Afande Sele akamatwa na polisi kwa kuhusishwa na UKUTA

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,961
xAfande.jpg.pagespeed.ic.SCXkTUCsHD.jpg

Msanii mkongwe wa muziki kutoka Morogoro, Afande Sele amedai anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Morogoro kwa madai anagawa pesa kwa watu ili kuwashawishi wajitokeze katika maandamano ya UKUTA ambayo yamepigwa marufuku.
Rapper huyo ambaye ni mwanasiasa na aligombea ubunge kupitia cha ACT Wazalendo katika uchaguzi uliyopita, amedai yupo mikononi mwa polisi toka jana.

“Huku ni kushindwa kama sio kufeli, toka jana nipo mikononi mwa polisi eti naambiwa nimeratibu mkutano wa UKUTA , nimechapisha T-shirt na kugawa fedha ili kesho watu waandamane, pia kuaandaa mkutano maeneo ya Msamvu.,” aliandika Afande Sele kupitia facebook yake.

Aliongeza, “Nina zaidi ya mwezi sijakaa maeeneo ya Msamvu zaidi ya kupita nikiwa naelekea mikoani tena nikiwa kwenye gari yangu. Ila hii aibu na fedheha kwa jeshi la polisi, maamuzi ya kukurupuka . Tusubiri,”
 
UKUTA na ACT wapi na wapi ........... na UKUTA wenyewe umeahirishwa.
 
Huu uonevu usipopigwa vita utamgusa kila moja wetu kwa wakati wake
 
Yupo mahabusu halafu anatumia fb.
Kama kweli basi polisi mnamuonea afande Sele ela zenyewe za kugawa mtu pori atapata wapi.
 
Atakua alikamatwa na bangi asituchanganyie habari. Tangu lini chama chake ACT kilijihusisha na UKUTA?
 
Afande sele ametoa wapi pesa za kugawa na kuchapisha T-shirts?

Amepewa na nani wakati yeye ni wa ACT isiyohusiana na UKUTA
 
nyie hamjamuelewa. hapo anaelezea kuhusu ukuta wa msamvu stendi. Huyu jamaa nasikia pale msamvu si ndo maskani yake sasa naskia wana kaukuta kao kalibomoka ndo Akawa anagawa pesa kuujenga.
 
Anataka usajili tu uyu UkAWA basi hana lolote na dirisha lishafungwa tayari pole yake
 
Back
Top Bottom