijita kihehe kikurya basi mtu usipate shida kuita jina unachagua tu Mara moja
 
Back
Top Bottom