Asubuhi ya leo nilikuwa naangalia tv ya Citizen ya Kenya nikaona Seneta mmoja anayeitwa Sonko. Kavaa hereni, cheni, pete za dhahabu vidole vyote kumi, kapelo la kileo, tsheti kama la mtoto wa kijiweni vile, lakini maneno yaliyokuwa yakimtoka kuhusu rushwa, ufisadi, dhuluma na maonevu dhidi ya raia wa hali ya chini wa Kenya, na mikakati yake ya kuelimisha Wananchi juu ya kukataa mambo hayo na kuyapiga vita, utapenda. Hata maseneta maprofesa hawana hiyo meseji. Baada ya kuchaguliwa kuwa seneta amajiendeleza na sasa ana shahada ya kwanza. Anafanana na Afande sele. Simjui sana Afande huyu kwani muziki sio hobi yangu, lakini pia sipendi kumhukumu kwa muonekano wake wa kitamaduni bali fikra zake, uwezo wake wa kuchambua hoja (critique) na maadili yanayoongoza maisha yake!