Africa amka, anza kutengeneza majina yako

Muongo="Al-Watajamaast: 25428493, member: 15144"]Wazungu wengi ni wakristo, wanatumia majina ya kikristo ambayo yana asili ya Uyahudi au mashariki ya kati.

Kwa hivyo unaweza kusema katika hili wao ni sawa na sisi tu.

Sema jingine.[/QUOTE]
Muongo sana we jamaa
 
Ndugu fikili Mara mbili ukiitwa john na Mzungu kuitwa John unajiona upo sawa na mzungu OK.huo mtazamo wako, kwani ukiitwa mbalawa ama kichuya dini yako itakua imekufa, ama jina zuli toka.kwenye biblia.linaweza kukupeleka mbinguni hapana si kweli msingi Wa imani.ni imani.na.matendo jina halihusiki, ukiitwa mkomora ukaendelea kushika dini yako utapungukiwa nini
 
Lengo haswa la Uzi huu ni kufufua majina ya asili na maana yake ili anaependa kuita jina asipate shida kujua maana yake, ama Mimi nataka kuita jina la kinyakyusa isinipe shida kujua maana ya hilo jina
Unaweza kufufua majina ya asili unavyotaka, lakinibkama hujaweza kuvumbua vitu kuingezea ujuzi wa kisayansi na utekelezaji wa teknolojia itakuwa bure tu.

Nchi za magharibi hazikufika zilipo kwa sababu zilishikilia mila na tamaduni za ulaya.

Zimefika hapa zilipo kwa sababu zimejua kuchukua mambo mazuri ua watu wengine.

Ukisoma chemistry utakutana na majina kibao ya kiarabu ( alkali comes to mind). Ukisoma mathematics utakutana na algebra (mzizi wa kiarabu). Ukimsoma Aristotle utakuta mambo kibao ya mashariki.

Kurudi majina yetu ni kitu kizuri, lakini tusijidanganye kwamba hilo ndilo tatizo letu.

Wazungu waliweza kuendelea hata baada ya Mfalme Constantine wa Roma kutupa dini zao za awali na kufanya Ulaya iwe ya Kikristo. Na sasa wameuufanya Ukristo kuwa dini yao na majina ya Kikristo kuwa majina yao.
 
Tusichanganye dini na majina kwani Mimi nikibatizwa kwa jina la okonkwo ama papii ,ama kabamba , ama shishimbi je nitakua nimeenda kinyume na mzizi Wa dini?
 
Pia kwani ukiitwa petro ndo utaweza vumbua mambo sidhani kama hiyo ni logic
 
Mkuu mtoa mada idea yako ni nzuri sana hiyo nadharia haihitaji professor wala msomi mbobezi hata wewe unaweza kukifanya hicho kitu. Usisubiri kufanyiwa na mtu
Pia kama unataka jina lako litafutwe na kufatiliwa zaidi tengeneza umaarufu hata ukiwa unajiita mavi wazungu watatafuta maana yake.
Ova.
 
Mbona wachina wanatumia majina yao, pia lengo la Uzi huu ni kushea mawazo tu kwamba ikitokea majina yetu ya makabila mbalimbali yakawekwa katika mfumo mzuli itapendeza hivyo yyte anaetaka kuita jina la asili isimpe shida kupata maana, hivyo ningeomba tujikite katika kutaja changamoto zipi zitampata mtu kutengeneza kitu kama hicho
 
Pia wakuu hili ni bonge la idea ikitokea mtu akafanya research hiyo badae akatengeneza kitabu, ama hata application(app) ya majina ya asili na maana yake utauta si wote hupenda kuita majina ya kizungu
 
Wazungu wa wapi unaowazungumzia?
Waingereza, Wafaransa, Wajerumani, Wahispania.

Celts, Welsh, Scots, Anglo-Saxons, Poles, Slavs, Cosacks, etc.

Europe is full of biblical names, biblical names are from the middle east, not Europe.
 
Wachaga sasa jamani ndo wahanga wakubwa wa majina ya kizungu,utaskia, Godlisten,Godliver,Godbless,Godenough,junior,moureen, na mengine mengi mpaka aibu
 
Ukienda kwa wenzetu hutoweza kupata mzungu anaitwa juma , onyango, ama, Mkome, lakini mtu atajiona Wa maana sana kuita jina la kizungu kuanzia jina la kwanza kati hadi la mwisho
Maungo nn
 
Ukienda kwa wenzetu hutoweza kupata mzungu anaitwa juma , onyango, ama, Mkome, lakini mtu atajiona Wa maana sana kuita jina la kizungu kuanzia jina la kwanza kati hadi la mwisho
Maungo nn
 
Jose
Wazungu wengi ni wakristo, wanatumia majina ya kikristo ambayo yana asili ya Uyahudi au mashariki ya kati.

Kwa hivyo unaweza kusema katika hili wao ni sawa na sisi tu.

Sema jingine.
Joseph
Yousef
Yusufu
Jozef
Yosefu
Unaelewa nini hapo Mkuu?
 
hatuna cha kujivunia maana tumepandikizwa utumwa usio kifani, m nashauri Tanzania iwe nch ya kwanza kuupinga umarekani kwa kuanzisha utaratibu wa kuandikisha upya vyeti vya kuzaliwa kwa majina yote ya asili..

Hii itatupa cha kujidaia,laa sivyo yule bwana akiskia hata majina yetu hatuyataki atatutukana zaidi ya hapo.
 
Jose

Joseph
Yousef
Yusufu
Jozef
Yosefu
Unaelewa nini hapo Mkuu?
Joseph Kabila, Joseph Stalin na Joseph Biden wote wametumia jina la kibiblia, la Kiyahudi.

Nchi zao zina mafanikio tofauti sana ya kiuchumi.

Hivyo, majina kama majina tu hayana uhusiano na maendeleo ya kiuchumi.
 
Ndugu wana jamvi,

Nimekaa nikafikiria sana hivi kwanini Africa hatutaki kutumia majina yetu ya asili, ama hivi kweli tumekosa watafiti ama maprofesa ambao wangeweza kutembea nchi nzima kila kabila wakatafiti majina ya asili na maana zake wakatengeza kama kitabu kikubwa cha majina ya asili na maana zake ambayo yangeweza kutumika kiujumla kwa mtu yoyote bila kupata usumbufu wa kuita jina alafu hujui maana yake hiyo ingetupa heshima sisi waafrica.
mkuu binafsi nimekusoma vilivyo,ila kwa sababu jf sk Hz imajaa form four leavers jiandae kubezwa
 
Tanzania iwe nch ya kwanza kuupinga umarekani kwa kuanzisha utaratibu wa kuandikisha upya vyeti vya kuzaliwa kwa majina yote ya asili..
Nadhani itakuwa ya pili.
Mobutu Sseseseko aliwahi kufanya hivyo kipindi DRC ikiitwa Zaire.
 
Tusichanganye dini na majina kwani Mimi nikibatizwa kwa jina la okonkwo ama papii ,ama kabamba , ama shishimbi je nitakua nimeenda kinyume na mzizi Wa dini?
Inategemeana na maana ya hilo jina mkuu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom